TheChoji
JF-Expert Member
- Apr 14, 2009
- 5,771
- 17,849
Hili li ugonjwa limekaa kipigaji pigaji sana. Mi sio mtaalam wa mambo haya, lakini sijui kwanini naona kabisa li korona kama ni li biashara fulani la kupigia hela. Kinachonifanya niwe na wasiwasi ni haya mambo yafuatayo:
1. Ndani ya miaka miwili, kuna zaidi ya variants 5 za korona! Halafu eti kila nchi ina aina yake ya korona. We ulisikia wapi? Yaani kirusi kila kikivuka mpaka wa nchi kinajibadilisha? Kuna variant ya China, India, South Afrika, UK, Brazil nk.. Mbona HIV tuko nayo tangu miaka ya 70 lakini mpaka leo kuna HIV 1 na HIV 2 tu? Influenza yenyewe tunayo tangu kuumbwa kwa Adam na Eva ila mpaka leo kuna A, B, C na D tu! Hizi variants za korona zinaonekana kama zilitengenezwa na kusambazwa kwenye nchi mbalimbali ili kuwavuruga madaktari, ili tupigwe!
2. Ndani ya miaka miwili tayari kuna aina zaidi ya 9 za chanjo za korona, na zingine zaidi ya 50 zipo kwenye clinical trials!! Wakati mwanzo tuliambiwa oooh kutengeneza chanjo itachukua miaka mingi sana.. oooh sijui nini.. kiko wapi? Jamani! HIV ina umri wa miaka 45 sasa na hakuna hata aina MOJA ya chanjo, Hii imekaaje? Mi naona tu kama tunapigwa wakuu..
3. Msisitizo na vitisho vikubwa vinavyoambatana na chanjo. Yaani hizi chanjo zimekua kama nini sijui. Mi naona ni kama tunasukumiziwa hayo machanjo yani lazma utumie hima hima!!! Wakati huo huo nchi kama UK ambayo mwanzo ilichanja karibu raia wake wote, jana wamerecord cases mpya 28,000 na zinazidi kuongezeka! Ukiuliza sasa haya machanjo yanasaidia nini, hupewi majibu ya kueleweka ni danadana tuu. Wajameni, hatupigwi kweli hapa..?
4. Kwanini chanjo na sio dawa? Tuachane na ule upuuzi wa kwamba virusi hua havina dawa, maana mwanzo tuliaminishwa pia virusi havina chanjo. Mi naona kama hawa jamaa wameona biashara ya dawa inachukua muda mrefu sana kurudisha faida (wamejifunza kutoka kwenye HIV), maana ni mpaka mtu augue ndio atafute dawa. Njia nzuri ya kurudisha hela mapema, ni kupitia kwenye chanjo ambapo unaweza kulazimisha watu wote bilioni 8 waliopo duniani kuchanjwa immediately (uwe unaumwa au huumwi) na ukarudisha pesa yako fasta! Na ili upige hela zaidi unasema dozi moja haitoshi lazima urudie rudie kila baada ya muda.
Mi kwakweli naona tu kama kuna ajenda kubwa sana ya siri kwenye hili gonjwa wakuu, labda wataalam mtanisahihisha