Kwisha! Yanga yatolewa CAF

Kwisha! Yanga yatolewa CAF

Grader

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2009
Posts
445
Reaction score
64
Ilikuwa mechi ngumu sana iliyojaa ufundi na kukamiana na mwishowe ESS ikafanikiwa kushinda kwa uzembe wa mabeki. Timu za ukanda cecafa zinajifunza nini?
 
Kushnei kabisa sasa kelele zitapungua jijini, ila wamecheza vizuri kweli kweli tatizo umaliziaji tu
 
Wanasimba tuliwataka washinde lakini nadhani viwango vyao bado sana!
Pole yao.... wajifariji na hili "kufunga wametufunga lakini chenga twawala"
 
Bye bye,young africans,nitapumua mtaani ukweli utabaki simba ni timu pekee iliyowatoa waarabu mtake msitake na naomba mwakan ktk round ya kwanza mkutane na enyimba,au waarabu wa misri tena ili mtoke mapema
 
Mmebaki kung'ang'ana na historia tu wengine tulikuwa hatujazaliwa
Toka nianze kuwa mshabiki sijaiona simba ikipanda ndege ni boti na
magari tu.
 
Afadhali walivyofungwa!nchi ipoe kwanza tuwaze mambo ya sarafu yetu.
 
Mmebaki kung'ang'ana na historia tu wengine tulikuwa hatujazaliwa
Toka nianze kuwa mshabiki sijaiona simba ikipanda ndege ni boti na
magari tu.

Kesho nenda sunday school, mpira umeanza shabikia lini kama kumbukumbu zako fupi hivyo ka piriton????
 
Kwani kuna aliyetegemea matokeo tofauti na hayo?jamaani hii ni sawa sawa na bunge lijalo theluthi tatu kutangazwa kuwa ni ukawa na hivyo kupata waziri mkuu kutoka ukawa au rais wa zanzibar kuwa maalim hizo sio news ni mambo yaliyowazi kuwa lazima yatokee...Nyie hamkuona wanasherekea ubingwa kabla ya kwenda tunisia kusudi wakitoka huko kila mtu zake..
 
Tunaomba kwenye sherehe za kitaifa kuwepo na mashindano sababu sisi ni wa hapa hapa, si mnaona tunavyofanya vizuri kwenye mabonanza! Michezo ya kimataifa tuwaachie hakina Azam na Yanga.
 
Tunaomba kwenye sherehe za kitaifa kuwepo na mashindano sababu sisi ni wa hapa hapa, si mnaona tunavyofanya vizuri kwenye mabonanza! Michezo ya kimataifa tuwaachie hakina Azam na Yanga.

Hahahaaa, sisi wenzetu kina Jang'ombe kwenye kombe la Mapinduzi teh teh teh
 
Back
Top Bottom