Ndugu yangu Malecela, katika hili kuna baadhi ya maswali ngependa unijibu... Hivi ni nani kati ya CCM na Wapinzani aliyedandia swala la katiba? Hivi ni kwa nini CCM haitaki serikali tatu, kuna nini nyuma ya pazia? Hivi ni lini wewe utaitwa Mtanganyika, mbona hii ni Zanzibar na hii ni Tanzania bara? Nini faida na hasara ya muungano, je unafahamu kuwa Zanzibar ni nchi yenye katiba, rais, bendera, bunge n.k? Hivi ni nani kati ya CCM na Wapinzani aliyetumia nguvu nyingi kuunda mabaraza ya katiba? Naomba unapojibu haya ujibu kwa ukweli na sio kwa kusapoti chama. Mungu na akusaidie