ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 25,030
- 61,298
Bado Neema na Baraka za Mungu zilizomo ndani ya nafsi ya kiongozi huyo, kinabaki kua kipimo muafaka sana cha uwezo na umahiri wa kiongozi husika.Katika zama hizi za AI kama OpenAI ChatGPT, nyie mnampimaje uwezo wa kiongozi wa chama tawala au upinzani? Maana leo hii wote wanaweza kutafuta hoja kali, hotuba nzuri na majibu ya kisomi kupitia AI wakaonekana wana akili sana mbele ya watu.
Zamani mtu alikuwa akitoa hotuba nzito watu wanaamini moja kwa moja kuwa ana uwezo mkubwa wa kufikiri, lakini sasa teknolojia imefanya hata mtu asiye na uwezo mkubwa wa uchambuzi aonekane ana upeo mkubwa kwa sababu tu amepewa hoja tayari na AI.
Kwa hiyo katika kipindi hiki, kipimo cha kiongozi kinabaki kuwa nini hasa? Je ni uwezo wa kuongea mbele ya kamera? Umaarufu mtandaoni? Au matokeo halisi aliyowahi kuyaonyesha kwenye nafasi alizopata?
Kwa sababu ukweli ni kwamba leo hii hata viongozi wanaopingana kisiasa wanaweza kutumia source hizohizo za AI kupata takwimu, hoja na majibu yanayofanana. Ndiyo maana imekuwa rahisi sana kwa jamii kushawishika na maneno makubwa kuliko ushahidi wa vitendo.
Mfano mtu anaweza kuambiwa fulani ni mchumi mkubwa sana au mwingine ni fisadi mwenye mabilioni, lakini ukiuliza ushahidi wa moja kwa moja mara nyingi hakuna zaidi ya simulizi za mtandaoni na propaganda za kisiasa. Sasa kwenye zama ambazo AI inaweza kutengeneza hoja nzuri kwa kila upande, wananchi wanapaswa kujifunza kupima viongozi kwa matokeo yao halisi badala ya uwezo wao wa kuongea tu.
Na hata hilo la kupima kwa “matokeo halisi” bado ni gumu, kwa sababu wananchi wengi hatujui uhalisia wa kinachoendelea ndani ya ofisi na mifumo ya serikali. Mara nyingi tunachokiona ni taarifa rasmi, interviews, propaganda za kisiasa au vipande vya video mtandaoni.
Hivyo kwenye zama za AI na media kali, imekuwa rahisi sana kujenga taswira ya mtu kuonekana shujaa, msomi au mchapa kazi hata kama wananchi hawaujui ukweli wote wa nyuma ya pazia. Ndiyo maana leo hii si rahisi tena kutofautisha kati ya uwezo wa kweli wa kiongozi na image inayojengwa kupitia teknolojia, media na ushawishi wa mtandaoni.
kwa ufupi mtu kama mwana Fa anapaswa awe hata rais wetu kwa sababu si hana kashfa yoyote...mwanafa vs lissu bora nani awe rais kwa haraka harakaUmeangalia upande mmoja wa hotuba tu, kitu ambacho si kweli, kuna vigezo vingi na kimojawapo ni rekodi ya huyo mwanasiasa, hapo AI haitokusaidia chochote..
MwanaFA hajawahi kushinda uchaguzi wowote, kuanzia ndani ya chama chake amekuwa akibebwa.kwa ufupi mtu kama mwana Fa anapaswa awe hata rais wetu kwa sababu si hana kashfa yoyote...mwanafa vs lissu bora nani awe rais kwa haraka haraka
sasa viongozi wenyewe tunawaona kwenye hotuba pekee utawaonea wapi kwengine kwa mfano mimi sijawahi kumuona heche wala lissu live zaidi ya kwenye cameraWewe ndio huwezi kutofautisha ubora wa viongozi kwa sababu unafikiri hotuba ndio kipimo cha uongozi
kama ishu ni matokeo kwanini sasa tu dealna sehemu ambazo hatuishi yaani nachomaanisha kwanini tusiachie wananchi wa kiteto wenyewe waamue sisi tudeal na tulipo labda ruangwaUbora wa uingozi unatokana na matokeo, sio hotuba wala hoja.
Hii ni sawa na wale wanaosema AI inatengeneza website/app ndani ya dakika tano, ni kweli inawezekana ila ukiwapatia hizo tools wanaweza maliza hata mwezi bila kuwa na matokeo ilihali AI iko na resource za kuwawezesha kweli kufanya hivyo so issue inabaki kwenye matokeo
Ukienda hospitali ya umma ukaambiwa dawa hakuna au kituo cha afya kina nesi mmoja, maabara mmoja na clinical officer mmoja hakuna daktari. Ujenzi wa Barabara km 80 wilayani kwenu umesimama kwa sababu mkandarasi hajalipwa madai yake, hakuna hela hazina. Hapo unahitaji AI kujua kua kiongozi aliyepo ni mbovu, hana uwezo? Wala kiongozi haitaji AI kumuambukiza hasira za kuwachukia na kuwashikisha adabu mafisadi wanaoiba hela ya serikali.Katika zama hizi za AI kama OpenAI ChatGPT, nyie mnampimaje uwezo wa kiongozi wa chama tawala au upinzani? Maana leo hii wote wanaweza kutafuta hoja kali, hotuba nzuri na majibu ya kisomi kupitia AI wakaonekana wana akili sana mbele ya watu.
Zamani mtu alikuwa akitoa hotuba nzito watu wanaamini moja kwa moja kuwa ana uwezo mkubwa wa kufikiri, lakini sasa teknolojia imefanya hata mtu asiye na uwezo mkubwa wa uchambuzi aonekane ana upeo mkubwa kwa sababu tu amepewa hoja tayari na AI.
Kwa hiyo katika kipindi hiki, kipimo cha kiongozi kinabaki kuwa nini hasa? Je ni uwezo wa kuongea mbele ya kamera? Umaarufu mtandaoni? Au matokeo halisi aliyowahi kuyaonyesha kwenye nafasi alizopata?
Kwa sababu ukweli ni kwamba leo hii hata viongozi wanaopingana kisiasa wanaweza kutumia source hizohizo za AI kupata takwimu, hoja na majibu yanayofanana. Ndiyo maana imekuwa rahisi sana kwa jamii kushawishika na maneno makubwa kuliko ushahidi wa vitendo.
Mfano mtu anaweza kuambiwa fulani ni mchumi mkubwa sana au mwingine ni fisadi mwenye mabilioni, lakini ukiuliza ushahidi wa moja kwa moja mara nyingi hakuna zaidi ya simulizi za mtandaoni na propaganda za kisiasa. Sasa kwenye zama ambazo AI inaweza kutengeneza hoja nzuri kwa kila upande, wananchi wanapaswa kujifunza kupima viongozi kwa matokeo yao halisi badala ya uwezo wao wa kuongea tu.
Na hata hilo la kupima kwa “matokeo halisi” bado ni gumu, kwa sababu wananchi wengi hatujui uhalisia wa kinachoendelea ndani ya ofisi na mifumo ya serikali. Mara nyingi tunachokiona ni taarifa rasmi, interviews, propaganda za kisiasa au vipande vya video mtandaoni.
Hivyo kwenye zama za AI na media kali, imekuwa rahisi sana kujenga taswira ya mtu kuonekana shujaa, msomi au mchapa kazi hata kama wananchi hawaujui ukweli wote wa nyuma ya pazia. Ndiyo maana leo hii si rahisi tena kutofautisha kati ya uwezo wa kweli wa kiongozi na image inayojengwa kupitia teknolojia, media na ushawishi wa mtandaoni.
Mchukue mwanaFA wako au Bashite wafanye interview ya nusu sasa tu na waandishi wa kama Odemba au Khalifa wa Chanzo uone walivyo weupe kichwani, Lissu anafanya interview BBC Hard Talk, CNN na Al Jazeera Head to Head na Mehdi Hasan bila shida yoyote.sasa viongozi wenyewe tunawaona kwenye hotuba pekee utawaonea wapi kwengine kwa mfano mimi sijawahi kumuona heche wala lissu live zaidi ya kwenye camera
Kama tatizo ni kutumuona Lissu live muulize mwanaCCM mwenzako Anna Makinda aliyekuwa anawaambia wabunge wenzake wa CCM wanyamaze wamsikilize Lissu akishusha nondo bungeni enzi hizo hakuna AI. Sasa hivi kuna AI na hakuna hata watu wanaofutalia au kujua nini kinaendelea huko bungeni.sasa viongozi wenyewe tunawaona kwenye hotuba pekee utawaonea wapi kwengine kwa mfano mimi sijawahi kumuona heche wala lissu live zaidi ya kwenye camera