Mara nyingi huwa najiuliza,
Inamsaidia nini yule mtu ambaye anafurahi kuona mwenzake akiporomoka???
Au inamsaidia nini yule mtu mwenye chuki na mtu asiyemjua???
Moja ya Jambo nililojifunza, watanzania hawapendi kuona maendeleo ya wenzao!
Utapanda bodaboda siku zote hata miaka 10 hakuna anayekuuliza au kukusalimia, lakini ukinunua hata Vitz wataanza kuweka vikao amepata wapi???
Ifike mahali watanzania tuwe na mioyo ya huruma, kuwa na moyo wa kuwatakia mema wengine nawe utafanikiwa!!!
Hii nyimbo ya kwetu ina ujumbe mzuri kwa watanzania, likewise Aje ina ujumbe mzuri kwa watanzania! kwa nini usijivunie kwamba Tanzania imepiga hatua ktk Mziki?? Huoni Nigeria ina wasanii wangapii???
For your information:
Mtu unayemchukia bila sababu au kutokana na juhudi zake za kazi, always anafanikiwa mpaka basi!
Ni Bora umpende adui yako! Maana hatari ni kwamba utakuja kumpenda siku usiyoijua!