Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
KWENYE MASHINDANO YA BONGO STAR SEARCH USITEGEMEE KUSHINDA KAMA UTAIMBA NYIMBO ZA BONGOFLEVA ALAFU WENZAKO WAIMBE ZA KIZUNGU.
Anaadika, Robert Heriel
Mtibeli
Juzi nilikuwa Mbweni kwenye finali ya BongoStar Search(BSS). Nampongeza Madam Rita kwa kupambana katika project yake hiyo ambayo imekuwa msaada mkubwa kwa vijana wengi wa kitanzania ambao wengi wametoka familia maskini.
Madam Rita ni moja ya wanawake wa mfano kwa nchi yetu wakuigwa.
Nirudi kwenye hoja.
Lengo la Bongo Star search ni kusaidia vijana wakitanzania kupata forum ya kuibua vipaji vyao hasa vya uimbaji. Hivyo inatarajiwa mshindi awe ni kijana wa kitanzania. Kwani hilo ndilo lengo.
Jambo hilo pia lilileta utata kwenye kutangaza mshindi.
Mshindi namba moja ambaye ni binti Mdogo Praise Wisdom ambaye nilimjua siku ya Finali kutokana sikuwa mfuatiliaji wa maonyesho hayo.
Aliimba vizuri sana.
Hakukuwa na namna ya kumzuia Praise asiwe mshindi labda tungeingiza siasa kwamba Zawadi na pesa zote hizo anapaswa achukue kijana wetu wa kitanzania ili hela ibaki ndani.
Lakini Madam Rita aliamua kubaki na msimamo na haki itendeke na ilitendeka.
Ninachotaka kusema, kama haya mashindano ya bongostar Search yatakuwa ya East Africa kwa kuhusisha nchi Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Congo, Sudan na Tanzania. Basi vijana wetu wanawakati mgumu sana kupata ushindi namba moja.
Hizo milioni 50 kila wakati zinahati Hati ya kwenda nchi jirani.
Kwa sababu Wabongo wengi hatujui kingereza na lugha za kimataifa.
Huwezi shinda shindano la uimbaji kwa kuimba nyimbo za bongofleva bhana, nyimbo za singeli, nyimbo za taarabu, nyimbo za kina Zuchu.
Sio kwamba ni nyimbo mbaya, hapana. Ni nyimbo nzuri lakini hazipo kwenye level za kuwekwa kwenye mashindano ya kushinda kimataifa.
Hata yule mshiriki wa Congo aitwaye Joshua alibutuliwa na kushindwa kuingia top 3 kutokana na kujiingiza kuimba nyimbo za kiswahili ambazo nyingi ni ordinary. Hazipimi quality mwimbaji.
Nyimbo za mashindano zinahitaji ziwe na key za juu, kupanda sauti kwa muda, kuzishusha kuziyumbisha, sasa nyimbo gani utaimba ikupe ushindi.
Nyimbo mfano wa zile za Whitney Houston, Celine Dione n.k. nyimbo za kina Rkelly.
Wewe unaimba singeli au nyimbo za kina Dudubaya au Twente percent ambazo ni nzuri lakini haziko kimashindano.
Unapokuja kwenye mashindano ya kuimba lazima ujue sauti ni kitu muhimu sana kuonyesha sauti yako sio ya kawaida, kisha kufuata nota za muziki, kisha kutawala jukwaa, kisha muonekano wako na kuonyesha hisia(kuuvaa wimbo), mwisho kuwa na nidhamu wakati unaimba. Sio muda wa kuimba umeisha wewe unakazana kuendelea, au unashangiliwa unajawa na mihemko unapoteza focus.
Vijana wa kibongo hapa tutakuwa na mlima mrefu hasa kwa sisi tusiojua kingereza lakini tunakipaji cha kuimba. Tukiimba tutaonekana wa kawaida.
Kingine, kwa yule dogo aliyeshika nafasi ya Pili, Aitwaye So fire. Yule Amefika nafasi ya pili kimakosa kutokana nafikiri ni shinikizo la mashabiki kumshangilia.
Lakini kimsingi hakupaswa kuwa namba mbili.
Unapoleta mashindano ya uimbaji mtu anayerapa hata siku moja hawezi mshinda muimbaji. Never.
Rapa anaweza kufanya yeyote lakini kuimba ni kwa wachache.
Hii inamaanisha Waandaji wa BongoFleva wanatakiwa waweke Category katika uimbaji. Kwani Rapa hawezi kushinda mbele ya waimbaji.
Madam Rita project yako ni nzuri lakini usisahau lengo ni kuinua vijana wa kitanzania. Ukizangatia wadhamini pia ni makampuni ya kitanzania.
Hivyo ni vizuri kujua kama umeamua kualika nchi jirani basi ujue watoto na vijana wako wa kitanzania wanachangoto ya kingereza.
Na ikiwa ni hivyo wakiimba watasikika kama local artists huku majirani wakiimba zile za kingereza watasikika kama international artists.
Nimemaliza.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam