Kwenye mamlaka na uongozi wa kisiasa vijana kuna cha kujifunza kwa watangulizi wetu kwamba cheo ni dhamana tu

Kwenye mamlaka na uongozi wa kisiasa vijana kuna cha kujifunza kwa watangulizi wetu kwamba cheo ni dhamana tu

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Yawezekana tuna elimu ya kutosha sana na tumewazidi hata watangulizi na mabosi zetu, yamkini tunafahamu mambo mengi, ni wabunifu na wenye ushawishi mkubwa maeneo fulani kulingana na nafasi, vyeo au dhamana za kimamlaka tulizopewa na mamlaka za uteuzi kwa niaba ya watanzania.

Vijana tunajiamini kupita kiasi, mpaka inafikia mahali kuna kujisahau kulikopitiliza, na kuanza kufanya kazi kwa mazoe, kiburi, dharau, kujisifu, majivuno na kupelekea kujengeka dhana kwa wananchi tunao waongoza kwamba, kwa tabia, misemo, uamuzi na hatua anazochukua uongozini kwake, na mienendo ya kijana yule ni dhahiri amelewa madaraka.

Ni muhimu kujizuia na kujidhibiti na ujuaji mwingi na kijipa umuhimu tusio stahili nao, kuna taasisi zina asili ya wivu kupindukia ni vema kuzijua kitaalamu.

Ni vizuri kuiga hekima, busara na mienendo ya wakubwa zetu na watangulizi wetu uongozini.
kwa kufanya hivyo, ni dhahiri tutachota maarifa mapya na tutakua wepesi hata kusikiliza sauti za matakwa, maoni na mitazamo ya wananchi juu ya masuala mbalimbali ya kijamii, kisiasa na kiuchumi nchini, na hapo ndipo tunaweza kumshauri vyema mh. Rais kwa hatua muafaka za kuchukua...

Mabadiliko ya kiutendaji na kisiasa yanayotukumba, iwe ni somo, fundisho na fursa muhimu sana ya kujisahihisha na kujirkebisha vizuri zaidi katika yale makosa, dosari au kasoro zilizochochea mabadiliko yanayotuhusu.

Hii ni Rai yangu kwa vijana wote nchini walio uongozini na wanao kusudia kua viongozi wa vyama vya siasa, serikalini au kwenye mashirika ya kitaifa na kimataifa, kutambua kwamba cheo ni dhamana na sio zawadi, hisani au njia ya kujinufaisha kibinafsi.

REMEMBER.
#1. Law of Power
NEVER OUTSHINE YOUR MASTER
Always ensure that those above you feel superior. In your desire to impress or please them, do not go too far in displaying your talents or hardwork, you might accomplish the opposite 🐒
 
Kama wangeifuata ahadi ya mwana TANU, baadaye CCM Kwa dhati iliyokuwa inasema cheo ni dhamana, sitakitumia cheo changu Kwa faida yangu binafsi.

Matatizo ya hawa viongozi kujilimbikizia Mali kunapopitiliza kungekoma
 
Back
Top Bottom