Invisible nashukuru kwa maelezo lakini inasemekana kuwa huyu jamaa anaufadhili mtandao huu,imeandikwa kwenye magazeti yanayoheshimika sana hapa nchini (like Mwananchi la jumatatu).
Nadhani si mimi tu peke yangu niliyenazo habari hizi nawe umezisikia mahali pengine. Habari hii ilivyoandikwa inaonesha kama ufadhili wake ni wa kipekee tofauti na uchangiaji wa hao uliowataja.
Ni siasa za wanasiasa... Wanajua namna ya kutumia Print Media kupindisha ukwelui. Wambieni hao Majira/Mwananchi kuwa Mimi Invisible nimeandika na kumkana waziwazi Mwakalinga kuwa mfadhili wa JF na kuhusika kwa namna yoyote katika kuanzishwa kwake... Wanachama wa mwanzo kabisa kujiunga na JF Mwakalinga nadhani ni mmojawapo lakini akijiunga miezi 3 baada ya JF kuanzishwa, hivyo basi hata wewe jiulize amehusikaje na kuzishwa kwa JF... Technically and financially.
Pia jamaa anavyozungumziwa humu JF ni kama vile ni mtu maarufu sana hapa ndani kama akina Mwanakijiji na hiyo inaleta hisia kwamba labda huyu mtu kweli ni kama magazeti na vyanzo vyetu vingine visemavyo.
Mwanachama yeyote hapa JF (aliyejisajili) anajenga credibility yake kwa michango yake. Huenda kuna wanaofahamu Mwakalinga ni nani (username) na hivyo kuhusudu uandishi wake (Am not good at name calling and I do not entertain that on these forums). Wanaomtetea basi ni kwa mapenzi yao binafsi, hajataka kutetewa na JF na JF haitafanya kazi hiyo kwa wakati huu. Kaongea na wenzetu walio Dar na kakana kugombea ubunge na kasema ni mikakati ya kuhakikisha hagombei (kama ana nia hiyo).
Nina imani na JF,sitaki kuamini kuwa tunataka kuchukua nafasi ya kuuza wagombea,lakini tuwe makini. Wachangiaji wa fedha wawe wazi na wawekwe wazi ili tuondoe "conflict of interest". JF inaheshimika sana,kama mtu akisoma habari jinsi ilivyoandikwa kwenye gazeti na akaona jinsi Mwakalinga anavyouzwa humu JF ataamini kuwa mtandao huu umegeuka kama sehemu ya kampeni za baadhi ya wagombea.
Kwakuwa hujachangia sikulaumu, waulize waliochangia wanauzwa wapi. Hivi kwanini uamini JF ipo kumuuza mtu? Tofautisha wanachama na Management ya uendeshaji JF. Hatuwezi kuwazuia wanasiasa kufanya kazi yao ya siasa, lakini mwisho wa siku historia itawahukumu.
Sikutaka kutia neno katika hoja hii lakini imenilazimu tu. Premium Members wana heshima yao kama wawezeshaji wa JF. Wewe ni mwanachama na ungekuwa umesoma JF ungeona JF ranking inakwendaje na ungeweza kujua kuwa hao walioandika habari juu ya Mwakalinga kuwa mfadhili wa JF walichanganya madawa na hawajui walitendalo.
Mpaka sasa mwanachama aliyeichangia kiasi kikubwa sana cha hela ni Mukubwa (if am not mistaken)... Kauzwa wapi? Lakini heshima yake inabakia palepale kuwa ni mtanzania wa kipekee aliyejitolea kila mwezi kuichangia JF kuhakikisha inaendelea kuwepo!
JF ina members wengi sana na hata wanasiasa wanaweza kuitarget kama sehemu ya kujiuzia. Pia JF ni chanzo cha habari nyingi sana kwani mabo mengi yanatoka hapa ndiyo tunayaona magazetini. Kama mgombea akiweza kuteka JF ana weza kuteka magazeti mengi yanayochukua habari zake hapa.
Mkuu hii ni public forum... Msimamo wa JF utatolewa na Invisible, Silencer, PainKiller au Ab-Titchaz. Msemaji mkuu wa JF atakuwa ni JamiiForums katika masuala nyeti sana.
Naomba usichukulie mawazo binafsi ya mwanachama kuwa msimamo wa JF. Na tunapoandika kama msimamo wa JF unaweza kutumia busara yako kujua hapo tunamaanisha msimamo wa JF! Maoni yangu binafsi ni rahisi kuyatambua pia.
Suala la Mwakalinga lilikuwa closed topic,iweje lirudishwe kama new post wakati lilishaongelewa na kufungwa. Mwakalinga ni nani mpaka akapewa publicity kubwa kiasi hiki katika JF? Hili linanipa mashaka kwa nafasi ya huyu bwana katika JF. Tunaomba ukweli wa jambo hili kama inawezekana.
Umejitahidi kulalamika, nashindwa kujibu kila mstari. Naamini umenisoma mkuu...
Sijajua mnaoomba 'ukweli wa jambo' mko wangapi. Ila nashauri tumieni busara zenu kung'amua msimamo wa JF na maoni ya wananchi.
JAMII FORUMS Where We Dare to Talk Openly!
Kusema "Where We Dare To Talk Openly" haileti maana ya kuwa ni kuongea openly kuupotosha ukweli mkuu Mponjoli. Changia JF kisha uone kama hutakuwa na status ya Premium Member. Yani hata Tshs 5,000 yako inaweza kukuingiza kwenye kundi la wawezeshaji wa JF. Sasa wewe ndo utakuwa mfadhili?
Asante kwa clarification hiyo mkuu.....I thought kwa sababu ya IDs zetu kufichwa pengine yes Mwakalinga is Max or Robot etc!
BWT: Haya meneno ya Kanda2 (quoted below) yanatoka wapi?.....i.e Mwakalinga, Mwanzilishi, Mdhamini, Mmiliki, IT expert wa JF ......and lots of bla blas yanatoka wapi sasa!
Mkuu NL,
Hata wewe kwakuwa ni Premium Member utasikia ukitajwa kuwa mdhamini, mmiliki na mwanzilishi wa JF hahahahahaha!
Kama Robot yupo sahihi (which I believe he is) we Kanda2 unaimong'onyoa sana credibility ya Mwakalinga coz unamsemea uwongo hapa....vinginevyo bishana na Robot!
Kanda2 ndo maana ilibidi kumfungia. Yeye mwenyewe hata Tshs 5,000/= hajatoa kuiwezesha JF, kishaanza speculations ati Mwakalinga ni mwanzilishi, mdhamini, IT expert etc... Uwongo daima una ukweli nyuma yake. Ndo alichofanya mkuu mmoja aliyeleta link toka Wikipedia ambayo inaonesha nani mwanzilishi na mwendeshaji wa JF.
Mmechelewa sana kuaction Mods....au mlitoa onyo kwanza?
Mkuu tunatoa onyo kwanza, tunawakumbusha watu sheria za JF zinasemaje wakiendelea tunawafungia kwa muda mfupi, wakizidi tunawafungia permanent (usernames) na wakionekana kukaidi basi tunatoa server ban!