Kwenye mapendekezo 21 ya ripoti ya Kamati ya Professor Osoro, yapi yana ukweli, yapi si ya kweli? Tumeshatekeleza mangapi? Makinikia ilikuwa usanii?

Hii ni serikali ya kishetani na kilaghai sana.... ndio maana watz hawaitaki kabisaa.....
 
Kitu muhimu sana ni Watanzania have the right to information the basis ya kumsamehe mwizi wetu!.

Kama deni hilo ni bonafide genuine, serikali inapoamua kusamehe, it got to give reasons. Na baada ya hapo TRA watoe taarifa kuwa wamelifuta deni hilo.

Haya mambo akina sisi tuliyasema sana humu, kama mwanzo tulizuia makinikia kwasababu tulihisi tunaibiwa kwasababu hatujui kilichomo!.

Tukafanya uchunguzi tutathibitisha ni kweli tumeibiwa!. Tukapiga hesabu tulichoibiwa, baba mtu mbio kaja na ahadi wamekubali kila kitu na ili kuonyeshea nia njema wakahidi kishika uchumba cha Dila milioni 300!.

Mwisho wa mazungumzo tukasamehe deni lote, na kuruhusu makinikia yaondoke huku mpaka leo mpaka kesho, bado hatujui kilichomo!.

Kama tulizuia makinikia kwasababu tunaibiwa kwa kutojua kilichomo, tukathibitisha tunaibiwa!, Tumeruhusuje makinikia bila kujua kilichomo?, kwanini tulizuia?!

More explanation on this is needed.
P
 
Duh! Sikuwa nafahamu kuwa makinikia yameruhusiwa kuondoka bado tukiwa hatujui kilichomo. Kwahiyo issue ya makinikia ilikuwa ni usanii. Kama sivyo, Kuna watu wamekula mlungula.

Hii nchi ngumu sana aisee!
 
Duh! Sikuwa nafahamu kuwa makinikia yameruhusiwa kuondoka bado tukiwa hatujui kilichomo. Kwahiyo issue ya makinikia ilikiwa ni usanii. Kama sivyo, Kuna watu wamekula mlungula.

Hii nchi ngumu sana aisee!
Kuna vitu vingine kiukweli...
  1. Yaani wewe uzuie makinikia kwa hoja tunaibiwa kwasababu hatujui kilichomo
  2. Kisha wewe uunde tume mbili kuchunguza
  3. Matokeo ya tume zote mbili yakathibitisha tunaibiwa.
  4. Ukakasirika sana na kuahidi kamwe makinikia hayataondoka na kuanzia sasa yatachenjuliwa nchini.
  5. TRA wakaleta tax bill inayotosha kumnunulia Noah kila Mtanzania.
  6. Baba wa mwizi wetu akatua nchini kwa mazungumzo na kuahidi kishika uchumba cha dola milioni 300
  7. Mazungumzo ya tax bill yakaanza
  8. Mazungumzo yakaisha mkakubaliana kusamehe deni lote!.
  9. Pia makinikia yakaruhusiwa kuendelea kutoka huku hatujui kilichomo
  10. Hakuna issue yoyote ya kuchanjua makinikia nchini!.
Mwacheni baba wa watu apumzike kwa amani huko peponi alipo.
P
 
Nasisitizi, wote waliotajwa wamechunguzwa, waliokutwa na washitakiwa na wamehukumiwa. Hao ambao sijasikia ujue wamechunguzwa wakakutwa hawana hatia!.

P.
Waliohukumiwa ni nani na nani?
 
Hii ni hatari kuliko hatari yenyewe...

Unajua ukiwa unafanya jambo hutakiwi kuwa na mihemko au kukurupuka..

Issue ya makinikia ilikuwa aibu ya nchi
 
Hii ni hatari kuliko hatari yenyewe...

Unajua ukiwa unafanya jambo hutakiwi kuwa na mihemko au kukurupuka..

Issue ya makinikia ilikuwa aibu ya nchi

Usiefahamu mambo utasema hivi.

Ila Ulikua ushujaa usio wa Kawaida kupata walau 16%

Mwizi alikubali yaishe huku akitoa Ofa kadhaa ikiwemo Maabara, Ujenzi wa Barabara 2 , na Pia Kuanza kulipa Kodi stahiki , Kampuni iwe na Ofisi hapa ( Zamani ilikua London)

Ni Vigumu sana kuelewa nini maana ya Majadiliano
 
Mkuu...

Unajua shughuli za migodi zilifungwa kwa karibu mwaka mmoja na miezi kadhaa kwa ajili ya ripoti hii ya kusadikika?

Unajua maelfu ya watu walikaa nyumbani hasa kanda ya ziwa.. Shughuli nyingi za kiuchumi zilisimama.... (multiple effects zilitokea)?

Unajua hata kama ripoti inatengenezwa.. Inatakiwa angalau asilimia 40 iwe na uhalisia? Hivi unajua maana ya kodi sh tril 360 ? Yaani kiufupi tuseme miaka 18 hizo kampuni zimevuna madini zaidi ya tril 5000? Ili sisi tuweze kudai tril 360...
Unajua tusijitoe ufahamu kwa neno UZALENDO.. ambalo lilitumika kijinga wakati huo...

Hiyo asilimia 16 tusingeweza kupata kwa majadiliano mpaka tufunge shughuli za migodi miezi 15....? Unajua Serikali ilipoteza kiasi gani cha PAYE kwa maelfu ya wafanyakazi kukaa nyumbani.?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…