Ndugu zangu wanaJF. Kwanza, napenda niwathibitishie wote kuwa MWAKALINGA SI FISADI! JAMANI SI FISADI HATA KIDOGO! Ni kijana wa Tanzania anayeishi Ulaya ambaye anatumia haki yake ya kidemokrasia kurejea nyumbani na kugombea ubunge, PERIOD! Anahitaji tumuunge mkono badala ya kumkatisha tamaa! Mimi ni mwandishi wa habari, nimekuwa karibu sana na kundi lake la kampeni katika ziara yote aliyofanya ndani na nje ya Mkoa wa Mbeya, hususan Kyela.
Tatizo linalomkabili Mwakalinga mpaka wengine wanamfikiria kuwa Fisadi ni ukaribu wake na campaign team ya Mwakipesile, ile ile ambayo Mwakyembe aliibwaga mwaka 2005! Kazi tuliyonayo wenzake ni kumtoa huko kubaya alikojichimbia, si kuzuri!
Mwakalinga anaelewa vema kuwa kabla ya kuja kwake Mwakipesile amefanya ziara ya Wilaya nzima kumfagilia njia. Hivyo si vema kwa Mwakalinga kumthibitisdhia kila mtu kuwa yeye ni mtu wa Mwakipesile! Mwakalinga ameishi kwa muda mrefu mno Ulaya hivyo hajui kuwa Mwakipesile ni mwanasiasa aliyepoteza ushawishi na mvuto wa kisiasa wilayani Kyela. Hivyo basi kwa kujihusisha sana na Mwakipesile, anajihusisha na matatizo ya Mwakipesile! Hali hii inamsaidia sana Mwakyembe kupata sympathy ya watu dhidi ya kundi ambalo wanaamini limekuwa likimsakama mbunge huyo machachari tangu 2005 kwa kuwa alimuunga mkono kaka ya Mwandosya wakati wa kinyang'anyiro cha Urais. Mwakipesile na wenzake akina Mzee Apson Mwang'onda na Mulla, hawaelewi kuwa alichofanya Mwakyembe ni heshima kwa Rungwe na Kyela! Wao wanadhani ni kosa, hivyo apigwe vita! Ni kukosa upeo mzuri wa siasa kwa Mwakalinga kuingia kwenye kundi hilo ambalo limefunga ndoa na mafisadi akina Lowassa, Chenge, Karamagi na Rostam Aziz!
Mwakalinga tumemweleza, lakini haelewi kitu kuwa mwezi wa nne mwaka huu Lowassa alikuja Kyela, akalala nyumbani kwa Mwaitenda, rafiki mkubwa wa Mwakipesile. Kyela wanajua!
Hivyo basi, huyu kijana si Fisadi, ila kwa namna moja au nyingine na kwa bahati mbaya sana, Mafisadi wako karibu naye.