Kwenye kampeni mwaka 2015 huko Monduli Magufuli aliahidi kufanya kazi kama hayati Edward Sokoine,-Video

Kwenye kampeni mwaka 2015 huko Monduli Magufuli aliahidi kufanya kazi kama hayati Edward Sokoine,-Video

Richard

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
15,692
Reaction score
23,038
Mwezi April tarehe 12 mwaka 1984 majira ya jioni, watanzania tulitangaziwa habari mbaya za kifo cha Edward Moringe Sokoine ambae alikuwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mtangazaji wa habari hizo alikuwa ni hayati baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Leo ni miaka 36 imepita tangu tumpoteze kiongozi shujaa wa kupambana na ulanguzi, wala rushwa na mafisadi.

Lakini nimepata video ambayo ilikuwa ni taarifa ya habari iloushwa na kituo cha televisheni cha Channel Ten mwaka 2015 wakti wa kampeni ya uchaguzi wa uraisi huko Monduli mkoani Arusha.

Msikilize mgombea wa uraisi kwa tiketi ya CCM na ambae sasa ni raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Joseph Pombe Magufuli kwa manejo yake mwenyewe akiahidi kufanya kazi kama alivyokuwa hayati Sokoine.



Mungu Ibariki Tanzania.

Kumbuka:

Kunawa mikono kila mara kwa maji yanayotiririka na sabuni
Tumia kitakasa mikono au sanitiser
Epuka misongamano na uweke umbali wa mita moja kati yako na mtu mwingine.
Epuka kuzurura mitaani bila sababu maalum
 
Ndo maana hakuna wachangiaji ktk huu uzi siku mbili sasa, huwa inaudhi sana kusifia tu mtu ambaye amefanya maisha yetu wengi yawe dhohofu.
mfano nimesikia wananchi wa uko Arusha wanaomba msaada wa ndoo za maji za elfu20 ili wawe wananawa mikono yao ili kujikinga na korona, imagine wewe mbulula unasifia wkt wananchi elf20 hawana uwrzo nayo, nadhan ungefuatilia ni eneo gani uko ukawape izo ndo kumsafisha na aibu uyo unayemsifia mda wote wakati wananchi wake hawana hata elf20 ya kununulia ndoo ya kujikinga na korona.
Aya yako wazi ww endelea kusifia tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom