Kwenu wazazi mnaosomesha Watoto, Msisitize watoto wasomee Udaktari, Sheria, Engineer ama Uhasibu. Soko la ajira ni gumu ila huku kuna Nafuu

Kuna jamaa kamaliza intern MD mwaka Jana wakapiga lile paper la post intern akafeli juzi nimekutana naye hospital kaja kufunga kidonda kidoleni na aliyekuwa anamfunga kidonda ni mama yake mzazi ambaye ni nesi mstaafu, jamaa alivyoondoka baada ya kumaliza kupata huduma nikamuuliza mama yake kile kidole mwanaye kafanyaje? Mama akanijibu "walikuwa wameenda kufanya kibarua Cha kujenga sasa bahati mbaya tofali likamteleza na kumponda kidoleni" Daah moyo wangu uliumia sana kusikia hayo maneno.
 
chochote unachosoma ni marketable.
shida tunasoma tunavyosoma kwa bahati mbaya, shida nyingine hata tukihitimu hatuwi competent.
 
Bwana mdogo kumbe chalii tu? Unapotoaga nondo kule za kijeshi huwa nadhani ni mtu mzima mwenzetu.

Back to topic umetoa ushauri mzuri siku hizi vijana wasisome kwa kufuata mkumbo au sifa za kozi someni kwa kozi mnazopenda.

Wakati mimi nasoma nilikaa na jamaa alikuwa anasomea graphics na mambo ya kuchora tulikuwa tunamdiss sana kwamba anapoteza muda kusoma usanii.

Asee sahivi ni anapesa sana pamoja na kazi nyingi mno mpaka zingine ana out source. Sisi tukiwa na maisha ya kawaida pamoja na kusomea kozi za kiume.

Mwingine alikuwa kipanga tulisoma nae o level akaenda PCM akafanya vizuri chuo akasoma Electronics Eng. Sahv ni fundi wa computer na ving'amuzi. Sidharau kazi yake lakini ana regret sana mpaka anajificha tusimuone school mate wake.
 
Haah kuna watu wanahisi nina vyeo vya ajabu wakati hamna kitu ndio kwanza naanza maisha
 
Noted loud and clear!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ma Dr wamejaa mtaani kazi hakuna. Wanaofanikiwa wameajiriwa zahanati binafsi Kwa mshahara wa laki 3.5Kwa mwezi.

Wahasibu wamejee mtaani wachoma mihogo ajira hakuna.

Wanasheria wamejaa mtaani kama wote. Watu wanaona kupeleke kesi Kwa wanasheria ni kupoteza muda , njia rahisi ya kutatua kesi ni kurogana tu halafu hutumii pesa na muda mwingi
 
Seen.
 
Seen.
 

[emoji28][emoji28][emoji28] hapo kwenye kurogana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…