Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM

Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM

Anaufadhili mtandao huu?

Waliochangia kwa mwaka huu wanapatikana hapa:



Hakuna mfadhili zaidi ya hao! Wengine wamechangia miaka ya 2007 nao hakuna alochangia zaidi ya $200!

Haya maneno ya ati ni mfadhili wa JF au mwanzilishi sijui yanatoka wapi! Labda kama yumo kwenye list hiyo.

Asante kwa clarification hiyo mkuu.....I thought kwa sababu ya IDs zetu kufichwa pengine yes Mwakalinga is Max or Robot etc!

BWT: Haya meneno ya Kanda2 (quoted below) yanatoka wapi?.....i.e Mwakalinga, Mwanzilishi, Mdhamini, Mmiliki, IT expert wa JF ......and lots of bla blas yanatoka wapi sasa!

Kama Robot yupo sahihi (which I believe he is) we Kanda2 unaimong'onyoa sana credibility ya Mwakalinga coz unamsemea uwongo hapa....vinginevyo bishana na Robot!

sio mwanzilishi tu bali pia ni mdhamini.mfuko wake uko wazi kuichangia JF ili wewe uje kutumia huduma ya bure.elimu yake ya Computer ndio iliyotuletea starehe hii JF.

akitajwa Mwakyembe mnakuja juu nyinyi nani aliyewapa authority ya kumtaja mh.Mwakalinga kwa ID yake?

ama kweli binadamu hatuna shukrani tuko kwenye jamvi la Mwakalinga na kupitia jamvi lake tunamtukana. unafikiri JF mwanzilishi wake ni Mwakyembe? ama kweli wewe huna adabu kabisa unakula matunda ya Mheshimiwa Mwakalinga na unatumia platform aliyoiasisi kwa manufaa ya watanzania kumtukana. ingekuwa JF tunalipa membership fee wewe usingekuwepo hapa.

Hongera Mheshimiwa Mwakalinga kazi ulizotufanyia JF na ulizowafanyia wana Kyela tunalazimika kukuita Mheshimiwa Mbunge hata kabla ya 2010 kutinga rasmi Dodoma.

ni fahari kwetu sisi wa
na Jamii Forums kuona mwenzetu anatuwakilisha bungeni wenye wivu mnaweza kula sumu maana kamba inachelewesha kifo.

Kwa Taarifa yako, kaka yake Mwakalinga (Marehemu) alikuwa akiishi Monduli miaka ya 80 na akaolea huko mama wa Kimasai na wakawa na watoto. Sasa Mwakalinga kama Ambwene, na family man, ni wajibu wake (amejipa yeye) kuwahudumia mama na watoto.
.

Mbona hii habari inauchanganya sana.....mara oooh alienda Arusha kutalii mbugani....tena we unakuja na mambo ya kuona mjane Monduli.......?????? what a coincidence?

Kuna ban zaidi ya 20 zinakuja tokana na name calling katika topic hii.

Sheria hii imezingatiwa katika kufanya maamuzi haya:



Nasikitika kwa watakaoathirika na mamauzi haya.

Atakayeendelea kukiuka atapata Server ban and that will be a permanent one.

Mmechelewa sana kuaction Mods....au mlitoa onyo kwanza?
 
Mwakalinga ni fisadi na anaandaliwa na mafisadi kulinda ufisadi kama ilivyo kwa ngeleja na malima. Hana ubavu wowote wa kuwaletea wana Kyela maendeleo. Aseme ana nini kipya anaweza kukifanya Tanzania na kyela zaidi ya kufizia ruzuku na fadhila za waliomshauri kuja kuleta kitimtim.
 
Jamani;

Kwani kuna ubaya Mwakalinga kujadiliwa humu? ni sawa na Chadema walivyojiandikisha wengi humu mpaka watu wakadai JF ni ya Chadema, kumbe ni uzembe wetu CCM wa kukumbatia viongozi wazee wasiojua hata Blogs ni kitu gani, wanaishia kuwatuma ma secretary wao kuwasomea na kuwapa update!!

Joji tupo pamoja mkuu, rudi ulete mambo mapya uliyojifunza huko nje!!

FP
 
Invisible nashukuru kwa maelezo lakini inasemekana kuwa huyu jamaa anaufadhili mtandao huu,imeandikwa kwenye magazeti yanayoheshimika sana hapa nchini (like Mwananchi la jumatatu).

Nadhani si mimi tu peke yangu niliyenazo habari hizi nawe umezisikia mahali pengine. Habari hii ilivyoandikwa inaonesha kama ufadhili wake ni wa kipekee tofauti na uchangiaji wa hao uliowataja.
Ni siasa za wanasiasa... Wanajua namna ya kutumia Print Media kupindisha ukwelui. Wambieni hao Majira/Mwananchi kuwa Mimi Invisible nimeandika na kumkana waziwazi Mwakalinga kuwa mfadhili wa JF na kuhusika kwa namna yoyote katika kuanzishwa kwake... Wanachama wa mwanzo kabisa kujiunga na JF Mwakalinga nadhani ni mmojawapo lakini akijiunga miezi 3 baada ya JF kuanzishwa, hivyo basi hata wewe jiulize amehusikaje na kuzishwa kwa JF... Technically and financially.

Pia jamaa anavyozungumziwa humu JF ni kama vile ni mtu maarufu sana hapa ndani kama akina Mwanakijiji na hiyo inaleta hisia kwamba labda huyu mtu kweli ni kama magazeti na vyanzo vyetu vingine visemavyo.
Mwanachama yeyote hapa JF (aliyejisajili) anajenga credibility yake kwa michango yake. Huenda kuna wanaofahamu Mwakalinga ni nani (username) na hivyo kuhusudu uandishi wake (Am not good at name calling and I do not entertain that on these forums). Wanaomtetea basi ni kwa mapenzi yao binafsi, hajataka kutetewa na JF na JF haitafanya kazi hiyo kwa wakati huu. Kaongea na wenzetu walio Dar na kakana kugombea ubunge na kasema ni mikakati ya kuhakikisha hagombei (kama ana nia hiyo).
Nina imani na JF,sitaki kuamini kuwa tunataka kuchukua nafasi ya kuuza wagombea,lakini tuwe makini. Wachangiaji wa fedha wawe wazi na wawekwe wazi ili tuondoe "conflict of interest". JF inaheshimika sana,kama mtu akisoma habari jinsi ilivyoandikwa kwenye gazeti na akaona jinsi Mwakalinga anavyouzwa humu JF ataamini kuwa mtandao huu umegeuka kama sehemu ya kampeni za baadhi ya wagombea.
Kwakuwa hujachangia sikulaumu, waulize waliochangia wanauzwa wapi. Hivi kwanini uamini JF ipo kumuuza mtu? Tofautisha wanachama na Management ya uendeshaji JF. Hatuwezi kuwazuia wanasiasa kufanya kazi yao ya siasa, lakini mwisho wa siku historia itawahukumu.

Sikutaka kutia neno katika hoja hii lakini imenilazimu tu. Premium Members wana heshima yao kama wawezeshaji wa JF. Wewe ni mwanachama na ungekuwa umesoma JF ungeona JF ranking inakwendaje na ungeweza kujua kuwa hao walioandika habari juu ya Mwakalinga kuwa mfadhili wa JF walichanganya madawa na hawajui walitendalo.

Mpaka sasa mwanachama aliyeichangia kiasi kikubwa sana cha hela ni Mukubwa (if am not mistaken)... Kauzwa wapi? Lakini heshima yake inabakia palepale kuwa ni mtanzania wa kipekee aliyejitolea kila mwezi kuichangia JF kuhakikisha inaendelea kuwepo!

JF ina members wengi sana na hata wanasiasa wanaweza kuitarget kama sehemu ya kujiuzia. Pia JF ni chanzo cha habari nyingi sana kwani mabo mengi yanatoka hapa ndiyo tunayaona magazetini. Kama mgombea akiweza kuteka JF ana weza kuteka magazeti mengi yanayochukua habari zake hapa.
Mkuu hii ni public forum... Msimamo wa JF utatolewa na Invisible, Silencer, PainKiller au Ab-Titchaz. Msemaji mkuu wa JF atakuwa ni JamiiForums katika masuala nyeti sana.

Naomba usichukulie mawazo binafsi ya mwanachama kuwa msimamo wa JF. Na tunapoandika kama msimamo wa JF unaweza kutumia busara yako kujua hapo tunamaanisha msimamo wa JF! Maoni yangu binafsi ni rahisi kuyatambua pia.

Suala la Mwakalinga lilikuwa closed topic,iweje lirudishwe kama new post wakati lilishaongelewa na kufungwa. Mwakalinga ni nani mpaka akapewa publicity kubwa kiasi hiki katika JF? Hili linanipa mashaka kwa nafasi ya huyu bwana katika JF. Tunaomba ukweli wa jambo hili kama inawezekana.

Umejitahidi kulalamika, nashindwa kujibu kila mstari. Naamini umenisoma mkuu...

Sijajua mnaoomba 'ukweli wa jambo' mko wangapi. Ila nashauri tumieni busara zenu kung'amua msimamo wa JF na maoni ya wananchi.

JAMII FORUMS Where We Dare to Talk Openly!

Kusema "Where We Dare To Talk Openly" haileti maana ya kuwa ni kuongea openly kuupotosha ukweli mkuu Mponjoli. Changia JF kisha uone kama hutakuwa na status ya Premium Member. Yani hata Tshs 5,000 yako inaweza kukuingiza kwenye kundi la wawezeshaji wa JF. Sasa wewe ndo utakuwa mfadhili?

Asante kwa clarification hiyo mkuu.....I thought kwa sababu ya IDs zetu kufichwa pengine yes Mwakalinga is Max or Robot etc!

BWT: Haya meneno ya Kanda2 (quoted below) yanatoka wapi?.....i.e Mwakalinga, Mwanzilishi, Mdhamini, Mmiliki, IT expert wa JF ......and lots of bla blas yanatoka wapi sasa!

Mkuu NL,

Hata wewe kwakuwa ni Premium Member utasikia ukitajwa kuwa mdhamini, mmiliki na mwanzilishi wa JF hahahahahaha!

Kama Robot yupo sahihi (which I believe he is) we Kanda2 unaimong'onyoa sana credibility ya Mwakalinga coz unamsemea uwongo hapa....vinginevyo bishana na Robot!
Kanda2 ndo maana ilibidi kumfungia. Yeye mwenyewe hata Tshs 5,000/= hajatoa kuiwezesha JF, kishaanza speculations ati Mwakalinga ni mwanzilishi, mdhamini, IT expert etc... Uwongo daima una ukweli nyuma yake. Ndo alichofanya mkuu mmoja aliyeleta link toka Wikipedia ambayo inaonesha nani mwanzilishi na mwendeshaji wa JF.

Mmechelewa sana kuaction Mods....au mlitoa onyo kwanza?
Mkuu tunatoa onyo kwanza, tunawakumbusha watu sheria za JF zinasemaje wakiendelea tunawafungia kwa muda mfupi, wakizidi tunawafungia permanent (usernames) na wakionekana kukaidi basi tunatoa server ban!
 
Jamani;

Kwani kuna ubaya Mwakalinga kujadiliwa humu? ni sawa na Chadema walivyojiandikisha wengi humu mpaka watu wakadai JF ni ya Chadema, kumbe ni uzembe wetu CCM wa kukumbatia viongozi wazee wasiojua hata Blogs ni kitu gani, wanaishia kuwatuma ma secretary wao kuwasomea na kuwapa update!!

Joji tupo pamoja mkuu, rudi ulete mambo mapya uliyojifunza huko nje!!

FP
Nowadays CHADEMA nao wameisha JF! Sijui kama umeshtukia hilo. Kabakia Dr. Slaa peke yake
 
Ndo alichofanya mkuu mmoja aliyeleta link toka Wikipedia ambayo inaonesha nani mwanzilishi na mwendeshaji wa JF

Asante sana invisible kwa ufafanuzi wa Kina Ilibidi kuperuse kuona Mh Mwakalinga katoka wapi na JF, kwenye wikipedia hakuwepo....lakini magazeti yameisha muuza....very cheap and low!
 
Asante sana invisible kwa ufafanuzi wa Kina Ilibidi kuperuse kuona Mh Mwakalinga katoka wapi na JF, kwenye wikipedia hakuwepo....lakini magazeti yameisha muuza....very cheap and low!
tehe tehe tehe shem labda wame mu edit si unajua wikipedia....

Wambieni hao Majira/Mwananchi kuwa Mimi Invisible nimeandika na kumkana waziwazi Mwakalinga kuwa mfadhili wa JF na kuhusika kwa namna yoyote katika kuanzishwa kwake.....
hoja closed unless aje akanushe andiko lako......sasa tunabaki na idea zake za kuleta laptop kyela.....na mengineyo.....huyu jamaa msanii sana tehe tehe arudi majira waambie alikosea wa edit....
ila atakana tu ngoja msemaje wake mkuu SteveD aje na waraka wake.....
 
Nowadays CHADEMA nao wameisha JF! Sijui kama umeshtukia hilo. Kabakia Dr. Slaa peke yake

Duh hata Mh.Zitto kala kona nashangaa hata John Mnyika kijana kabisa anashindwa kuchungulia chungulia ili apate uzoeefu hapa? Wale wazee wa CCM wanavijana wao wanang'amua tu humu kisha wanawapelekea.
 
Shem Y

Nadhani SteveD ameisha kufa tusubiri matanga yake, tumemtafuta aje na waraka wake kala pori, ila anachungulia JF kwa chat....


huyu jamaa msanii sana tehe tehe arudi majira waambie alikosea wa edit....
ila atakana tu ngoja msemaje wake mkuu SteveD aje na waraka wake.....
 
Jamani huyu Mwakalinga ni nani?

Chechenya Mwakalinga ni mbunge mtalajiwa wa jimbo letu la kyela.We si ulikuwa naye rungwe,Tambaza, UDSM na Sokoine?baadaye akapotelea majuu.ndo huyohuyo
 
Nilikuuliza katika hao, wahandisi gani ni wa IT na Telecomicanitions?
hivi na wewe ni shem wangu?.....basi nina mashem vilaza wawili humu JF wewe na nyani ngabu
 
hivi na wewe ni shem wangu?.....basi nina mashem vilaza wawili humu JF wewe na nyani ngabu

Yo Yo,

Itabidi uwe unapita mitaani na kujisifu kuwa Sikonge wa JF ni shemeji yangu. Wee Sikonge jina kubwa ati. Wengine hadi wanafikiri mie Mwakalinga, wengine wanafikiri mie Dr. wengine wanafikiri ......

Sasa wewe unatoa sifa ya siye vilaza? Hii sifa ni sifa moja nzito sana pale inapotolewa JF. Respact all vilaza wa JF. Inabidi nibaki nayo mie peke yangu (warning, kama wee si mtani wa Wanyamwezi na hujaowa au kuolewa huko, basi utumiaji wa neno KILAZA unaweza kukuletea MATATA).

Kwanza wajua Sikonge inatamkwa vipi weee? Hatausemi kibantu Sikonge, ila twasema "Kinyamwezi" - SAIKONG. Ndiyo maana unaona watoto wa MUJINI wanasema "Unyamwezini", "Wanguwangu", "mwanawane" ......
 
Chechenya Mwakalinga ni mbunge mtalajiwa wa jimbo letu la kyela.We si ulikuwa naye rungwe,Tambaza, UDSM na Sokoine?baadaye akapotelea majuu.ndo huyohuyo

Huu sasa ni KUCHAFULIANA to power 4. Yaani mtu jina lake unalibadili na kumwita Chechenya Mwakalinga? Unataka na wewe tukushukie? Wee Mnyakyusa wee. Hebu kwanza angalia dental forumula yako. Unafikiri una uwezo wa kuja na kuanza kumwaga pumba zako hapa kuita watu majina ya ofyo ofyo? Jamaa kasota ki-vyake na mwakani atakuwa mbunge wako. Ita unavyotaka kuita. Kama usiporidhika na ushindi wake mwakani JINYONGE.
Kama unaogopa kujinyonga, basi kunywa sumu au nenda Ziwa nyasa kajitupe, ila usifie karibu.

Mtu kama wee utakuwa ki-JEBA fulani, cheusi kaa chungu cha Makande ya Kipare, roho KOROSHO ile mbaya na mkono wa BIRIKA. Kama Mnyakyusa mwenzio Mwakalinga ni Chechenya, wee ni IMBOMBOGASTAN aka Afganistan?
 
I love some members humu, kwa kuua character siwawezi. Mtu hata humjui ushaanza ni fisadi! mweh!!
 
Kumbe mwakalinga anapewa shavu hapa JF sababu anaufadhili mtandao huu?
KWELI MKONO MTUPU HAULAMBWI. Huyu jamaa hana Historia yoyote ya maana ya uzalendo na taifa letu,anatafuta namna ya kurudi nchini.
Naomba mnaomwita engine mtoe wasifu wake na mchango wake kwa maendeleo ya Tanzania.
.

Weee kweli ndiye mponjoli.Uko nyuma kama koti.

Hiyo Kyela Fm Radio inamilikiwa na nani?Na wale vijana wote wafanyakazi wa hiyo radio,Hotel na supermarket sio Watanzania?.

Ongea kama msomi na toa dataz
 
I love some members humu, kwa kuua character siwawezi. Mtu hata humjui ushaanza ni fisadi! mweh!!

kwani fisadi ni kumjua au ni tabia yake. wengi hawamjui Rostam, Chenge , Mgonja, manji, Yona, mramba, Dr. Idrisa, balali, Mwanyika, Lowasa, Hosea, Karamag nk ila hilo halitufanyi tusijue ufisadi wao. Ufisadi ni tabia na matendo pamoja na mwelekeo, mtoto wa nyoka ana matendo ya kinyoka.

Ukiingizwa kwenye siasa na mafisadi unakwenda kuwa fisadi na una-serve mafisadi, tusitetee mtu tuwaache wajitetee wenyewe kwani wako hai.
 
Wambieni hao Majira/Mwananchi kuwa Mimi Invisible nimeandika na kumkana waziwazi Mwakalinga kuwa mfadhili wa JF na kuhusika kwa namna yoyote katika kuanzishwa kwake...

Wamekusikia Mkuu, nahisi wakati unaandika huu ujumbe kama angetokea jamaa wa Majira/Mwananchi angekula konzi.

Hili suala kweli yawezekana huyu Mwakalinga kuna mbinu ya kumchafua, lakini kama alizungumza kweli washauri wake wanatakiwa kujipanga upya. Hivi kweli unaenda kuwaeleza watu (tena ushagoni) mimi ni mfadhili wa JF ama mtunza hazina wa Tanzanet, sidhani hata kama wanakuelewa unasema nini. Kweli huyu jamaa wamemponza waliomlipua.

Ila kaza buti Mwakalinga, ila kuwa mwangalifu na watu wanaokuzunguka na pia yale utakayozungumza.
 
kwani fisadi ni kumjua au ni tabia yake. wengi hawamjui Rostam, Chenge , Mgonja, manji, Yona, mramba, Dr. Idrisa, balali, Mwanyika, Lowasa, Hosea, Karamag nk ila hilo halitufanyi tusijue ufisadi wao. Ufisadi ni tabia na matendo pamoja na mwelekeo, mtoto wa nyoka ana matendo ya kinyoka.

Ukiingizwa kwenye siasa na mafisadi unakwenda kuwa fisadi na una-serve mafisadi, tusitetee mtu tuwaache wajitetee wenyewe kwani wako hai.


Ufisadi wa George Ambwene Mwakalinga ni UPI?

Weka wazi na sio kukashifu watu bila angalau ka piece ka evidence.
 
Ufisadi wa George Ambwene Mwakalinga ni UPI?

Weka wazi na sio kukashifu watu bila angalau ka piece ka evidence.

Keep ur eyes and ears open, time will tell. tell me ur friends and i will tell ur character. do u get that.
 
Back
Top Bottom