Wanajamvi, nadhani suala hili, halikuzungumziwa vya kutosha hata kidogo. Lissu yeye alishaumizwa na wengine walitishika kabisa kulizungumzia!
Hata hivyo, bado limezungumziwa sana na makada wa CCM hata humu ndani. Mfano kina Pasco! Lakini kwa namna ya uongo na propaganda nyingi.
Ripoti yenyewe imelalamika zaidi kuhusu kodi, na ikapendekeza uwepo uwajibikaji kwa watumishi mbali mbali wa ngazi tofauti za serikali kutokana na misamaha ya kodi kwa makampuni hayo!
Ya kuhusu makinikia, hapo hakukuwa na lolote! Hata kile ambacho kada maarufu wa chama humu
Pascal Mayalla, alikuja na uongo mwingi sana humu kuhusu kile alichokiita “kishika uchumba”. Lakini ukifuatilia kwa makini, utagunduwa kuwa hata hicho kilicholipwa na Barick kwa niaba ya ACACIA, walilipa tu ili thamani ya hisa zao, isiendelee kushuka kwenye soko la dunia, pamoja na gharama zinazotokana na kuzuiwa kwa makontena hayo, habari kuwa yamezuiwa, ni mbaya zaidi kwa uchumi wa kampuni kuliko kuwndelea na kesi MIGA! Lakini hakuna nilichoona kwamba wamekubali kuwa wamefanya chochote kile kinyume na mkataba ambao ni CCM waliusaini.
Sitaki kuzungumza mengi, nitayaleta mapendekezo yote hapa, kisha tuyachambuwe, kwasababu uchaguzi umekaribia, sasa tujulishane ukweli ili tujuwe kama tuwape kura au tuwapumzishe.
Maana mojawapo ya mapendekezo, ni sisi kuifahamu mikataba, na wale walioisaini na kuipitisha, wawajibike, lakini naona usanii tu huku wapinzani wakisingiziwa na Lissu wa watu.
Pia kamati ilipendekeza kuwa “Serikali ifanye uchunguzi na kuchukua hatua za kisheria, dhidi ya waliokua mawaziri,wanasheria wakuu wa serikali na manaibu wao, wakurugenzi wa idara za mikataba na makamishna wa madini, wanasheria wa Wizara ya madini na watumishi wengine wote waliohusika katika kuingia mikataba ya madini.“
Hapo chini, ni kasehemu ka ripoti hiyo ambayo iliitwa “rubbish” ama takataka ya kiprofesa! Ukiisoma kiukweli ni uongo mtupu! Na ndiyo maana tukalipwa kile
Pascal Mayalla alichokiita kuwa ni “kishika uchumba”, yani pesa ama gharama za kumzuilia “mwali”, ama mchumba pale bandarini! Ambapo hicho kishika uchumba cha usd 300m, kilitolewa na Barrick, siyo kwasababu eti wamekubaliana na hiyo ripoti, bali ni kwasababu wanaendelea kupata hasara, khasa kwenye thamani ya hisa zao, ambapo wote tunafahamu kuwa taarifa kama hizo huwa zinaathiri thamani yake kwenye soko la dunia! Lakini kama wangelazimishwa kulipa hicho kiasi kilichotajwa, basi ni kweli MIGA ingehusika! Na hapo ndipo point ya Tundu Lissu ilipokuwepo!
Hapo chini ni sehemu hiyo, nimepunguza vipengele vya madini waliyosema yamo ndani ya makinikia! Vipengele hivyo...
“4. Kwa ujumla thamani ya metali/madini yote katika makinikia kwenye makontena 277 yaliyozuiliwa bandarini, ni TZS bilioni 829.4 kwa kutumia viwango vya wastani na TZS bilioni 1,438.8 kwa kutumia viwango vya juu. Kwa kuwa viwango hivi vya thamani havitumiki kukadiria mapato ya Serikali, ni wazi kuwa kuna upotevu mkubwa sana wa mapato kwa nchi yetu.
5. Thamani zote za madini kwenye makinikia yaliyo ndani ya makontena zilizoainishwa hapo juu, zimepatikana kwa kutumia uzito wa wastani wa tani 20 za makinikia kwenye kila kontena. Hata hivyo, katika kupima uzito wa makinikia ndani ya makontena, kuna makontena kadhaa yaliyokuwa na uzito zaidi ya tani 20 za makinikia, kwa mfano makontena yenye namba CAIU 2461301, TCLU 0701267, MRKU 6880530 na MSKU 4280570 yalikuwa na makinikia yenye uzito wa tani 23.1; 22.9; 22.7 na 22.2, kwa mtiririko huo. Hivyo basi, ongezeko hili la uzito linaongeza thamani ya makinikia na hivyo kuongeza upotevu zaidi wa mapato ya Serikali.
6. Pamoja na kuchunguza makinikia, Kamati pia ilichunguza shehena ya mbale za copper ndani ya makontena matano (5) yaliyozuiliwa bandarini. Sampuli za mbale hizo zilipatikana kuwa na viwango vya dhahabu hadi kufikia 38.3 g/t, viwango ambavyo havikuoneshwa kwenye ripoti ya upimaji wa kimaabara wa TMAA, na hivyo kutotumika katika kukokotoa malipo ya mrabaha Serikalini.”
Ripoti ya uchunguzi wa mchanga wa madini. (Ripoti ya Osoro na Mruma)
cc
Nguruvi3
Je, wajua kuna uwezekano Barrick wanatuingiza mkenge?!. Hili la kugawana 50/50 ya faida ni kweli au ni changa la macho tu?.
Update: 22/8/2020
Baada ya hotuba hii ya Lissu, sasa nime connect the dots kuwa yote niliyosema ni ya kweli.