Kwenye hili Majizo umezingua

Huwezi kulinganisha pesa kutoka kwenye Matamasha na Youtube views. Kwa Wastani wa Views Milioni 1 Msanii anaweza kutengeneza Tsh. Laki 5 hadi 8, Jiulize ni wasanii wangapi wanaweza kutoa nyimbo zenye kupata 1+ mil Views ndani ya muda mfupi? Linganisha na Msanii akipanda Jukwaani kwenda kupiga playback na makelele ya "Mikono juu, tuimbe wote sasa" then akishuka Jukwaani anakunja milioni mbili/tatu mfukoni.

Mfano kipindi cha nyuma, Tamaduni Muzik content zao zilikua zinatembea sana kwenye digital na mitaani lakini kwenye media huwasikii hata kidogo na ni wachache waliofanikiwa kupata atleast airtime kama akina Nikki, Stereo
Ni kweli walifanikiwa kujitangaza na kufikia walengwa wao, lakini hawakunufaika kiuchumi na ndio maana sasa hivi hata kazi zao(albums) hawaziachii sana kwenye Streaming platforms ila wanaziuza Mkono kwa mkono/E-mail/Whatsapp
 
Yote kwa yote
Majizo hana cha kujifunza kwa mondi ila mondi ana cha kujifunza kwa majizo....
 
Majizo anataka kigezo kiwe kuchezwa kwenye redio yake anasahau kwamba watu wameshatoka huko. Yani Marekani wanatumia Youtube kama kigezo lakini kilaza mmoja bongo aliyebahatisha maisha anawapinga.
 
Majizo anataka kigezo kiwe kuchezwa kwenye redio yake anasahau kwamba watu wameshatoka huko. Yani Marekani wanatumia Youtube kama kigezo lakini kilaza mmoja bongo aliyebahatisha maisha anawapinga.
Majizo kabahatisha maisha[emoji44][emoji44][emoji44]


Kweli kupenda upofu
 
Hayo matamasha yako wapi na Korona hii bro ? Hata kama yangekuwepo ni akina nan wa kupewa 2mil per show? Kwa kuongezea Tu YouTube ndo platform yenye pesa kiduchu kuliko zingine , views mil 39 wimbo wa WAAH umeingiza mil 89 , sasa hv Una views 60 mill sjui iliyoongezeka , ukiachana na YouTube kuna mauzo ya Sportfy na Apple music ndo zenye hela na wimbo wa diamond umeuza Sana nje nafkr ukipewa data zake hela ulizoingiza huo wimbo huenda ni bajeti nzima ya matamasha ya fiesta na Wasafi festival combined together Kwa nchi nzima ...

Whatever the stuation diamond anatengeneza pesa bhana , mzikiii hawajakurupuka kutoa bill 11+ Kwa Wasafi , Sisi wengine wacha tukomae na kilimo Kwanza huenda tutatoboa
 
Ni wasanii wangapi wanaotengeneza hizo Pesa ama kupata Views & Streams kama za Diamond? Kama unamzungumzia Diamond pekee uko sahihi? Ila kama unazungumzia 'Wasanii' fanya utafiti zaidi.
 
Ah huyu usihangaike anashindwa tu kumfata diamond pale wcb akamloge..
 

Majizo yuko sahihi sana

Mno

Labda unaishi kariakoo haujui tandahimba vijijini wanasikiliza redio zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…