Kwenye mkutano wa ACT-Wazalendo Lindi hakukuwa na Mwananchi mwenye Elfu 10 mfukoni. Halafu tunaambiwa tuna Uchumi wa Kati

Kwenye mkutano wa ACT-Wazalendo Lindi hakukuwa na Mwananchi mwenye Elfu 10 mfukoni. Halafu tunaambiwa tuna Uchumi wa Kati

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Posts
34,188
Reaction score
62,952
Bernard Membe aliuliza wananchi waliohudhuria mkutano wake kuhusu fedha walizonazo mfukoni.

Katika wananchi waliohudhuria mkutano ule wa kampeni hakuna aliyekuwa na shilingi elfu 10 mfukoni mwake.

Wakati huohuo serikali inajigamba kwamba tumepanda daraja na kufikia uchumi wa kati.

Kwa kweli CCM, Dkt. Magufuli, na Serikali, wako out of touch na hali halisi ya maisha ya Watanzania.

Propaganda walizokuwa wakieneza zimeanza kuwaathiri hata wao wenyewe.
 
Wahudhuriaji wengi wa hayo mambo ndio walivyo, Watu hawawezi kuacha ofisi au biashara Mkuu.

..unaposema uchumi wa kati maana yake hata mwananchi wa kawaida ameguswa.

..sasa mkutano wote ule anapokosekana mtu mwenye elfu 10 ujue kuna tatizo ktk hii dhana ya uchumi wa kati.
 
Jokakuu,

Swala la nchi yetu kuingia uchumi wa kati sio tamko la Serikali yetu wala CCM ila ni tamko la World Bank

Hvyo kama una pingamizi, manung'uniko, sikitiko, kisununu, miwasho miwasho, kiraruraru basi wapigie World Bank kwa hii namba +1 202-473-1000
 
..mimi nilimsikia waziri wa fedha, Dr.Mpango, akitoa taarifa hizo kwenye vyombo vya habari.

..pia bungeni mawaziri na wabunge wa ccm waliendelea kuzishabikia habari hizo.

..hivyo ni kweli taarifa zilitolewa na WB, lakini ccm na serikali wamefanya makosa kuzishabikia kana kwamba zina uhalisia ktk maisha ya waTanzania.
 
Kazi ya mwananchi n
..Bernard Membe aliuliza wananchi waliohudhuria mkutano wake kuhusu fedha walizonazo mfukoni.

..katika wananchi waliohudhuria mkutano ule wa kampeni hakuna aliyekuwa na shilingi elfu 10 mfukoni mwake.

..wakati huohuo serikali inajigamba kwamba tumepanda daraja na kufikia uchumi wa kati.

..kwa kweli ccm, magufuli, na serikali, wako out of touch na hali halisi ya maisha ya waTanzania.

..propaganda walizokuwa wakieneza zimeanza kuwaathiri hata wao wenyewe.
Kazi ya mwananchi ni kupata huduma kutoka kwa wagombea na sio kazi ya wananchi kuwachangia pesa kisha wakishida hata msaad binafsi hawatoi.
 
Watu wenye uchumi wa Kati hela zao wanaweka bank ndio maana hawakuwa nazo mfukoni. Zitakuwa ziko kwenye macrdb yao huko
 
Jokakuu,

Swala la nchi yetu kuingia uchumi wa kati sio tamko la Serikali yetu wala CCM ila ni tamko la World Bank

Hvyo kama una pingamizi, manung'uniko, sikitiko, kisununu, miwasho miwasho, kiraruraru basi wapigie World Bank kwa hii namba +1 202-473-1000
Data wanapewa na serikali ya ccm.
 
Uchumi wa Kati lkn wananchi wengi walishasahau kunywa chai, ni mlo mmoja tu Tena wa kubahatisha
 
Ni kweli, nilikuwepo lakini mfukoni nilikuwa na buku mbili tuu...
CCM ni kuibana tu kwenye "facts" ndipo ubabaishaji wao utakapo eleweka. Katika kipindi cha kampeni huvaa sura za kinafiki na kuanza kutoa kauli zenye kutoa matumaini na hata kujifanya ni watu wenye kujali na wapo karibu na matatizo ya Watanzania.

Kampeni zikiisha tu huchakachua matokeo ya kura na kuiba ushindi wa yule ambaye amechaguliwa kidemokrasia, huanza kujawa na kiburi cha uzima, huwasimanga watu na kuwafanyia kila aina ya udhalimu na ufedhuli kwa kuwa mioyoni mwao hutambua kuwa waliwakataa ktk sanduku la kura.

Viongozi hawa hatambui kabisa pale inaposemwa; "Truth without love is cruelty, and love without truth is hypocrisy"
 
Ukienda vijijini huna change ya elf 10 utalala njaa, wawezazunguka Kijiji kizima unatafuta change ya elf 10
 
Data wanapewa na serikali ya ccm.

..Hold on!!

..kwa hiyo inawezekana kabisa serikali ya Magufuli wamewapa WB data za uongo zilizopelekea tukapandishwa daraja.

..kwa kweli sikuwahi kulifikiria suala hili ktk angle hiyo.
 
Jokakuu,

Swala la nchi yetu kuingia uchumi wa kati sio tamko la Serikali yetu wala CCM ila ni tamko la World Bank

Hvyo kama una pingamizi, manung'uniko, sikitiko, kisununu, miwasho miwasho, kiraruraru basi wapigie World Bank kwa hii namba +1 202-473-1000
Hao World Bank wakimkuta Saniniu Mount Meru Hotel "kachafua meza" wanasema Watanzania wapo njema.
 
Kwa sababu hakuwepo mwenye noti ya elfu kumi basi hatujafikia uchumi wa kati!!.

Very weak argument.

Kule Los Angeles kuna watu wanaishi ndani ya maboksi pembeni ya barabara lakini Hollywood ndio wanaishi kina Tom Cruise na Denzel Washington. Na US ni nchi ya dunia ya kwanza.
 
..Hold on!!

..kwa hiyo inawezekana kabisa serikali ya Magufuli wamewapa WB data za uongo zilizopelekea tukapandishwa daraja.

..kwa kweli sikuwahi kulifikiria suala hili ktk angle hiyo.

Mkuu unaongelea masuala makubwa kama vile unaongelea habari za kina Haji Manara na Antonio Nugaz.
 
Back
Top Bottom