FairPlayer
JF-Expert Member
- Feb 27, 2006
- 4,145
- 723
mkulu wenu nasikia anakwea pipa sasa hivi......
huyo sikonge nimemwambia ni kilaza na nina mashemeji vilaza wawili JF yeye na Nyani Ngabu....???? ama una maana 1000km/hr
Msiwe na wasiwasi,
Mwakalinga ni mie hapa. Kama kuna mtu ana ubavu na aje tuzichape. Kama huna basi nakugambira kufront ya Ru-pabiliki lwa watu - shatapu!!
Niko huru kufanya nilipendalo, so longer sijavunja katiba wala sheria ya UK au Tanzania. Nitaamua lini na wapi niseme nagombea ubunge na si kijitu fulani kianze kunisemea. Nitagawa misaada na kitu chochote kwa wananchi wenye kuhitaji. Wengine wanashangaa mie kugawa Laptop, khaa, Laptop? Unafikiri uwezo wangu uko chini namna hiyo? Mie nitagawa hadi Mbuzi za kukunia NAZI. Eeeee, any problem with this one?
Nitaenda popote pale Tanzania na duniani na kukutana na mtu wa aina yoyote, hata kama ni Yo Yo. Kwani Yo Yo chi Ntu? Kama chi ntu ni ......... tete teteeeteee.
Nawasalimia kutoka kwenye PIPA la QATAR AIR, 10 km from dunia ya MAJUNGU na UFISADI. Tutaonana kesho jioni nikishafika London.
Boss la IT na Telecominications (Mbunge wa Kyela Mtarajiwa)- Ms Eng. Computer Science.
uzuri wake upi?The guy is good
FP
Sikutegemea utakuwa mtu wa kununua habari za Kanda2. Maelezo ya Kanda2 anayemaliza na Mwakalinga Oyeeeee!!!!! yanatosha kabisa kujua UPUPU ulioko ndani. Na bado mtu unasoma na kujichanganya humo?
Sikonge kama nimekusoma vizuri, upo sana kambi ya Mwakalinga..sawasawa na mpiga debe Kanda2.....right? Kama ilivyo machango wa member yeyote tuna haki ya kusoma na kudadisi mchango wa Kanda2 uwe wa uwongo au ukweli mpaka tujiridhishe kuwa ni either uwongo au ukweli!
Kwa kesi hii, wale wa Kambi ya Dr. wamekuwa wakidai Mwakalinga alienda Monduli kumwona EL ....lately jana wewe ukaja na hadithi ya hukohuko Monduli but kutembelea mjane wa kaka yake (hili halikuwahi kutamkwa kabla ya wewe tangia thread imeanza)......ndipo nilipo ona kuna coincidence fulani and hence either madai yako ni sahihi au wongo na yale ya kambi ya Dr. ndo sahihi au ya uwongo! Usitegemea tu nitachgua upande kama sina sababu na vigezo vya kutosha mkuu takuwa mnafiki.....so point ya confusion ilikuja hapo!
Kwa sababu huku maanisha!Mbona mie nimeandika kuwa Mwakalinga ndiyo mie na sijakuchanganya?
Mkuu tuko interested na Monduli not Karatu au kula sijui kulala etc....!Juu ya kwenda Monduli/Arusha. Je unafikiri Mwakalinga alipokuwa Arusha aliishia kutembelea mbuga za wanyama tu? Hakula, hakulala, hakununua ticket? Hakuongea na watu? Mbona hapa imeandikwa kuwa alienda hadi Karatu na hakuna mtu aliyelifuatilia hilo? Ila hilo haulioni?
Kwani wee unapokuwa kwenu kuwatembelea wazee huwa unaishia hapo tu? Si unaanza kupepesa macho vibinti vya majirani? Nasikia kamoja huwa ukifika tu, lazima ukatafute, si ukaowe tu?
Ha!ha!ha!ha!ha!...mkuu please nitake radhi......!
SIKONGE acha uchochezi! Huwezi ukawa boss la IT & Telecommunications mwenye Msc. Eng.(Computer Science) halafu unafanya vibarua zaidi ya vinne kwa siku jijini London: kufua nguo, kufagia ofisi ya IT, kulisha nguruwe chakula nk! Wote tumeishi Ulaya,tunajua maisha ya kubangaiza yakoje. Mwacheni Mwakalinga bila kulazimisha watu kumchokonoa zaidi kwa kauli za utanitani kama hizo!
Washikaji nipo Uwanja wa Ndege wa Mwalimu JK Nyerere kumsindikiza mwana JF mwenzetu, George Ambwene Mwakalinga, ambaye alikuwa Kyela kufanya vitu vyake vya kisiasa. Anaondoka sasa hivi na ndege ya Shirika la Ndege la Qatar kwenda London kupitia Doha. Ndege inaondoka sasa hivi(yaani saa saba na nusu).
Hivi majuzi jina la Mwakalinga lilitawala vyombo vya habari nchini kwa kuwania kiti cha ubunge cha Kyela kinachoshikiliwa na Mbunge maarufu nchini, Dk. Harrison Mwakyembe. Anatarajiwa kufika Doha jioni na boarding pass yake inasema ataondoka Doha saa sita usiku hadi Heathrow, London ambapo mshikaji ataingia mapema alfajiri kesho.
Mimi nilimpokea Mwakalinga alipoingia nchini wiki mbili zilizopita na nilikuwa miongoni mwa wale waliomsindikiza katika kujinadi kwa viongozi na wananchi wa Kyela. Ni wajibu wangu vilevile kuwaeleza kuwa anaondoka!
Kalengama
PakaJIMMY,Ameenda kufuata zile `laputopu` za wanakyela wote!
Nimeuliza UFISADI wa Mwakalinga naona jamaa nimewakimbiza.
Leteni jipya.
huyo sikonge nimemwambia ni kilaza na nina mashemeji vilaza wawili JF yeye na Nyani Ngabu....
Fataki,
Kumbe ndiyo wee unafanya kazi pale ZOO???
Kisa ni hiki:
Zoo ya UK moja ilipungukiwa wanyama, wakaamua kuwavisha watu ngozi za wanyama. Fataki nakumbuka ukaamuwa kwenda kuwa Mnyama wa zoo. Ukavishwa ngozi ya Gorila na ukaanza kurukaruka kwenye miti na kufurahisha watalii. Siku moja baada ya mvua kunyesha, ukateleza kwenye na ukaanguka moja kwa moja chini na hapo alikuwepo Simba. Nikasikia kilio "Mama wee, leo nakufaa". Mie nikakujibu " Kelele wee, mie siyo Simba ila Mbongo mwenzio".
Ilikuwa safi sana na watalii wakashangaa kuwa wanyama wanaongea!!!
Mhandisi wa IT na Telecominications.
ufisadi wa Mwakalinga ni kufadhiliwa na mafisadi - mtoto wa Kikwete.
Hivi Mwakalinga yuko wapi asafishe hewa kwenye maandishi kama haya? Yaani haiwezi kwenda low zaidi ya hii.
Mtoto wa Kikwete azua balaa kwa Mwakyembe
Kundi la vijana lapanga kumfanyia vurugu kwenye harambee
na Moses Ng'wat, Mbeya
HARAMBEE ya kuchangisha fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), wilayani Kyela, mkoani hapa, iliyopangwa kufanyika juzi, imeshindwa kufanyika kutokana na kile kinachodaiwa kuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo, mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete, kushindwa kufika.
Habari za uhakika kutoka ndani ya umoja huo wilayani Kyela, zilidai kuwa Ridhiwani ambaye ni mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa, akiwakilisha Mkoa wa Pwani, alishindwa kufika kwenye hafla hiyo iliyopangwa kufanyika katika ukumbi wa Kyela Business Center (KDF), kwa madai ya kuwapo kwa kundi la vijana lililopanga kufanya vurugu, kwa sababu za kisiasa.
Vyanzo vyetu vya habari kutoka Kyela, vinadai kuwa kundi hilo la vijana ambalo halijulikani liko upande gani, lina hofu kuwa harambee hiyo ilikuwa na lengo la kumjenga mmoja wa vijana (jina limehifadhiwa), anayedaiwa kutaka kuwania kiti cha ubunge katika jimbo hilo ambalo kwa sasa linashikiliwa na Mbunge machachari bungeni, Dk. Harrison Mwakyembe.
Kwa mujibu wa habari hizo, Ridhiwani alitarajia kufika katika ukumbi huo majira ya saa mbili za usiku juzi, lakini licha ya vijana kuwapo kwa wingi wakimsubiri mgeni huyo rasmi, hakuweza kutokea na hakuna sababu zilizotolewa na kusababisha harambee hiyo ishindwe kufanyika.
Ilipofika majira ya saa nne usiku, minong'ono ilianza kuzagaa ndani ya ukumbi huo kwamba huenda mtoto huyo wa Rais Kikwete, alishindwa kufika kutokana na taarifa za kiusalama kwamba kuna kundi lililoandaa vurugu ili harambee hiyo isifanyike kwa hofu za kisiasa.
Baadhi ya wanachama wa UVCCM, waliozungumza na Tanzania Daima kwa sharti la kutotaja majina yao, walisema baada ya kukwama kufanyika kwa harambee hiyo, kuliibuka makundi mawili ndani ya ukumbi huo, moja likifurahia kutofika kwa Ridhiwani, likiamini kuwa limeshinda, huku jingine likihuzunika kwa kutofanyika kwa shughuli hiyo.
Hata hivyo kundi lililokerwa na kushindwa kufika kwa Ridhiwani, lilielekeza lawama zake kwa uongozi wa jumuiya hiyo kwamba haukuwa na uhakika na kitu walichokiandaa na kwamba hiyo ni ishara ya uongozi huo kushindwa kutekeleza majukumu mbalimbali ya umoja huo, ikiwamo kushindwa kuwashawishi vijana kuachana na siasa za makundi katika wilaya hiyo.
Akizungumzia hali hiyo, Mwenyekiti wa UVCCM, mkoani Mbeya, Reginald Msomba, alikiri kuwapo kwa ziara ya Ridhiwani mkoani mwake kwa ajili ya kuwa mgeni rasmi kwenye harambee hiyo ya kuchangia fedha kwa ajili ya miradi ya vijana wilayani Kyela.
Alisema yeye kama mwenyekiti wa Umoja huo, alipewa taarifa za ziara hiyo kwamba Julai 31, mwaka huu, alitakiwa ampokee mjumbe huyo wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana Taifa kutoka mkoani Pwani ili kwenda naye Kyela kwa ajili ya shughuli hiyo.
Kwa kweli jambo hilo lilikuwapo ndugu mwandishi, lakini mimi nilishangaa kutompokea mgeni huyo ambaye tulikuwa tuongozane naye hadi Kyela, lakini hadi majira ya jioni hakutokea na mimi nilipewa taarifa za kuelekea huko bila maelezo mengine," alisema Msomba bila kufafanua alikokuwa akipata maelekezo hayo.
Alipotakiwa kueleza sababu za kuahilishwa ghafla kwa ziara hiyo wilayani Kyela, alisema yeye hawezi kulizungumzia hilo kwa kuwa liko nje ya uwezo wake, na kuongeza kwamba watu waliopaswa kulizungumzia ni viongozi wa umoja huo Wilaya ya Kyela.
Juhudi za kumpata Mwenyekiti wa UVCCM Kyela, Hanta Mwakifuna, kwa njia ya simu kutoka Kyela zilifanikiwa, lakini hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo, hususan sababu za kushindwa kufika kwa mgeni rasmi Ridhiwani Kikwete.
Mimi sidhani kama kuna haja ya suala hili kupelekwa kwenye vyombo vya habari, kwa kuwa hata utaratibu wa kumualika hatukuufanya kupitia vyombo vya habari, naomba unielewe kuwa shughuli haikufanyika na sasa tunaangalia jinsi ya kuandaa upya, sihitaji kukuambia kama alifika au hakufika," alisema.
Alipotakiwa kuelezea iwapo kushindwa kufika kwa Ridhiwani kumekwamisha malengo ya umoja huo wilayani Kyela, mwenyekiti huyo alisema lengo lao halikutimia, na kusisitiza kuwa wanajipanga upya kumwita kwa ajili ya harambee hiyo.
Kuhusu tetesi za kuwapo kwa kundi lililopanga kumfanyia vurugu mgeni huyo kwa sababu za kisiasa, Mwakifuna alikanusha taarifa hizo, kwa madai kuwa si sahihi.
Alisema hafikiri kama kuna vijana waliochochewa kufanya vurugu, kwa kuwa kazi hiyo ililenga kufanikisha uchumi wa miradi ya vijana wa chama hicho.
Taarifa hizo ni za kisiasa tu na hazihusiki kwa namna yoyote na kutofika kwa Ridhiwani," alisema bila kutaja sababu nyingine iliyomfanya Ridhiwani kutofika kwenye harambee hiyo.
Alisisitiza kuwa harambee hiyo itafanyika katika tarehe itakayopangwa upya. Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, UVCCM wilayani Kyela katika harambee hiyo walitarajia kukusanya zaidi ya sh milioni 155, ambapo hadi kufikia juzi, walikuwa wamekusanya sh milioni 21.9, zilizochangwa na watu mbalimbali, wakiwamo vijana wa umoja huo kutoka kata zote 21 za wilaya hiyo.