sepema
JF-Expert Member
- Jun 13, 2019
- 591
- 1,001
Salaam kwenu,
Niko kwenye ndoa mwaka wa 8 saivi na tumejaaliwa kuwa na watoto wawili. Mimi na mwenzangu tumeajiriwa Kwenye taasisi moja ya umma japo kwenye vituo tofauti.
Mwezi huu kukatokea agizo la kuhuisha taarifa za wafanyakazi ili ziwe za kisasa na halisia kuliko mwanzo.
Zoezi hili lilihusisha urekebishaji wa baadhi ya taarifa zilizopo kwenye mikataba ya wafanyakazi ambayo waliijaza walipoajiriwa.
Kwa kuwa wakati tunaanza kazi hatukuwa na familia, sehemu ya warithi kwenye mikataba tulikuwa tumeweka wazazi na ndugu zetu. Sasa kutokana na kuwa na familia tulichopanga mimi na mwenzangu ni kwamba kwenye maboresho tujiandike sisi wenyewe Kama warithi wa kwanza pamoja na watoto wetu. Mimi kwenye mkataba nikamweka mke na watoto wangu Kama tulivyokubaliana.
Nimekuja kushtuka baada ya kuona mkataba wa mke wangu ambapo yeye kamwandika baba yake mzazi pamoja na watoto. Mimi hakuniandika kabisa.
Mkataba wake nimefanikiwa kuuona baada ya kuongea na mhusika aliyekuwa anaikusanya Kisha kuipeleka sehemu husika. Hadi sahivi mke hajui kwamba nimegundua kitendo hicho.
Najiuliza, hili tukio mke kalifanya kwa makusudi au bahati mbaya.
Au kitaalam sio lazima mwanamke kumwandika mumewe Kama mrithi?
Je, niendelee kujifanya sijui au nimuulize nijue nia yake ya kufanya hivyo?
Wasalaam!