Kwikwi (Hiccups): Chanzo na Tiba (matibabu) yake

Mpelekeni hospital haraka,anko wangu tulizembea kwikwi ikamuua..!!
 
Jaribu kumshtua, akishtuka basi ataacha. unaweza kumdanganya hata fulani (Mtu wa karibu yake sana) amefariki, jaribu hili zoezi akishndikana muone daktari mapema
 
MUNGU AMPONYE mimi si mtaalam jaribu kufuata hayo hapo juu au tungoje wataalam wengine watakusaidia ila hosp ni mahala pa kwanza pa kukimbilia
 
Habari jf doctor... Nina ndugu yangu kuanzia jana ana kwikwi inayomuumiza hadi kufua haitulii naomba msaada wa haraka atumie nini ili ipoe??
Eee kweli nimekumbuka dawa ingine, umgandishie uzi usoni !!
 
kwanza poleni! chukua asli mbichi vijiko viwili vya chakula na sukari vijiko vinne vya chai koroga ktk bilauri moja ya maji ya kunywa kunywa mfululizo hadi iishe utapata nafuu haraka endapo hali hii ikiendelea nijulishe tafadhali
 
Ni vizuri kwenda hospital kwani wakati mwingine kwikwi ni dalili ya serious illness kama vile uremic syndrome iliyotokana na tatizo la figo kwa muda mrefu.
 
kwanza poleni! chukua asli mbichi vijiko viwili vya chakula na sukari vijiko vinne vya chai koroga ktk bilauri moja ya maji ya kunywa kunywa mfululizo hadi iishe utapata nafuu haraka endapo hali hii ikiendelea nijulishe tafadhali

Ametumia lakini bado inaendelea.
 
Mimi nimekuwa napata tatizo hili kwa kujirudia rudia kwa, mara ya kwanza lilinisunbua kwa siku mbili, nilikunywa maji nadhani yanaweza fika ndoo mbili halikuisha, nikaenda hospitali...marie stopes wakanichoma sindano kwenye mshipa wa mkono ndio likaisha (hii sindano ilinilaza kama masaa saba hivi), baadae ilivyonitokea nikashauriwa kula ndizi mbivu (visukari) na ikakata, juzi kati limenitokea tena nikajaribu ndizi zikadunda, nikapitia humu jf kuna uzi mzizimkavu alishauri kutumia juisi ya muwa mweusi na asali, sikupata huo muwa mweusi ila nilipata juisi ya muwa nikatia asali kidogo nilivyokunywa kwikwi ikakata hadi leo, hebu jaribu hivyo ila mkuu ikishindikana hospitali ni muhimu zaidi, kwikwi inatesa mno ......
 

Asante kwa ushauri nitaitafuta.
 
mfululizo nilimaanisha anywe pasina kupumua hadi amalize bilauri km ndivyo alivyofanya basi yawezekana ni syndrome ya tatizo lingine mwilini
 
Tafadhar naomba kujua dawa ya ugonjwa wa kwikwi kwan inanisumbua sana, Umri wangu 25 miaka pia ningeomba kujua visababishi
 
Kunywa maji ya kutosha kila siku mpaka lita 3.5 katika masaa 24

Pia kila nusu saa kabla ya kula, kunywa maji, ukisikia kwikwi kunywa maji.


Nitajie uzito na urefu wako kwa msaada zaidi
 
Tafadhar naomba kujua dawa ya ugonjwa wa kwikwi kwan inanisumbua sana, Umri wangu 25 miaka pia ningeomba kujua visababishi
TIBA MBADALA YA MARADHI YA KWIKWI HICCUPS TREATMENT



MARADHI YA KWIKWI (Hiccups)


Kwikwi hutokana na kushtuka na kusinyaa kwa ghafla kwa misuli mikuu ya upumuaji (diaphragm) ambako hujirudia rudia na kusababisha hewa kuingia kwa kasi kwenye mapafu.
Hii husababisha milango ya sauti katika koo (vocal cords or voice making cords) kufunga ghafla na kutoa sauti inayosikika wakati wa kwikwi.


Kwikwi sio ugonjwa; kwikwi ya muda mfupi ni kero ndogo tu ambayo inapita, lakini kwikwi isiyokatika inaweza kuwa dalili ya tatizo lingine ambalo huenda likahitaji uchunguzi wa kitaalamu.
Sababu zinazopelekea kupata kwikwi;

Kula haraka haraka au kula sana (kuvimbiwa)

Kula vyakula vyenye viungo sana (very spicy foods)

Kunywa vinywaji vyenye gesi(carbonated beverages) au vya baridi sana

Ulevi au kunywa pombe nyingi kwa mpigo

Upungufu wa maji na madini mwilini (dehydration)

Tumbo kujaa gesi, asidi (hyperacidity) au vidonda vya tumbo

Sababu hizi mara nyingi husababisha kwikwi ya muda mfupi ambayo huisha bila kuhitaji matibabu wala uchunguzi wa kitaalamu.

Sababu nyingine (Rare but serious) ni pamoja na;

Upungufu au kuvurigikwa kwa kiasi cha madini mwilini(electrolyte imbalances)

Kukusanyika kwa sumu mwilini kama vile sumu ya figo (Uremia)

Magonjwa ya mapafu kama vile vichomi(pneumonia), pumu(asthma), TB au maji kukusanyika nje ya mapafu(pleural effusion),

Saratani au uvimbe kwenye mapafu, ubongo, uti wa mgongo au tumboni.

Magonjwa ya moyo (heart attack, arrhythmias, infections to the heart)

Kidole tumbo(Apendix illness) na magonjwa ya kufanania nayo

Magonjwa ya Ini, kongosho au mfuko wa nyongo

Madawa au kunywa sumu aina fulani

Kuumia katika eneo la misuli ya upumuaji (diaphragm injuries).

Kwikwi itokanayo na matatizo haya huwa ya muda mrefu au inayojirudia rudia sana, na huisha tu kama tatizo lililosababisha

likigundulika na kutibiwa. Ukiona dalili ya kwikwi isiyoisha tafadhali muone daktari.

Sababu ya kisaikologia (psychological reason) Hii huwapata watu wachache. Watu hawa hujidhania kuwa wana kwikwi isiyokatika,

hivyo huendelea kutoa sauti kama mtu mwenye kwikwi. Kwikwi ya aina hii haina mfumo maalum, na haitokani na kusinyaa kwa misuli

ya upumuaji; kwa mtu mwenye tatizo hili ni muhimu kutafuta tatizo alilo nalo kisaikologia na kulitatua.

Namna ya Kuzuia Kwikwi

Kula taratibu haraka haraka hujaza gesi tumboni na kusababisha kuvimbiwa

Kula kiasi kidogo kwa wakati ; Inashauriwa kuongeza idadi ya milo kwa siku badala ya kiasi; milo mitano midogo midogo badala ya mitatu mikubwa kwa siku.

Punguza au ondoa kabisa vyakula vyenye viungo vingi/vikali.

Kunywa maji Unywaji mzuri wa maji huzuia na kutibu kwikwi, pia hulinda mwili na maradhi kama vile upungufu wa maji na madini(dehydration) na figo kutofanya kazi vizuri.

Fanya mazoezi - huboresha ufanyaji kazi wa mapafu na misuli ya upumuaji, pia husaidia kuongeza kinga mwilini na kuimarisha ufahamu (mind state)

Kuzuia kwikwi ni muhimu tu kwa wale wanaopata mara kwa mara.Matibabu ya kienyeji: (Usifanye kwa mtoto)

Kumshitua mhusika, au kumzubaisha ili kuondoa mawazo yake kwenye kwikwi

Kunywa glasi ya maji iliyojaa bila kukata pumzi

Kubana pumzi na kuhesabu mpaka kumi


Kuweka sukari chini ya ulimi

Kulala. Usingizi ni dawa moja nzuri sana ya kwikwi

Kwa mtoto anayenyonya waweza kumnyonyesha, au kumuweka begani acheue.

.KWIKWI-twanga hiliki changanya na maziwa kisha kunywa glasi moja.


Matibabu ya kitaalam
Muone daktari kwa matibabu kama

Kwikwi haikatiki kwa muda mrefu (siku au zaidi),

Kwikwi inakusababisha kuchoka sana,

Kama mapigo ya moyo yanabadilika,

Kama unashindwa kulala kutokana na kwikwi

Kama inasababisha msongo mawazo kutokana na kujirudia mara kwa mara.

Kabla ya kuanzisha dawa ni muhimu kufanya vipimo ili kuhakikisha magonjwa yanayoweza kusababisha kwikwi yanapatiwa matibabu kama yapo.

Kama chanzo cha kwikwi kimefahamika katika uchunguzi, tibu chanzo na kwikwi itaisha.

Ikiwa Umetumia karibu njia zote bado hujapona nione kwa wakati wako Dawa ya kukutibu Kwikwi ninayo ukihitaji dawa bonyeza hapa.Mawasiliano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…