Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Raisi Magufuli ametoa kauli kwamba piga ua VAT kwenye utalii itakuwapo. Kaenda mbali kwa kusema ni afadhali kuwa na watalii wachache wenye kulipa VAT kuliko wengi wasiolipa VAT!
Namheshimu sana Raisi wangu, lakini kuna mambo mengine kama hii biashara ya utalii afadhali awaachie watalaamu wajadiliane na wadau katika sekta hiyo badala ya kutoa kauli za ujumla kama hizi ambazo zinaweza kusababisha mjadala wa hili suala uishe - maana Raisi kishatoa tamko!
Kuna mambo kadhaa niliyoorodhasha hapa chini ambayo ni sababu za msingi kwa nini mtazamo wa Magufuli juu ya suala la VAT kwenye huduma za utalii una makosa sana;
Update: Kipanya kanielewa vizuri sana!
Namheshimu sana Raisi wangu, lakini kuna mambo mengine kama hii biashara ya utalii afadhali awaachie watalaamu wajadiliane na wadau katika sekta hiyo badala ya kutoa kauli za ujumla kama hizi ambazo zinaweza kusababisha mjadala wa hili suala uishe - maana Raisi kishatoa tamko!
Kuna mambo kadhaa niliyoorodhasha hapa chini ambayo ni sababu za msingi kwa nini mtazamo wa Magufuli juu ya suala la VAT kwenye huduma za utalii una makosa sana;
- Suala la kuweka VAT kwenye utalii ikiwa lengo lake ni kudhibidi idadi ya watu wanaoingia katika mbuga zetu ili zisiharibike, basi tunakosea mno kutumia VAT ili kudhibiti hilo. Udhibti huu ungefanywa kwa kuongeza vingilio vya kwenye mbuga, kwa watalii wa ndani na nje
- Kauli kwamba ni afadhali kuwa na watalii wachache wenye kulipa kodi kuliko wengi wasiolipa kodi haina mantiki ya kiuchumi. Na si kweli kwamba hawatalipa kodi kabisa, suala ni kwamba ni kodi ipi na kiasi gani wanalipa. Kumbuka kwamba kupunguza watalii kwa kuongeza VAT kwenye huduma za utalii kunaathiri maeneo mengi mengine, kutia ndani ada za visa kuja Tanzania, mapato yanayotokana na huduma za usafiri wa magari, airport taxes, chakula mahotelini na migahawani, wachukuzi wa upandaji Mlima Kilimanjaro, mapato ya huduma za kulala hotelini, mapato na kodi toka safari za ndege za ndani, ununuzi wa bidhaa za sanaa kama kule Tinga Tinga Oysterbay, nk. Na pia kuna suala linaloitwa "economies of scale" ambalo lazima lizingatiwe kwenye maamuzi kama haya.
- Tuna ushindani katika biashara ya utalii dhidi ya nchi za Kenya, South Africa, Botswana, Rwanda nk. Kusema kwamba hatujali kinachoendelea huko ni "ujinga uliovuka mipaka katika fani ya biashara". Mafanikio katika biashara yeyote yanataka ujue washindani wako wanafanya nini. Hadi sasa washindani wetu wanachekelea sisi kuongeza vitu kama VAT kwenye utalii kwa kuwa wanajua Tanzania tayari ina viwango vya juu vya fee kwenye mambo ya utalii na hii VAT itazidi kufanya watalii waone Tanzania hakufikiki kwa gharama kubwa.
- Ni lazima tusiwe na mantiki ya kitoto kwamba hawa watalii wanaokuja Tanzania au Afrika ni watu matajiri wenye pesa za kutupa tupa tu. Kuna watu wanaamini kila mzungu, au kila ngozi nyeupe inayokuja nchini huyo ni tajiri. Tusitoze kodi kwa msingi huo. Wengi wao ni watu wa kipato cha kati na hata wanafikia hatua ya kula kwa mama nitilie ili kubana matumizi wanapokuja kutalii. Wengi wao wanajibana sana ili kupata fedha za kuja kutalii. Sasa hao ndio tunaowalenga kwenye kusema kama hawataki kulipa kodiya VAT wasije! Hawatakuja si kwa kuwa hawataki kulipa VAT bali kwa sababu wanapotaka kutalii wanaangalia sana wapi kuna gharama nafuu zinazoendana na fedha waliz weza ku-save kwa mwaka mzima au hata maka miwili ili waweze kuja Afrika! Wengi wao lengo ni kuja Afrika, hivyo hawajali kama ni Tanzania, Botswana au South Afrika, wanachojali wapi kuna bei nafuu.
- Kimsingi raia wa kigeni hatakiwi kutozwa VAT. Japokuwa mara nyingi kutotozwa VAT kwa raia wa kigeni ni katika bidhaa za kushikika (tangible goods) badala ya huduma, lakini hata katika suala la bishaa za kihuduma au "consumables" ambazo ni rahisi kumtengansha raia wa kigeni na yule wa hapa nchini, sio haki kumtoza raia wa kigeni VAT.
- Athari za VAT kwenye utalii ikiwa zitapunguza idadi ya watalii, zitapunguza ajira za Watanzania katika sekta ya utalii. Labda Raisi Magufuli hajali ikiwa tunapata watalii wachache nchini. Lakini je, ina maana Raisi Magufuli hajali ikiwa Watanzania wanapoteza ajira zao? Athari za Watanzania kupoteza ajira zao Raisi Magufuli hazielewi? Na ni mara ngapi serikali inaingia gharama kubwa kwa ajili ya kuendeleza ajira kwa wananchi? Sasa je, kuondoa VAT kwenye huduma ya Utalii ili kulinda ajira za Watanzania ni jambo ambalo gharama yake kwa taifa ni kubwa kuliko gharama za Watanzania haokupoteza ajira zao?
- Suala la vivutio vya utalii linaenda mbali zaidi ya kuwa ni mali ya Watanzania.Tunaviita "world heritage" na ndio maana hata kuna jitihada za kimataifa kusaidia kuviendeleza. Japo kwetu ni bashara, lakini hatuna haki ya kuwanyima fursa raia wa kimataifa kuja kuvitemebelea vivutio vyetu kwa sababu nao wana haki navyo, na wengi wao wanatusaidia sana katika kuvilinda, na hata wengine kupoteza maisha yao kati kufanya hivyo. Hatungekuwa na ndovu au faru nchini kama raia wa kimataifa wasingehusika kulinda ndovu na faru hao. Leo hii hatuwezi kusema tutaongeza kodi na hao watalii waje kwetu au wasije hiyo ni shauri yao. Hatupaswi kufanya iwe vigumu kwao kuja kutalii vivutio ambavyo ni "world heritage". Namna moja ya kuwashukuru ni kurahisisha wao kuja kututembelea. Tanzania inajulikana kuwa nchi ya ukarimu. Hatutaki kuwa shamba la bibi, lakini haina maana tuwe wachoyo ili tusiwe shamba la bibi.
Update: Kipanya kanielewa vizuri sana!