Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM

Hii inaitwa "Wape wape vidonge vyao, wakimeza wakitema shauri yao".

We call it fighting fire with fire (wimbo wa Kenny Rogers).

Kama huu ndio mpango wa kushindana kisiasa wa Mwakalinga, yaani kulinganisha watu na wanyama, kukashifu wenzake, basi wazee wa Kyela watabidi watafute pamba za kuziba masikio.

Mambo mengine nii too much kwa watu wengi wanaopenda ustaarabu kwenye masuala ya kisiasa. Katika hili, mnaenda low zaidi ya viwango vya kawaida vya siasa. Na huu pia ni ufisadi.
 

Good observation Semilong,

unajua kuna watu wanaamini kuwa mtoto wa Kikwete hakujiingiza kwenye hili suala la uchaguzi wa Kyela bila baraka za baba yake. Kama ulimsoma vizuri mzee wa data FMES, mtoto wa Kikwete asingemchagua Mwakalinga over Mwakyembe bila kuwa na sababu maalumu.

Hapa kunaonekana kama kuna mkono mzito ulio nyuma ya kampeni ya George Mwakalinga. Usishangae kukuta kuwa mtoto wa Kikwete analazimishwa tu na watu wengine ambao hawana ubavu wa kwenda kumpinga Mwakyembe kwa wazi.

Hata hivyo nakubaliana nawe, huyu Ridhiwani angekaa mbali kwenye mambo kama haya maana huwa hayana mwisho mwema. SIjui angefanya nini kama watu wa Kyela wangefanikiwa kumpiga mawe kama ilivyokuwa imepangwa.
 
Huyu Mwakalinga msanii tu,haeleweki hata kidogo,mara aseme hili mara lile.
 
 
Wapi Kanda2?

kalengamab
Junior Member
Join Date: Fri May 2009
Posts: 4
Thanks: 1
Thanked 2 Times in 2 Posts
 
Semilong!
Nakushukuru kwa kuliona hilo. Huyu kijana alipata sehemu ya zile pesa za Deep Green iliyofilisiwa na Laurence Masha amabaye alipewa zawadi ya kazi nzuri na JMK awe Waziri pamoja na kuwa ni mwanasheria kilaza kama alivyo Ridhwan mwenyewe. Wazungu wanasema "" Show me your friend and I will tell you who you are"" Nimeweka soft Kiswa- kinge ili ieleweke kwani nimelenga waTz!!!
 
inatishaaaa!
ikitokea wana ccm wa kyela watamtosa mwakyembe
wajue jimbo hilo limepotea. Kwani ccm sio wenye mamlaka ya mwisho.
 
 
Kalengamab huyu mwakalinga hata atakaposhindwa kwenye kura za maoni mwaka 2010 pia usisite kutupa taarifa kama ulivyotoa taarifa ya kumsindikiza uwanja wa ndege! Ila nakukumbusha tu kuwa" only the wise can dance the melody of the night" na kama mwakalinga ni msikivu basi yatosha kusema" words are enough for the wise"
 
Ndugu zangu wanaJF. Kwanza, napenda niwathibitishie wote kuwa MWAKALINGA SI FISADI! JAMANI SI FISADI HATA KIDOGO! Ni kijana wa Tanzania anayeishi Ulaya ambaye anatumia haki yake ya kidemokrasia kurejea nyumbani na kugombea ubunge, PERIOD! Anahitaji tumuunge mkono badala ya kumkatisha tamaa! Mimi ni mwandishi wa habari, nimekuwa karibu sana na kundi lake la kampeni katika ziara yote aliyofanya ndani na nje ya Mkoa wa Mbeya, hususan Kyela.
Tatizo linalomkabili Mwakalinga mpaka wengine wanamfikiria kuwa Fisadi ni ukaribu wake na campaign team ya Mwakipesile, ile ile ambayo Mwakyembe aliibwaga mwaka 2005! Kazi tuliyonayo wenzake ni kumtoa huko kubaya alikojichimbia, si kuzuri!
Mwakalinga anaelewa vema kuwa kabla ya kuja kwake Mwakipesile amefanya ziara ya Wilaya nzima kumfagilia njia. Hivyo si vema kwa Mwakalinga kumthibitisdhia kila mtu kuwa yeye ni mtu wa Mwakipesile! Mwakalinga ameishi kwa muda mrefu mno Ulaya hivyo hajui kuwa Mwakipesile ni mwanasiasa aliyepoteza ushawishi na mvuto wa kisiasa wilayani Kyela. Hivyo basi kwa kujihusisha sana na Mwakipesile, anajihusisha na matatizo ya Mwakipesile! Hali hii inamsaidia sana Mwakyembe kupata sympathy ya watu dhidi ya kundi ambalo wanaamini limekuwa likimsakama mbunge huyo machachari tangu 2005 kwa kuwa alimuunga mkono kaka ya Mwandosya wakati wa kinyang'anyiro cha Urais. Mwakipesile na wenzake akina Mzee Apson Mwang'onda na Mulla, hawaelewi kuwa alichofanya Mwakyembe ni heshima kwa Rungwe na Kyela! Wao wanadhani ni kosa, hivyo apigwe vita! Ni kukosa upeo mzuri wa siasa kwa Mwakalinga kuingia kwenye kundi hilo ambalo limefunga ndoa na mafisadi akina Lowassa, Chenge, Karamagi na Rostam Aziz!
Mwakalinga tumemweleza, lakini haelewi kitu kuwa mwezi wa nne mwaka huu Lowassa alikuja Kyela, akalala nyumbani kwa Mwaitenda, rafiki mkubwa wa Mwakipesile. Kyela wanajua!
Hivyo basi, huyu kijana si Fisadi, ila kwa namna moja au nyingine na kwa bahati mbaya sana, Mafisadi wako karibu naye.
 
kalengamab Junior Member
Join Date: Fri May 2009
Posts: 5
Thanks: 1
Thanked 2 Times in 2 Posts

kalengamab

Haya mwandishi wa Mwakalinga tumekusoma, lakini mbona kuna wapiga debe wake wadiriki kusema ni heri CCM wapoteze jimbo iwapo Mtanzania hata pitishwa na SiSiem kugombea Kyela? Kuliko Mwakyembe kuendelea kuongoza jimbo!
 
Ndugu yangu naomba sana, huko msiniingize, sikuwezi. Mimi nilikuwa natoa maoni yangu tu ya dhati maana naona mjadala unayumba.
 
CCM kwa mapandikizi siwawezi,yangu macho ila wana Kyela huwa hawaburuzwi!
 
Kalengamab nimekupata na nimekuelewa na umekiri wazi wazi kuna connection ya wazi kati ya Mwakipesile na EL sasa na huyu EL anajulikana kama fisadi sasa huoni kama Mwakalinga nae anajuumuka na hao mafisadi maana wanamsafishia njia unataka tumuweke wapi au kundi lipi?
 

Hapa umenena vyema sana ......Sikonge Upo hapo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…