Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM

Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM

Sio kyela tu bali taifa zima bado linahitaji mchango wa Mwakyembe
 
safi sana kabla hajawa mbunge tayari ametoa ajira kubwa jimboni.sasa DR.wa sheria ya Katiba kafanya nini zaidi kwa wanaKyela?kwanini asijikite kwenye Corporate Law?

Hujui alichofanya Dr. mpaka mawe yanaongea!! nchi inatikisika!! hujui tuuu!!
 
- Jamii Forum, kutoka Jambo Forum baada ya TEF, kabla ya BCS. JF yaani Taasisi ya Great Thinkers, finally ime-produce vijana watatu watakaojitosa kwenye kinyanga'nyiro cha ubunge wa Tanzania katika majimbo matatu ya taifa,

- Kwanza tuliitwa wajinga, baadaye tukaitwa magaidi, kabla hatujawa wahuni and now tutapigana vikumbo nao kwenye uongozi wa taifa, may God bless JF katika msafara wa mamba makenge huwa hawakosi, badala ya kujadili hoja za George na DK, wamelilia kujadili laptop, halafu tunashangaa kwamba kwa nini viongozi wetu wanakuwa na mawazo kama yetu wananchi wa aina hii.

Kwa wana-JF wote mtakaochukua fomu, Mungu wa mbinguni awabarikie, maana mnatusafisha wote hapa kwamba we know what we are talking about, tunapoongelea uozo wa viongozi, tumewapa darasa sasa mtuwakilishe JF Kumkoma Nyani!

- Vijana msitishike na kelele za kina Clinton against Obama, yaani kelele za mlango, wakilisheni JF alitutisha Lowassa na Manumba lakini JF ipo na sasa tunatoa wabunge watarajiwa, what a turn arround of events! Sasa tutatembea vifua mbele sana as JF members!

Mungu aibarikie JF!

FMEs!
 
Nikweli George anagombea Kyela kwa kupitia CCM, na nime confirm hilo kutokana na mmoja wa washauri wake ambaye anaishi hapa USA na amekwenda Tanzania kuungana na yeye.
Financial crisis ni sooo.....lazima wafulie....unajua mie hii kitu inanikera sana....ati ku;eta mabadiliko lazima uwe mbunge? nakereka sana mwangalieni kijana kama mwakaL atakavyofulia.....
mie nilifikiri labda angewasaidia wana kyela hata akiwa nje ya bunge......labda credit crunch imemsukuma zaidi apate wazo la kuingi mjengoni....

- Jamii Forum, kutoka Jambo Forum baada ya TEF, kabla ya BCS. JF yaani Taasisi ya Great Thinkers, finally ime-produce vijana watatu watakaojitosa kwenye kinyanga'nyiro cha ubunge wa Tanzania katika majimbo matatu ya taifa,
1.joji 2.wiliamu 3.? labda nyani ngabu,masanilo au fidel80......

pamoja na yoote uliosema kuhusu JF bado tupo pale pale.....hawa wana JF wana jipya gani?
 
Last edited:
Endapo Mwakyembe atashindwa Ubunge itakuwa ni simanzi kubwa katk nchi nzima na nafurahi kwa sababu sioni uwezekano wa hilo kutokea Kyela 2010. Ata Mwang'onda alileta upinzani kwa Mwandosya kwenye UNEC mkoa na kwa mishemishe nyingi kama alizoanza nazo Mwakalinga lakini mwisho wa siku wote tunajua matokeo yalikuwaje,na hilo ndilo litakalotokea Kyela 2010.
 
Nakumbuka wakati naongea na Mwakalinga alisema haya:

  1. Si kweli kuwa nimekuja Tanzania rasmi kugombea Ubunge, ikiwa hivyo nitawafahamisha watu wazi bila kificho.
  2. Mwakyembe anajaribu kunimaliza hata kabla sijafikiria kupambana naye kwa kutumia gazeti la Majira. {Mwezi Machi aliwahi kunipigia simu akinieleza kuwa Mwakyembe (ambaye pia ni member wa JF) alikuwa akimsumbua sana kwenye PM na alidai kuwa anatumia gazeti la Majira kuendeleza propaganda dhidi yake.}
  3. Hata kama nikigombea Kyela kwani jimbo hilo Mwakyembe ana hati miliki nalo?
Sasa sitashangaa kama kaamua kugombea rasmi, yaelekea ndo maana hata SteveD hajatia neno katika topic hii, atakuwa alipata kanusho toka kwa Mwakalinga na anashtushwa na habari hizi!
 
Ili kuleta ushindani wa kweli kwenye chaguzi majimboni ni vizuri sana kupambanisha vichwa kwa vichwa, hii inasaidia sana wagombea kuwa makini katika kumwaga sera zao na kuhakikisha zinatekelezwa ipasavyo.

Hata na hivyo si vuzuri sana kuingia kny siasa kwa njia za kuchafuana hasa kuchafua wale viongozi waliokutangulia tena ambao watanzania wameshawakubali kwa michango yao kwa Taifa kwa ujumla. Ni vizuri sana Mwakalinga akaingia kwa sera atakazo wauzia wana Kyela na pindi akishinda atazisimamia na kuzitekeleza kwa manufaa ya Kyela na Taifa kwa ujumla sio tu kundia wale walio mtangulia bila kusema yeye atafanya nini tofauti na akifanyacho aliyopo sasa!

Pia tunapowaassess hawa waheshimiwa tusiangalie tu michango yao kny majimbo yao tu....no tuwaangalie katika global picture......ya kitaifa. Je, wanauwezo sawa wakusimamia maslahi ya Taifa? au wanauwezo wakusimamia na kutetea maslahi ya majimbo yao tu? kwa mfano Mwakalinga akija kushinda ubunge, akateuliwa kuwa Waziri fulani, au kule mjengo akijabahatika kuwa kwenye kamati fulani ya bunge, je,anauwezo wakutetea maslahi ya Taifa kama tulivyoona Mwakyembe akilitetea taifa hili na hata kujiongezea maadui wengi wa kisiasa na kijamii?

Masuala ya Laptop sijui utalaam wa mambo ya IT sijui kubobea kny sheria, sijui kuwa na supermarket+ Hotel.....to me ni mambo mema but not very much relevant kumjudge mtu kama anafaa kuwa mbunge au laa. Wangapi wanamiradi mikubwa, wanaelimu za kutisha, watalaam wa hali juu hapa nchini wameweza kuconvert hivyo vipawa au mali walizonazo kny uongozi mzuri uliotukuka wa nchi hii na kuwakwamua wa Tanzania?

Kwangu mimi ni rahisi sana kumjudge Dr. kwa sababu tumeshamuona UWANJANI akicheza mpira...hivyo ni rahisi kumkosoa au kumkubali kwa yale aliyofanya au anayofanya coz we see him dancing! Kwa bwana Mwakalinga, ni vigumu sana kumjudge kwa sasa based on what we think he is good at....waswahili husema umdhaniaye ndiye kumbe siye! Wadau....ni mara ngapi tumeona watu wakiwa nje ya pitch wanachonga sana na kuwa laumu wanaocheza ndani kwa kuona na kukosoa kirahisi sana makosa yao....but pindi wakikabidhiwa njumu na jezi....huishia kuonekana vituko kwa kuwa watalii uwanjani!

So to me though naona changamoto na upinzani kama huu ni bomba sana kwa maendeleo ya jimbo na Taifa but tuwatendee haki viongozi walipo au waliotutangulia kuwa madarakani!
 
Du mjadala mtamu sana, wengine tunangoja muda mwafaka risasi zenyewe chache kwa hiyo inabidi kuzitumia kwa uangalifu sana.

Poti
unasema unangoja muda?Si umeona mambo magumu kwenye timu yenu ndo maana umenyamaza.
Umeme wa upepo umefikia wapi?Rudi mtumbwi unazama uku,msomi sana na mheshimiwa mkubwa kabisa kabanwa,Kifukwe anaangaika lakini Kyela sio YANGA.
 
Mnaelewa siasa za Kyela na Mbeya kwa ujumla ni ngumu sana kuliko sehemu yoyote Tanzania. Mtasikia na kwa Prof. Mwandosya nako muda si mrefu
 
Acheni watu wapya wajitokeze ili tulibadili BUNGE letu ambalo sasa limejikita kwenye VISASI na kuviziana. Hakuna namna ya kuibadili SERIKALI iliyoko madarakani kama Wabunge watabaki hawahawa na nyimbo zao za RICHMOND, KIWIRA,....
 
Mnaelewa siasa za Kyela na Mbeya kwa ujumla ni ngumu sana kuliko sehemu yoyote Tanzania. Mtasikia na kwa Prof. Mwandosya nako muda si mrefu
Kifupi nilienda Mbeya na kuzunguka kwenye majimbo ya Kina Mwakyembe, Mwakyusa na Mwandosya nikagundua mambo mengi ya kuchekesha na kuhuzunisha sana.

Kuna picha nilipiga za hali ya mambo huko nitaziweka hapa soon.

Barabara zinasikitisha, yani heri ziitwe barabara za vumbi basi, ni makorongo tu. Usafiri toka Mbeya mjini kwenda majimboni mgumu sana.

Umeme wengine wamevuta kwa kupitisha maeneo ambapo hawataki kushirikiana na majimbo ya wenzao ambao wapo majimbo jirani hivyo umeme unaenda kwenye jimbo la mmoja na hataki wenzake waunganishe kwenye line ileile. Nadhani hili ndo linapelekea barabara nyingi kutotengenezwa ili majimbo ya majirani yasifaidi!

Raia wana imani na wabunge wao, wengine wamemchoka Mwakyembe, wengine wanasema kwao Mwakyembe ni sawa na mfalme. Ni kweli huwezi kupendwa na watu wote...

Kifupi maisha ya watanzania mikoani ni magumu, mkuu Omutwale anaweza kuwapa reality ya hali ya sasa maana tulikuwa tukizunguka pamoja yeye akiwa Singida, Kigoma na Tabora. Jimbo la Rostam ni kuzuri kuliko majimbo kadhaa ya Dar!

Mwakalinga ndiye mmiliki wa KBC Hotel? Hilo nilisahau kuuliza lakini issue ya yeye kuwa na vitega uchumi kadhaa pamoja na kuanzisha FM Radio Station pale Kyela niliambiwa.
 
Ili kuleta ushindani wa kweli kwenye chaguzi majimboni ni vizuri sana kupambanisha vichwa kwa vichwa, hii inasaidia sana wagombea kuwa makini katika kumwaga sera zao na kuhakikisha zinatekelezwa ipasavyo.
Wakati mwingine hata ukipata vichwa, tatizo linakuwa ni sera za vyama kwa maana inafika wakati wanalazimika kuhubiri sera za chama na si yale wanayoyaamini wao wenyewe. Kama kungekuwa na utaratibu wa wagombea binafsi, hapo ndipo tungeshuhudia vichwa vikishindana kikwelikweli
 
Umeme wengine wamevuta kwa kupitisha maeneo ambapo hawataki kushirikiana na majimbo ya wenzao ambao wapo majimbo jirani hivyo umeme unaenda kwenye jimbo la mmoja na hataki wenzake waunganishe kwenye line ileile.

Hahahaha hii ndio ipo kwenye jimbo la Prof. Mwandosya kwake umeme mpaka kijijini kwake kwa wenzie NO kisha barabara hivyo hivyo ya jimbo flani wametengeneza safi kwa changarawe ukiendelea na safari kwenye jimbo jingine unakutana na mashimo ya ajabu ndo Siasa za Mbeya yaani ngumu sana kuzielezea lakini ukifika kule ndo utajua.
Kikubwa unajua wananchi wa Kyela na wa Tukuyu hawaivi kabisa.
Kanda2 tunaomba ufafanuzi kwa nini hamuivi?
 
Endapo Mwakyembe atashindwa Ubunge itakuwa ni simanzi kubwa katk nchi nzima na nafurahi kwa sababu sioni uwezekano wa hilo kutokea Kyela 2010. Ata Mwang'onda alileta upinzani kwa Mwandosya kwenye UNEC mkoa na kwa mishemishe nyingi kama alizoanza nazo Mwakalinga lakini mwisho wa siku wote tunajua matokeo yalikuwaje,na hilo ndilo litakalotokea Kyela 2010.

Na Mwakyembe akishinda itakuwa simanzi kubwa kwa Kyelans maana alichofanya kyela Kikubwa ni kumwondoa Mwakipesile TU..Baada ya hapo ata ofisi ya mbunge wa Kyela ikaamia TEGETA
 
Hujui alichofanya Dr. mpaka mawe yanaongea!! nchi inatikisika!! hujui tuuu!!
Mimi wote Mwakyembe na Mwakalinga najua ni JF members ambao wanatumia Pen names, lakini kwa aliyeenda Kyela na kujionea hali halisi hawezi kusema Mwakyembe kafanya kitu cha ajabu kwa wana Kyela mpaka mawe yaongee.

Juu ya Richmond: Hivi Mwakyembe ndiye aliifumua Richmond? Nadhani nimepoteza memories.

The bottom line ninadhani wale wanaosema mtu kugombea ubunge ni kuwa umefulia na unafukuzia 12m ni kutaka kuwakatisha watanzania wenzetu ambao wanaamua kuchukua hatua za kuona namna ya kulinusuru bunge letu ambalo tumekuwa tukilipigia kelele kuwa limekaa kisanii sana. Heri ziingie sura mpya tuone kama kutakuwa na mabadiliko ya kuleta tija.

Hii tabia ya kukatishana tamaa ndo inasababisha tuendelee kulalamika ati wazee hawaachii ngazi ilhali sisi wenyewe tunakatishana tamaa kwa madai ati tunaweza kubadili system tukiwa nje ya system yenyewe.

Wakuu Next Level, Kinyamana etc, ingieni kilingeni, tutawaunga mkono na mkienda kombo huko bungeni hatutasita kuwakosoa.

Au kutoa upinzani kwa Mwakyembe ndio dhambi? Bahati mbaya/nzuri Mwakalinga anapinga kwa nguvu zake zote kuwa hana mpango na kugombea Kyela na hizi zote ni propaganda za watu, anasema akimaliza vacation yake anarudi UK na family yake na mtamwona JF soon.
 
Nakumbuka wakati naongea na Mwakalinga alisema haya:

  1. Si kweli kuwa nimekuja Tanzania rasmi kugombea Ubunge, ikiwa hivyo nitawafahamisha watu wazi bila kificho.
  2. Mwakyembe anajaribu kunimaliza hata kabla sijafikiria kupambana naye kwa kutumia gazeti la Majira. {Mwezi Machi aliwahi kunipigia simu akinieleza kuwa Mwakyembe (ambaye pia ni member wa JF) alikuwa akimsumbua sana kwenye PM na alidai kuwa anatumia gazeti la Majira kuendeleza propaganda dhidi yake.}
  3. Hata kama nikigombea Kyela kwani jimbo hilo Mwakyembe ana hati miliki nalo?
Sasa sitashangaa kama kaamua kugombea rasmi, yaelekea ndo maana hata SteveD hajatia neno katika topic hii, atakuwa alipata kanusho toka kwa Mwakalinga na anashtushwa na habari hizi!

Steve D na Field Marshal,kunisakama sana kwa habari yangu iliyofanyiwa uhakiki sana wilayani Kyela ya kugombea Mwakalinga sasa tunawaomba toeni tamko maana mlituhakikishia kabisa kuwa Mwakalinga HANA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE KYELA 2010!

Mwakalinga George nahisi sisi wana Kyela tunamfahamu zaidi kuliko hawa akina SteveD na Field Marshal ambao najua wanamjua kwa sababu tu ya kukutana kwao makazini au kwenye mahusiano ya mitandao kama vile hapa JF na kwingineko!

Kwa taarifa zaidi Mwakalinga sasa wanashirikiana na mkuu wa Mkoa wa Mbeya mzee Mwakipesile kufanya kampeni kumuangusha Mwakyembe;na habari zaidi mwenyekiti wa Mwakalinga wa kampeni kijana mnyakyusa mzaliwa wa Kyela , profesa,msomi wa elimu-mafuta anayefanya kazi zake nchini USA jinbo la California kawasili Dar jana na leo anaelekea Kyela tayari kabisa kufungua rasmi kampeni za chinichini za Mwakalinga!

Yatakayojiri zaidi tutawaeleza na plz Steve D na Field Marshala tupeni tamko la Mwakalinga maana nyie ni kama vile mlitaka tuamini kama vile ndiye wasemaji wake na wala si huyu Profesa anayeingia leo hapa Kyela!
 
Kikubwa unajua wananchi wa Kyela na wa Tukuyu hawaivi kabisa.
Sasa hizi siasa za chuki ndo zinaiua Mbeya kwa ujumla!

Steve D na Field Marshal,kunisakama sana kwa habari yangu iliyofanyiwa uhakiki sana wilayani Kyela ya kugombea Mwakalinga sasa tunawaomba toeni tamko maana mlituhakikishia kabisa kuwa Mwakalinga HANA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE KYELA 2010!

Mwakalinga George nahisi sisi wana Kyela tunamfahamu zaidi kuliko hawa akina SteveD na Field Marshal ambao najua wanamjua kwa sababu tu ya kukutana kwao makazini au kwenye mahusiano ya mitandao kama vile hapa JF na kwingineko!

Kwa taarifa zaidi Mwakalinga sasa wanashirikiana na mkuu wa Mkoa wa Mbeya mzee Mwakipesile kufanya kampeni kumuangusha Mwakyembe;na habari zaidi mwenyekiti wa Mwakalinga wa kampeni kijana mnyakyusa mzaliwa wa Kyela , profesa,msomi wa elimu-mafuta anayefanya kazi zake nchini USA jinbo la California kawasili Dar jana na leo anaelekea Kyela tayari kabisa kufungua rasmi kampeni za chinichini za Mwakalinga!

Yatakayojiri zaidi tutawaeleza na plz Steve D na Field Marshala tupeni tamko la Mwakalinga maana nyie ni kama vile mlitaka tuamini kama vile ndiye wasemaji wake na wala si huyu Profesa anayeingia leo hapa Kyela!
Malafyale,

Mkuu ni hivi, ukiongea na Mwakalinga anakataa katakata kuwa ana dhamira ya kugombea ubunge na anasema ni kwakuwa ana urafiki na Mwakipesile basi Mwakyembe anakuwa na wasiwasi hivyo kuanza kutafuta kila namna ya kummaliza hata kabla hajatangaza azma yake (kama ipo).

Mkuu, siasa za Mbeya zinafurahisha sana! Hivi wewe hurudi kujipima na wakuu hawa?
 
Kwa taarifa zaidi Mwakalinga sasa wanashirikiana na mkuu wa Mkoa wa Mbeya mzee Mwakipesile kufanya kampeni kumuangusha Mwakyembe;na habari zaidi mwenyekiti wa Mwakalinga wa kampeni kijana mnyakyusa mzaliwa wa Kyela , profesa,msomi wa elimu-mafuta anayefanya kazi zake nchini USA jinbo la California kawasili Dar jana na leo anaelekea Kyela tayari kabisa kufungua rasmi kampeni za chinichini za Mwakalinga!

Hapa Mwakalinga ndipo anapokosea du siasa za Mbeya ni visasi kwa kwenda mbele.
 
Back
Top Bottom