Mbatizaji Mkuu
Member
- Jul 19, 2020
- 39
- 128
KWENYE HILI LA SABAYA, CHADEMA INAIFUNZA JAMBO CCM
Anaandika Mbatizaji Mkuu
Unaemwona pichani ni Mdude Nyagali, maarufu kama Mdude Chadema, huyu ndugu alikamatwa na dawa za kulevya kidhibiti kipo na kufikishwa Mahakamani, akafunguliwa mashtaka na hivi karibuni ilikuwa siku ya hukumu yake, hukumu ikaihirishwa.
Ninachotaka kuliongelea hapa sio kwa namna ambavyo alikamatwa na hayo madawa ya kulevya, sikuwepo na sina ushahidi ikiwa ni yake au sio yake, ninachokiangalia hapa ni namna ambavyo Chama chake Cha CHADEMA kupitia viongozi wake wa juu katika chama wanavyompambania ilihali wanajua fika alikamatwa na ushahidi mkononi, ikiwa ni kweli madawa ni yake au lah, wao wamechagua kusimama nae bila kujali chochote.
Ninasema haya nikiwa na picha mbili kichwani kupitia kwa Mdude, huyu kijana alijitolea kukosoa na hata kuvuka mipaka ya ukosoaji na kutoa lugha za kuudhi mitandaoni kwa viongozi wa serikali hata kwa Hayati Dr MAGUFULI, lakini hakuwahi kuachwa na viongozi wake asote mahabusu. Hakutumwa, lakini kwa kuwa alichokifanya alikinasibisha na chama, viongozi wake walimuunga mkono alipopatwa na mkono wa sheria.
Leo akiwa mbele ya hakimu akisubiri hukumu, pembeni yake alikuwemo Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema taifa. Yaani kesi ya mwanachama wa Chadema anaenda Mwenyekiti taifa kuisikiliza. Inafikirisha sana. Kuna la kujifunza hapa.
Sio kwamba Mbowe ameenda kwa kuwa Mdude ni kiongozi katika Chama chake huko juu, bali ameenda kwa sababu ni Mwanachama wa Chadema. Maana ya Mwenyekiti kwa tafsiri rahisi ni mfariji wa Chama, "Party comforter". Mbowe ameenda katika mstari sahihi.
Wakati hayo yakijiri, kuna kijana mwenzetu aliyekuwa DC wa Hai, Lengai Ole Sabaya, yuko mahabusu Kisongo siku ya wiki 2 sasa, sijasikia wala kuona kiongozi wa CCM aliyejitokeza walau kumsemea mazuri Sabaya. Watu wote kimya, Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi iko kimya, ile kauli ya kwamba Vijana ni jeuri ya chama tumeizika kabisa.
Ile kauli ya Mwenyekiti wetu, Kheri James kwamba "Vijana tunahitaji busara ili zitusaidie nini katika umri huu" hatuioni ikitumika hapa la kumsemea ndugu yetu, Lengai alisimama pale Hai kutuwakilisha Vijana wa CCM, alisimama pale kupitia CCM. Amekipa heshima chama cha CCM katika Jimbo hilo, ikiwa alikuwa mbaya na muovu kiasi kile tuliwezaje kumtoa Mbowe kwenye hilo Jimbo?, kwanini tumenyamaza katika hili?
Yaani wamebaki wanaomnanga vibaya Sabaya mitandaoni hasa Wapinzani, kila siku mapya yanaletwa, lakini jumuiya zote ziko kimya, Chama kipo kimya. Leo tunanyamaza kwa huyu, kesho kwa mwingine tutanyamaza au tutaanza kukimbiana?
TUKUTANE MAHAKAMANI LEO, NITAKUWEPO
#JusticeForSabaya
#FreeSabaya