Kwenye ajali ya Kariakoo, mmiliki wa jengo awajibishwe ili iwe mfano

Kwenye ajali ya Kariakoo, mmiliki wa jengo awajibishwe ili iwe mfano

Candela

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2021
Posts
817
Reaction score
2,180
Kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo video zinazosambaa inaonesha Jengo halikuwa na underground.

Hivyo mmiliki akaamua kuchimba kuweka maduka chini.

Hii bila shaka haikuhusisha mamlaka na wataalamu maana wasingeruhusu afanye alichofanya.

Naiomba serikali inipr huyu mtu nikae nae ndani siku moja tu halafu nimuachie.

Pia soma
- Waziri Mkuu Majaliwa aagiza Polisi kumtafuta mmiliki wa Jengo lililoporomoka Kariakoo
- Live Updates Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Watu 7 wengine waokolewa
- Waziri Mkuu: Waliofariki kwa ajali ya Jengo kuporomoka wamefikia 16, majeruhi 86
 
Mambo mengi mabaya hutokea kwa sababu ya tamaa.

Mfano ni hiyo ya kuongeza sehemu ya maduka. 👆Tamaa
Meli kuzama kwa sababu ya uzito kupita kiasi. Tamaa
Boda boda kuwa na haraka kimuwahisha abiria ili awahi kurudi kijiweni kumchukuwa yule abilia mwingine aliyempromise. Tamaa

Tamaa, tamaa, tamaa!
 
Kama alikua na vibali vinavyomruhusu kufanya alichokua anafanya kwa nini awajibishwe?.

Tatizo ni Serikali na watendaji wake washaambiwa wale kwa urefu wa kamba yao ndio shida ilipo.

Watu mnafahamu tatizo liko wapi lakini badala mliseme, mnakwepesha kweepesha.

Unapoona familia ipo kwenye matatizo, kisha kiongozi wa familia anakimbilia safari, basi ujue hapo hamna kiongozi.

Mzazi ndio mfariji wa kwanza kwa watoto.

Lakini mwisho wa siku naamini kwenye siasa Kila kitu hutokea kikiwa planed. Ndio maana Wala hawajashtuka. Lengo ni kelele zipungue Ili wafanye Yale wanayoyaona ya muhimu kwao kwa sasa.

Natabiri mwakan kuelekea uchaguzi yatatokea zaidi ya haya.

Mwenyezimungu atusimamie.
 
Wanaopaswa kuwajibishwa ni mamlaka zinazotoa vibali vya ujenzi osha nk hao wapo tu asilimia nyingi hawafanyi kazi zao ipasavyo ukitaka kujua hayo ingia kwenye site yoyote uone uozo unaofanyika Kariakoo ndio zaidi watu wanakufa sana kimya kimya bila kujua haki zao na
 
Kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo video zinazosambaa inaonesha Jengo halikuwa na underground.
Hivyo mmiliki akaamua kuchimba kuweka maduka chini.

Hii bila shaka haikuhusisha mamlaka na wataalamu maana wasingeruhusu afanye alichofanya.
Naiomba serikali inipr huyu mtu nikae nae ndani siku moja tu halafu nimuachie.
Hakuusisha wataalam? Hivi tz unaijua au unaisikia. Hapo wataalam walihusishwa kwa kupewa mlungura.
 
Kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo video zinazosambaa inaonesha Jengo halikuwa na underground.
Hivyo mmiliki akaamua kuchimba kuweka maduka chini.

Hii bila shaka haikuhusisha mamlaka na wataalamu maana wasingeruhusu afanye alichofanya.
Naiomba serikali inipr huyu mtu nikae nae ndani siku moja tu halafu nimuachie.
Hakuna mtu atakayewajibishwa/wajibika.

Nimekaa hapa...
 
Huko ngoja itoke zishuke gorofa 10 kwa wakati mmoja labda akili ndy zitakaa sawa

Ova
 
Yatakuwa yale yale tu. Business as usual.

Kama serikali wako serious ilitakiwa pawe na kariakoo ndogondogo kama 7 nje ya jiji. Ambazo zimepangwa vizuri. Viwanja vikiwa vikubwa na barabara kila upande.

Kariakoo imejaa mno na sio salama. Majengo yapo chini ya kiwango, underground za hatari. Maghorofa yamekaribiana na yamebanana. Viwanja vidogo vimebanana. Ni hatari mno.

Wapo wanasikilizia upepo tu. Hasa mipira na mitandaoni

Back
Top Bottom