Kwenye hili la Mbowe, vyombo vya Dola mmeitwisha zigo Serikali. Hivi hamjui nini?

Kwenye hili la Mbowe, vyombo vya Dola mmeitwisha zigo Serikali. Hivi hamjui nini?

Prof Koboko

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2020
Posts
350
Reaction score
2,550
Bado tunalia sana na weledi wa vyombo vyetu vya Dola hasa jeshi la polisi na TIS. Tunajua kua lengo kuu la kumsumbua Freeman Mbowe si kesi ya Ugaidi wala uhujumu uchumi, lengo kuu ni kuzima Mjadala wa katiba Mpya. Kwenye hili weledi umekosekana na mmeitwisha serikali mzigo utakaoisumbua sana na huenda hali ikawa mbaya zaidi mbeleni. Siamini kama CCM chama kinaweza kufanya mambo kama haya kabisa.

Mhe Freeman Mbowe ni kiongozi mkuu wa Chama kikuu cha upinzani nchini chenye wanachama na wafuasi zaidi milion 11, tofauti ya milion ya milioni 1 na Chama kikongwe cha CCM chenye wanachama na wafuasi milioni 12. Hivi hamuangalii madhara yake? Mmnasukumwa kufanya hata ukitumia hoja ya Uoga wa watanzania bila kujua ni kiongozi gani mmemkamata. Sitaki kuzungumza sana lakini yatazameni madhara yake mbeleni na KATIBA MPYA sasa itaenda kupatikana kupitia mwafaka wa kisiasa tena kwa lazima.

Moja ya Udhaifu mkubwa wa vyombo vyetu vya dola niliyouona na kuamini kua Mashtaka ya Mbowe ni ya uongo na kutunga, ni pale Msemaji wa jeshi la Polisi aliposema hadharani kwenye media tena bila aibu kua Mbowe alikua napanga njama za kuua viongozi wa juu wa serikali, lakini baada ya hati ya mashtaka kuandaliwa hilo jambo halikuwepo tena tukaona kesi ya kupanga kulipua vituo vya mafuta. Sasa Polisi walikua wanadanganya kwa maslahi ya nani na kwa misingi ipi?

Mtakamata wanachama na wafuasi wa CHADEMA nchi nzima, hamjasoma upepo kua kundi litakalofuata ni la wanaharakati ambao wanajua kua Mbowe yupo ndani kwa sababu ya KATIBA MPYA.Mmeitangazia dunia kua haki ya kudai katiba mpya ni Ugaidi. Kukamata mwanachama mmoja wa CHADEMA mnaibua wengine wengi wao na sasa wanachukuliwa kulala polisi ni jambo dogo wamezoea.Maana hakuna kesi mtu kuandamana au kudai katiba mpya, utamkamata kisha utamwachia.

Mmezipa jumuiya za kimataifa attention ya kutufuatilia kwa sababu ya kukosa weledi, hatukua na sababu ya kufika huku. Sina imani kama tutajenga uchumi imara kwa kukosa wahisani na hata sasa tumeshawatishia wawekezaji kua kuna Ugaidi nchini, wanaona ni kama kuna migogoro ya kisasa hawawezi kuja. Mmeitwisha serikali mzigo huu mgumu sana na mzito.

Hiki chama kikiamua kuhamasisha wanachama wake nchi nzima kushinikiza kiongozi wao aachiwe Mtakamata watu wangapi? Mtajaza Magereza nchini wanachama wa CHADEMA nchi nzima? Maana mmeshawapa usugu wanaona kwenda jela kwa makosa madogo kama haya ni kawaida na watatoka. Mkimwachia Mbowe hatokubali bado ataendelea na mbio zake za Katiba mpya.Ndio nini mnafanya sasa kama si kukosa weledi huko?

Rudini nyuma mtafakari kama mnachokifanya ni sahihi kwa mustakabali wa amani ya nchi.
 
Najua mh Mbowe ataachiwa huru; lakini raha ni kuwa katili yule wa kwanza alishazikwa hivyo wengine nao watazikwa tu.
 
Evolution of CCM toka kusimama kwa hoja hadi kwa bunduki.

CCM haiwezi jibu hoja yeyeto ya wapinzani bila msaada wa polisi. Polisi wamekosa weledi wanazidiwa weledi hata police wa Malawi huwezi kuta wanakisaidia chama tawala kujibu hoja za Wapinzani.

Screenshot_20210806_102721.jpg
 
Najua mh Mbowe ataachiwa huru; lakini raha ni kua katili yule wa kwanza alishazikwa hivyo wengine nao watazikwa tu.

Kama alivyotangulia bwana Charles Mbowe na baba yeke mkubwa mzee Mbowe. Na Mwesiga Baregu, kifupi hii dunia habaki mtu.
 
Nashangaa kwanini mpaka SASA hao wanachama 11m wamekaa kimya na Chairman anasota .
 
Kama alivyotangulia bwana Charles Mbowe na baba yeke mkubwa mzee Mbowe. Na Mwesiga Baregu, kifupi hii dunia habaki mtu.
Hatubaki na siku yako ikifika utakwenda tu; lakini furaha itakuja pale tu ambapo uliwatanguliza wenzio kwa mateso ukidhani kua wewe ni mchanga achilia mbali jiwe linaweza kupigwa baruti na kusambaratuka.
 
Back
Top Bottom