Mkutano wa Berlin ulimpa Ujerumani koloni linaloitwa Deutsch-Ostafrika ambalo lilikuwa ni mchanganyiko wa Tanganyika na Rwanda-Urundi. Lakini baada ya Ujerumani kushindwa vita ya kwanza ya dunia Umoja wa mataifa wa wakati huo uitwao The League of Nations uliamua kuyagawa makoloni ya Ujerumani chini ya usimamizi (Mandate Territories) wa mataifa yaliyoshinda. Tanganyika alipewa Uingereza na Rwanda-Urundi akapewa Ubelgiji.
Baada ya vita ya pili ya dunia kuisha mwaka 1945 Umoja wa Matafia uliamua kuyaacha haya makoloni chini ya usimamizi ule ule wa Uingereza na Ubelgiji. Kipindi hichi yaliitwa Trusteeship Territories, lakini ukiangalia kiundani zaidi huu haukuwa usimamizi bali ni mfumo uliohalalisha ukoloni kwa kutumia sheria za kimataifa.
Ukisoma vizuri utakuja kukuta kwamba Mandate or Trusteeship Territories yalikuwa hayana utofauti wowote ule na makoloni mengine duniani. Jina na aina ya unyonyaji vilikuwa ndivyo tofauti, kwamba Ujerumani alitumia Direct Rule na Uingereza alitumia Indirect Rule lakini features of colonial states were very present.