Huku nyuma tulishasema Mtanzania ndiye Mwakalinga, tukatukanwa, leo hii imedhihiri. Tulitishwa kwamba anazo data za wachangiaji fulani hadi mmoja kutilia mashaka MODs kwamba yawezekana kuna uwezekano ID za watu zinafichuliwa. Naamini JF ni jamvi lenye malengo yake mazito kwa taifa hili kuliko siasa za Kyela, lakini Mwakalinga a.k.a Mtanzania aliligeuza kuwa jamvi la siasa za Kyela, waelewa tulilishitukia hilo na tukaamua kukaa kimya. Naye ID yake ilipobainika kupitia uchangiaji wake akakimbia, najua bado yupo kwa jina jingine anapochangia kwenye siasa za Kyela.
Tatizo haliko kwa yeye kugombea Kyela, la hasha bali ni pale alipogeuza jamvi hili kama jukwa lake la kufanyia kampeni na hata kinachoendelea hapa ni kumpamba aonekane ni mzalendo wa kweli wakati sio kweli, na wakati ukifika itabainika kama ilivyo sasa.
Mwandishi wa Majira hajapika kitu, huyu ni mpambe wake na ndio maana hakutaka waandishi wa habari wengine wahusike. Hivyo hajatafuniwa maneno, kilichoandikwa ndicho alichotaka kitoke, na hapa ndipo udhaifu wake unapojibainisha kwa mara nyingine tena.
Mwakalinga haelewi kuwa utaratibu kura za maoni umebadilika, amekumbatia UVVCCM ambao siku zote chaguzi kwao ni gulio la rushwa, na tayari wameanza kupingana wenyewe kwa wenyewe kila mtu kutaka kuwa karibu naye, na watamla kweli kweli.
Kutokana na kujitambulisha kwake kuwa mwanzilishi wa JF ni lazima aweke bayana humu isije ikawa ndiye MOD mwenyewe, la sivyo JF inapoteza umaarufu wake siku si nyingi, wengine sio wataalamu wa IT, tutakosa imani na jamvi hili kwa sababu litakuwa na sura ya mtu au watu.
Pamoja na kumkaribisha Kyela, yeye pamoja na wapambe wake wanapaswa kufahamu mambo makuu ya muhimu kwa siasa za Mbeya.
1. Unapotaka kugombea ni lazima ujiridhishe kuwa unakubalika na wananchi a sio viongozi wa CCM. Dr Mwakyembe tangu ajitose Kyela hakuwa chaguo la CCM, viongozi wote waliimba wimbo wa Mwakipesile akiwemo shemeji yake aliyekuwa Mwenyekiti CCM Wilaya, lakini aliwabwaga, na hadi leo ngome yake kuu ni wananchi na wala sio viongozi wa CCM.
2. Kuingia kwa gia ya kupigiwa debe na kina Mwakipesile, RA na EL ni mweleka tosha katika siasa za Mbeya, huku hawataki viongozi wa kuchongewa, na hilo ndilo linalomtesa Thom Mwang'onda. Mwakalinga anaeleweka kuwa kapelekwa na Mwakipesile kwani huyo RC anapita akiwaeleza wananchi huko kuwa anawapelekea kijana toka UK, utapigiwaje kampeni na mtu aliyechafuka! Alimpigania THOM kwenye U-NEC akitumia ma DC wote na viongozi wa CCM bado alibwagwa vibaya.
3. Ujasiri na misimamo ni moja ya sifa za kuwa kiongozi Kyela, Mwakalinga ameshaonyesha woga, leo aseme sigombei, akiandikwa kidogo kuwa anagombea anatuma wake wapambe kutishia waandishi wa habari, halafu anakuja tena kutangaza anagombea, hawezi kubalika. Moja ya kete nzito ya Dr Mwakyembe Kyela ni ujasiri, anachukuliwa kuwa taswira hasa ya watu wa Kyela, hasa pale alipoisoma ripoti ya Richmond bila kupepesa macho.
4. Fitina, uongo na inda anavyovionyesha hapa kupitia baadhi ya wachangiaji kuhusu Dr havimsaidii kabisa zaidi ya kumwonyesha kuwa yeye ni mtu wa aina gani. Mara amejenga ghorofa kwa fedha za KDF, mara sijui huko Dodoma kaja na lexus, mara hana nyumba Kyela nk.
5. Kampeni za kuwafanya wana Kyela kuendelea na utegemezi hazimsaidii chochote, e.g kila mtu laptop, nitaibadilisha Kyela kuwa kama Ulaya, nitatoa ajira, zinaeleweka kuwa ni ghiliba za CCM miaka nenda rudi, kwani walishambiwa Maisha bora kwa Kila Mtanzania na hawayaoni.
6. Akumbuke kuwa tunahita kiongozi mwenye mtanzamo wa Tanzania na sio kieneo- Kyela, matatizo ya kitaifa kama vile ufisadi uliopo huko juu ndio ukoma unaoitafuna nchi, tukisafisha huko juu ni wazi huku chini kila kitu kitaenda sawa.
Mwisho niseme kwamba ni mjinga tu ambaye hawezi tambua mchango wa Dr. Mwakyembe kitaifa na jimboni mwake Kyela.
Mwakalinga a.k.a Mtanzania karibu sasa Kyela utugawie hizo laptop nasi tukawauzie wenye kuelewa jinsi ya kuzitumia kisha pesa tukanywee KADANSANA kutoka Malawi!!!!!