Kwenye mapendekezo 21 ya ripoti ya Kamati ya Professor Osoro, yapi yana ukweli, yapi si ya kweli? Tumeshatekeleza mangapi? Makinikia ilikuwa usanii?

Kwenye mapendekezo 21 ya ripoti ya Kamati ya Professor Osoro, yapi yana ukweli, yapi si ya kweli? Tumeshatekeleza mangapi? Makinikia ilikuwa usanii?

Hapana! Hawa sio wajinga bali ni wapumbavu kwa sababu maandiko yao yanaonyesha wanajua wanachokiandika!
Mkuu si uonyeshe huo werevu wako ili sisi wapumbavu tuonekane huo upumbavu wetu? Maana mtu hawezi kuwa mpumbavu kwasababu wewe tu umesema, who are you?
 
Huwezi kuona chochote, huoni ndio maana Paskali kaishia kupanick baada ya kuona watu wanahoji yasiyokuwa na majibu?
Yalikuwepo jana tu, toka siku naanzisha hii thread, mwenye hiyo link inaonekana kapita hapa! Labda ameogopa asitumbuliwe, au labda amoena imegeuka dhidi yao badala ya kuwa ni propaganda!😀🤦🏾‍♂️
 
chagu wa malunde , nimepata source nyingine. Njoo hapa mkuu...Pamoja na kwamba hii source imesema “unsecured”, potelea mbali, nimeipakuwa hivyo hivyo tu!😀


MAPENDEKEZO YA KAMATI



1.Hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya Acacia



2.Serikali idai kodi na makampuni yote yaliyokwepa kodi!.



3.Usafirishaji wa makinikia usitishwe mpaka kodi ilipwe



4,Mtambo wa kuchenjua makinikia ujengwe!.



5.Waliohusika wote katika kuingia mikataba wachukuliwe hatua za kisheria!.



6.Utaratibu wa malipo ya mrahaba ufutwe!.



7.Serikali ifanye uchunguzi kuhusu mwenendo wa watumishi wa mabaraza ya kodi!.



8.BOT ifuatilie malipo ya mrahaba



9.Serikali ianzishe utaratibu wa ulinzi kwenye migodi



10.Adhabu za waliokiuka sheria ziongezwe!.



11.Mikataba yote ya madini ipitiwe upya!.



12.Sheria iweke kiwango maaluma cha hisa!.



13.Serikali iunde chombo cha kusimamia ustawishaji wa biashara!.



14.Sheria iseme madini ni malinya watanzania chini ya udhamini wa rais



15. Mikataba yote iwe wazi



16.Madaraka ya waziri na kamishna yapunguzwe!.



17.Suala la ajira na mafunzo kwa wazawa izingatiwe!.



18.Fedha za mauzo ya madini ziwekwe kwenye mabenki!.



19.Serikali ifute ama izifanyie marekebisho kwenye sheria za kodi na madini!.



20.Serikali itoe mafunzo ya mara kwa mara kwa watumishi wake!.
Prof. Osoro : Mapendekezo 20 ya Kamati ya Pili ya Kuchunguza mchanga wa ...
 
Maendeleo ya nchi yanahitaji mipango. Ukilazimisha unapata hasara. Zote hizi ni propaganda tu! Wao ndo wamesaini mikataba na hata sasa ni siri bado!
Lazima ufahamu kuwa alichokifanya jpm ni kujitoa muhanga kuamua kumtia kashkash simba aliyevamia zizi la mbuzi ili angalau ajeruhi tu,tungemfuata lissu tusingefanikiwa,hii ni mfano wa sheria za madai MTU ukimdai anakuzungusha,sheria ipo inataka uhende mahakamani lakini kuipata itakuwa ni story,ila ukimvutia kwa afande fasta inatoka kila mtu anaendelea na mingo .
 
chagu wa malunde , hii hapo chini, ndo lilikuwa pendekezo la kwanza nililokuletea jana. Lakini kwenye hii link nyingine, pendekezo la kwanza ni kuichukulia hatua kampuni ya Acacia. Anyways, tutaendelea tu mbele na hiyo link mpya...


1. Serikali iendelee kusitisha usafirishaji mchanga wa madini “makinikia” nje ya nchi mpaka pale mrabaha stahiki utakapolipwa Serikalini kwa kuzingatia thamani halisi ya makinikia kama ilivyoainishwa kwenye uchunguzi huu.
 
Lazima ufahamu kuwa alichokifanya jpm ni kujitoa muhanga kuamua kumtia kashkash simba aliyevamia zizi la mbuzi ili angalau ajeruhi tu,tungemfuata lissu tusingefanikiwa,hii ni mfano wa sheria za madai MTU ukimdai anakuzungusha,sheria ipo inataka uhende mahakamani lakini kuipata itakuwa ni story,ila ukimvutia kwa afande fasta inatoka kila mtu anaendelea na mingo .
Amejitoa muhanga kivipi na wakati makosa tulifanya sisi wenyewe? Umesoma na kuelewa vyema? Au umelishwa propaganda?

Shida ilikuwa kwa viongozi waliowawezesha Acacia kukwepa hizo kodi! Lakini kitu kiliwaokoa serikali, ni kitendo cha Barrick kuingilia kati, na hii ni kwasababu walijaribu kusema ngoja wakae chini kuyamaliza, ili kwamba thamani ya hisa kwenye soko la hisa isiendelee kushuka. Kwa wanaofahamu umuhimu wa taarifa kwenye soko la hisa wanajuwa hili! Na ndiyo maana hata kipindi kuna habari za ugaidi, hisa za makampuni mengi tu zinashuka chini!

Sasa kilichofanyika, ni Barrick kuona pesa inayohitajika ni ndogo kuliko ile ya ma trillion iliyotolewa hapo awali. Acacia wao upande wao walishaamuwa iwe mbaya na wanaendelea kupambana!

Sasa wewe ndo useme kama hayo mapendekezo 21 yanaonyesha huko kujitoa muhanga? Na yenyewe yamefuatiliwa? Matokeo yake ni chanya? Pesa zilizotolewa, utofauti wake unaonyesha huo muhanga? Nini kina kufanya useme “alijitoa muhanga”?

Hapa ni maswali na majibu kwanza.
 
chagu wa malunde , nimepitia hii link mpya, sasa nimefikia namba 15. Hayo mengine mengi ni uongo uongo tu.

15. Mikataba yote iwe wazi

hapo vipi? Mbona mikataba haiko wazi?
 
Una uhakika haujapekekwa bungeni? Maana hata sheria ya 2017, Natural wealth and resources contract(review and negotiationa of unconsciable terms m) Act. Inasema bunge ndio inatakiwa ijadili hii mikataba iliyo na mapungufu.
 
Yanayotekelezeka ni mangapi?
Utakuwa unarudi kinyumanyuma wakati uliomba msaada kwenye tuta na Pasco akakusaidia. Nimeshakuambia baada ya mazunguzo ya serikali yetu na Accacia kukwama juu ya kodi ya usd bil190. Barrick waliingilia kati wakaiuza Accacia na wakaahidi kutoa Bil 700 kama kishika uchumba. Baada ya hapo mazungumzo yalilejea na ikazaliwa kampuni inayoitwa Twiga minerals ltd. Ambayo imesababisha mgogoro kuisha. Hayo mapendekezo ya Prof Osolo achana nayo. Unajiabisha maana unazumguzia suala ambalo ni hadithi tena.
We shukuru sasa hivi serikali yako ina 16% ya share za Twiga gold ltd na huku ikipata economic benefits 50%.
Na sio jambo dogo sababu mtaji wa kuendesha kampuni anautoa Barrick.
Kwa hiyo uwe unajipanga kudadavua mambo kabla ya kuleta lawama.
 
Back
Top Bottom