Salaam kwenu
Niko kwenye ndoa mwaka wa8 saivi na tumejaaliwa kuwa na watoto wawili. Mimi namwenzangu tumeajiriwa Kwenye taasisi moja ya umma japo kwenye vituo tofauti.
Mwezi huu kukatokea agizo lakuhuisha taarifa za wafanyakazi ili ziwe zakisasa na halisia kuliko mwanzo.
Zoezi hili lilihusisha urekebishaji wa baadhi ya taarifa zilizopo kwenye mikataba ya wafanyakazi ambayo waliijaza walipoajiriwa.
Kwa kuwa wakati tunaanza kazi hatukuwa na familia, sehemu ya warithi Kwenye mikataba tulikuwa tumeweka wazazi na ndugu zetu. Sasa kutokana nakuwa na familia tulichopanga mimi na mwenzangu nikwamba kwenye maboresho tujiandike sisi wenyewe Kama warithi wakwanza pamoja na watoto wetu.Mimi kwenye mkataba nikamweka mke na watoto wangu Kama tulivyokubaliana.
Nimekuja kushtuka baada ya kuona mkataba wa mke wangu ambapo yeye kamwandika baba yake mzazi pamoja na watoto. Mimi hakuniandika kabisa.
Mkataba wake nimefanikiwa kuuona baada ya kuongea namhusika aliyekuwa anaikusanya Kisha kuipeleka sehemu husika.Hadi saivi mke hajui kwamba nimegundua kitendo hicho.
Najiuliza,hili tukio mke kalifanya kwa makusudi au bahati mbaya.
Au kitaalam sio lazima mwanamke kumwandika mumewe Kama mrithi?
Jee, niendelee kujifanya sijui au nimuulize nijue nia yake yakufanya hivyo?
Wasalaam!