Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM

Haya kaka naona laptops zimekuchanganya....mweka hazina wa Tanzanet kumwangusha Dr Mwakyembe.....hii itakuwa sawa na Osama Bin Laden kuwa Papa wa Roman Catholic, tunasubiria hiyo 2010 tuombe uzima Gwamaka K

Masa,

Hapo nilipo highlight umeniacha mbavu zangu zimevunjika.....huu ulinganisho never imagined! OBL to be RC Pope?....!
 
Masa,

Hapo nilipo highlight umeniacha mbavu zangu zimevunjika.....huu ulinganisho never imagined! OBL to be RC Pope?....!

CCM hawezi kukubali kupoteza jimbo ndugu yangu, wanaakili sana wale....si ndo hao hao walimrushia mh mawe? watu wa Mbeya nawaheshimu sana wanajua haki zao ......hawana tofauti na wale wa Tarime!
 
Mwakalinga asome kwanza ramani. comments zake kwamba atatumia uzoefu wa kufanya kazi ulaya na pia ameacha kazi nzuri ulaya kuja kuwasaidia wana Kyela tayari zinaonyesha ubabaishaji wa hali ya juu. Hizi nazifananisha na propaganda za siasa za akina Osca Kambona na Abrahamani Babu walipokuwa ukimbizni huko ughaibuni.
Wao walikuwa wanaiona vema Tanzania na kuelewa zaidi jinsi ya kutatua matatizo ya Tanzania kwa kupitia mirror kuliko mtanzania anayeishi hapa Tanzania. Watu wa Kyela kama ni walevi chakari watampa Mwakalinga kura kwani huwezi kuchukua solutions za Ulaya uka zi impose Kyela zikafanya kazi. Kama nabisha muulize Nyerere aliyehamisha zana ya Ujamaa kutoka Israel akaiweka Tanzania bila kupima, ujamaa uko wapi?.

Ushauri wangu ni kwamba Mwakalinga hakuja na gunia la fedha za kugawa wala hana mpango wa kuwagawia wana Kyela vitega uchumi vyake bali amekuja na mdomo wa kuongea kama wanasiasa wengine. Mbaya zaidi kwa habari za kujua wanachohitaji wana kyela ni kama njozi kwake, yaani udhanifu zaidi kuliko uhalisia.

Plse amwache Dr. Mwakembe amalizie kazi ya kuwatoa mochwari mafisadi awazike then baada ya hapo aendelezee hapo la sivyo kikombe cha Mwakembe kikiachwa hakijaisha shubiri ya mafisadi kinaweza kuwa cha moto kwake akakitema.

Kuhusu Mwakembe kushindwa issue moja hiyo isiwe sababu ya kumhukumu plse tuangalie na mazuri aliyofanya kama ni machache kuliko hayo. Watu muelewe kuwapa watu ajira si jambo rahisi haswa katika ulimwengu tunaoishi kipindi hiki Mwakalinga mwenyewe pia hataweza labda awafukuze wafanyakazi kwenye projects zake awalete waliofukuzwa migodini.

Namshauri Mwakalinga atulize boli kwanza tumewaona wengi waliokuja kwa pupa za Ulaya na hatukuona difference. Fedha za maendeleo hutolewa na serikali na kama hawajatoa au wamepunguza utafanya nini kama si kubaki ukilaumiwa na wananchi kama mbunge yeyote ambaye hata hajafika Ulaya.


Please kubali ushauri wangu usidhalilike

Mtaalamu wa Rural Changes & social research
Gerad

Arusha
 

Mkuu Nsesi,

Heshima mbele! Nimependa sana uchambuzi wako you seem to know quite well these two persons and know quite well the Kyela politics...kula 5!

Vipi aren't you planning to join the battle huko Kyela 2010? Kama hujapanga, nakushauri tangaza kuingia huko uongeze ushindani ili tupate washindani wazuri kama Mchele wa Kyela!
 

NSESI,
Kama amevaa joho la Kikwete basi ajitangaze kuwa yeye ni Rais wa Tanzania. Naona umekiri kuwa kwao kakimbia na kuvamia kwenye kaya za wenzake.
Mkataa kwao ni mtumwa na zama hizi hatumtaki mtu kama huyo. Huwezi kukimbilia juu ya mti bila kupanda kwa kuanzia chini. Kachaguliwa na wana Kyela, na alitakiwa aanzie pale ndipo aende huku juu, au kama ataweza ayafanye yote kwa wakati moja.
Kama ni kitaifa basi subiri wamchague kitaifa, lakini Kyela mwakani tutamhukumu kwa kutudanganya kwa ahadi kibao ambazo ameshindwa hata kitu kimoja kutekeleza.
Kama na wewe unataka kuja njo tutakupima kwa uwezo wako, vinginevyo hatutaki waimbaji ambao nyimbo zinaishia ukumbini au majukwani, tunataka wanamaendeleo.
Kwa nini majimbo mengine yanapiga hatua na Kyela inabakia gizani? Kwani wale ni malaika? Baado kitambo kidogo, hukumu hiyo.
Kgwamaka
 

Sasa kama mlikuwa mkishirikiana na Mwakipesile alipokuwa Mbunge mbona hizo ajira hatukuziona?au mmefunuliwa upya safari hii, teh teh teh!!! na NI KWELI MWAKYEMBE SIO MWENZENU,KWANI YEYE NI MPIGANAJI ANAYEPAMBANA NA MAFISADI WAKATI NYIE MNAJINYENYEKEZA KWA MAFISADI KWA KUTAFUTA MANUFAA YENU BINAFSI NA SIO YA WANA KYELA WALA WATANZANIA,hamuwezi kuwa timu moja.
 
Nadhani fisadi ni neno pana na labda linakushinda kulifafanua.
Hata yeye ni fisadi, ziko wapi pesa za KDF? ana mengi ya kuja kutueleza mwakani, tunavuta pumzi
 
Haya kaka naona laptops zimekuchanganya....mweka hazina wa Tanzanet kumwangusha Dr Mwakyembe.....hii itakuwa sawa na Osama Bin Laden kuwa Papa wa Roman Catholic, tunasubiria hiyo 2010 tuombe uzima Gwamaka K

Hivi MTUME PAULO kabla hajawa Paulo alikuwa nani vile? Yohana Mbatizaji?
 
Mh Spika naomba mwogozo hili swali halieleweki.....!

Ha ahahaa, Masa.

Omba Biblia na siyo Mwongozo. Mwenyewe umeandika PAPA, sasa ukiambiwa Papa namba 1, unaomba mwongozo...... Ngoja tusubiri kaka 6 aje alete Mwongozo.
 
Nadhani fisadi ni neno pana na labda linakushinda kulifafanua.
Hata yeye ni fisadi, ziko wapi pesa za KDF? ana mengi ya kuja kutueleza mwakani, tunavuta pumzi

Nashukuru kwa atleast kukiri kuwa upo timu moja na mafisadi,kwa sasa ninaweza kuelewa kwanini hauwezi kuona mambo makubwa aliyoyafanya Mwakyembe kwa ajili ya Kyela na Tanzania kwa ujumla,keep it in ua mind....ufisadi una indirect effect kwenye kila nyanja ya maisha katika nchi maskini kama zetu.
 


duh njaa kweli mbaya,mwakyembe akishindwa ndo we kula hakuna?jifunzeni kujitegemea wa nyumbani....unasema mambo ya kitaifa inamaana mwakyembe hawezi kuendesha mambbo ya kitaifa na yale ya kyela kwa pamoja?
 
duh njaa kweli mbaya,mwakyembe akishindwa ndo we kula hakuna?jifunzeni kujitegemea wa nyumbani....unasema mambo ya kitaifa inamaana mwakyembe hawezi kuendesha mambbo ya kitaifa na yale ya kyela kwa pamoja?

Hivi wewe una majina mangapi humu?
 


Hawa ndio tunaowaita Watanzania! wanawaza kiwilaya wakati chanzo cha tatizo la umasikini wa watanzania ni hao huko juu wenye kula bila kunawa. Inpofikia hatua ya mtu kuhoji eti kwa nini dereva wa Dr. Mwakyembe anaitwa Msuya ujue hapo kuna tatizo kubwa. SIKULAUMU.

Kugombea ni haki yangu, nikitaka nitakuja na sitokuwa kama nyinyi wa sitaki nataka, mara sitaki mara nataka!!!!!!!

Sisi Kyela tunaelewa Mbunge wetu ni nani na msidhani kuwa ni washamba sana wa kubabaishwa na kuishi Ulaya, wapo vijana wengi tu wa Kyela wenye kuishi Ulaya na Marekani kwa hiyo hilo sio jambo la ajabu kwetu.

Narudia huyo mtu wenu anafanya cheap pilitics na ni kwa sababu kakubali umamluki wa kina Mwakipesile.

Leo hii tunaelezwa eti huko nyuma alishirikiana na Mwakipesile akiwa Mbunge, thubutu! Wote mligwaya mkamuomba Dr. Mwakyembe aende Kyela ili aung'oe mlouita mbuyu wakati huo (Mwakipesile), leo hii mmepata uhuru mnanyanyua midomo kwamba mnaweza.

Subirini 2010 sio mbali na msije kukimbia baada ya kuukosa huo ubunge. Ushauri mdogo tu, msimdangaye jamaa kwa ajili ya kukomba vijisenti vyake anavyosotea huko Ulaya!!!!!

Kumbe Rai ilisema kweli, wapambe wanasubiri kumchuna, na watamchuna kweli akamuulize Thom Mwng'onda!!!!!!
 
SteveD,

Vipi leo vidole na lips vimebanwa kwa SUPERGLUE mkuu? Talk!Talk!Talk please ....nasubiri comments zako on this mkuu!
SteveD kafulia mbaya na waraka wake.......yaani ni ile nitoke vipi......alafu kumbe mwakalinga alikuwa kwa ma mvi kudaka mishiko? steveD lazima andike waraka mwingine.....
 

Hakuna la kuongeza Mkuu, kama kweli ni mwelewa atachukua ushauri wako. Tatizo kafumbwa macho na wajanja, hivyo ushauri wowote ulio kinyume na mtazamo wake hauoni
 

Nsesi,

Kama akipoteza hela, si zake? Hajaiba Tanzania na sanasana atakuwa kawaibia Wachina wake anaofanya nao kazi huko. Wee YANAKUHUSU?

Kwani nani kasema MWAKALINGA ATASHINDA? Hapa inasemwa kuwa atagombea. Na wala hajasema "NINAGOMBEA". Hivyo kuna hatua mbili inabidi azipite. Kwanza NITAGOMBEA (yupo sasa), baadaye ije NINAGOMBEA, na mwisho ndiyo ije NIMESHINDA au NIMESHINDWA.

Kitu chochote chaweza kutokea hapa katikati hata akashindwa kusema NINAGOMBEA.
Tatizo lenu nyie kambi ya DR. mnataka kufanya kiti cha ubunge cha Kyela ni mali ya Mwakyembe. Mtu mwingine akipishie mbali kama mama mkwe. Nilifikiri Wanyakyusa mmechangamka, kumbe nyie ni WASHAMBA kiasi hicho? Au ni wewe tu Nsesi na kambi yako?

Vipi ile tume ya kuchunguza ajali ya Dr. imeishia wapi? Mwambie huyo Msuya aendeshe vizuri na kuwa mwangalifu. Atakuulieni kaka yenu na uendeshaji mbaya. Kama ni kaka yenu anamuamuru, basi mwambieni kaka yenu kuwa "Bado mwampenda, kama yeye hajipendi".
 
Kwa system mpya ya kura za maoni hakuna uwezekano wa Mwakalinga kumshinda Mwakyembe Kyela 2010,anyway...mzunguko wa pesa unaongezeka sana wakati wa kampeni na ni jambo zuri kwa maendeleo ya wananchi wa kawaida pale fursa hiyo inapotumiwa vizuri,na wajanja wengi wanajua 2010 ni wakati wa kuchuma pesa kutoka kwa wagombea,.......akili ku mukichwa!!
 
Huyu Mwakalinga naye ana ufisadi potential. Nyie subirini tu...kama akibahatika kushinda mtaziona rangi zake za kweli.
 
This is my honest opinion and I stand to be corrected. I look at politicians with 2 possible angles/spheres of influence. First - in his/her constituency and Second - nationally. Wanasiasa wa TZ wapo ambao wamelala, wengine active ktk mambo yao majimboni, na wengine mambo ya kitaifa, wengine mchanganyiko wa majimboni na mambo ya kitaifa.
Mwakyembe ametetea sana maslahi ya taifa hili, na anajitahidi hata jimboni, sasa anaetaka kumuondoa kweli atuthibitishie kuwa yeye ana nguvu zaidi ya Mwakyembe, na si vinginevyo. Sijui wenzangu mnaopenda kuingia ktk siasa nia yenu inakuwa nini hasa, je ni kupata ubunge tu au kutetea maslahi ya wananchi. Huo ndio uzalendo, sio kuweka historia kuwa ulishawahi kuwa mbunge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…