Kwenye Sekta ya Afya Rais Dr. Hussein Mwinyi amefanya Mageuzi, tumpe maua yake

Kwenye Sekta ya Afya Rais Dr. Hussein Mwinyi amefanya Mageuzi, tumpe maua yake

Ndio ni mageuzi kwani hatua alizochukua hazikuwahi kufanyika hapo nyuma ama kama zilifanyika basi zilikiwa kwa kiwango kidogo.

Dr. Hussein Ali Mwinyi ni Daktari kitaaluma yaani Dakatari wa Binadamu.

Tangu ameingia Madarakani Zanzibar kama Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amefanya yafuatayo yanayogusa Mwananchi moja kwa moja kwenye Sekta Mahususi ya Afya.

1. Ameongeza ajira kwa wafanya kazi wa sekta ya afya kwenye kada za Udaktari, Utabibu, Wauguzi, Maabara na Mionzi.

2. Dr Hussein Mwinyi imemchukua kipindi cha Mwaka mmoja tu madarakani ameweza kuongeza mishahara kwa wafanya kazi sekta ya afya. Kwa sasa Madaktari na Wauguzi katika serikali ya Mapinduzi Zanzibar yaani ni Neema tupu.

3. Ameongeza ufanisi ktk usimamiaji wa kutoa huduma bora kwa Wananchi na kuachana na hulka ya bussness asual. Ameweza kutoa management tendership na kuongeza watu wenye uwezo kusimamia utumishi kwenye sekta ya afya ( hii ni mada ya siku nyingine).

4. Dr. Hussein Mwinyi chini ya uongozi wake ameweza kuongeza Vituo vipya vya kutolea huduma za afya na kuboresha vilivyopo.

Ameongeza Hospitalu za wilaya kila wilaya na Mkoa kila Mkoa. Haya ni mafanikio makubwa kuhakikisha Jamii ya Wazanzibar wenye idadi takribani Milioni Mbili wanapata huduma bora na ya kuaminika.

Lakini ktk yoote hayo Dr Hussein Mwinyi ameonesha nia na uongozi thabiti kwenye jambo hili na amehakikisha mipango inafanyika kama ilivyopangwa.

Tumpe maua yake aweze kufanya vizuri zaidi.

Nawatakia Sabato Njema.
Kumbuka huyo ni Rais Si waziri wa AFYA.

Ongea zaidi.
 
Nami nimpongeze Mhe. Mwinyi na team yake ya SUK. Ila naomba aboreshe usafi mitaani. Anaweza kupanga siku moja kwa wiki kwa ajili ya usafi maeneo yanayozunguka wananchi. Wananchi wafanye usafi wao. Hili lisishirikishe wadau, ili kuwaonyesha kuwa hata sisi tunaweza kufanya kazi zinazotuhusu. Pia tujiepushe na kuomba misaada kwa vitu tunavyoviweza kufanya hasa kwenye usafi.
Tukiwa wasafi tutaondoa magonjwa mengi na hospital hazitakuwa na umuhimu.
 
Back
Top Bottom