Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM

Nadhani kama wewe ni mpiganaji lazima utumie udhaifu wa adui kumaliza kazi. Mwakalinga lazima akae na mmoja wapo kumaliza aliye mbele yake.
Mkuu wa mkoa sio fisadi na sisi hatuwezi kumchagulia marafiki.
Mwakyembe amekuwa akijiingiza makanisani kufanya kapeni chafu na kuwapotosha waumini kitu ambacho hata Mungu hakimpedezi.
Amekaa kwenye mgongo wa Reginald Menghi kama njia ya upataji pesa na kujaribu kujinusuru na hatimaye kushinda.
Kgwamaka
 
Mwafrika, mawazo yako yanaelekeana na yule mpumbavu Kalengama kwa kudai kuwa Mafisadi wako karibu na Mwakalinga. Kalengama ni mwongo na hatukumbuki kuwa na mwandishi wa habari kama huyo Kyela!

Asante sana mkuu Msonda,

na wewe mawazo yako yasiyo ya kipumbavu (masikini timu Mwakalinga imefika this low) yatakuwa yanaelekeana na nani vile ??
 

Mkuu, kumbe hizi ndiyo siasa za Mbeya wanazotusimulia hapa kila kukicha.

Sasa kama kutangaza tu kutaka kugombea ubunge watu wanaporomosha hadi mitusi, hivi hali itakuwaje wakati wa kampeni?maana najaribu kuiangalia hii movie ilivyoanza na kushika mwendokasi wa ajabu ilihali bado kuna takribani mwaka mzima hadi kufika kwenye zoezi la kura za maoni. Yaani sipati picha itakuwaje Kyela mwaka kesho wakati kampeni zitakapoanza rasmi.

Kwakweli Mbeya/ Kyela mna siasa zenu mnazijua wenyewe, yaani watu wanatoleana macho utadhani wameahidiwa ufalme wa mbinguni!!
 
Mwafrika, mawazo yako yanaelekeana na yule mpumbavu Kalengama kwa kudai kuwa Mafisadi wako karibu na Mwakalinga. Kalengama ni mwongo na hatukumbuki kuwa na mwandishi wa habari kama huyo Kyela!

Hehehehe kumbe mpo wengi sana. Naona laptop mlizo ahidiwa zinawachengua ni siasa tu mkuu.
 
Mwafrika

Kwa kifupi huyu dogo Mwakalinga hafai kabisa sababu hasimami kama yeye nyuma yake kuna kundi kubwa la watu wachafu, ambao wanamchafua na yeye kama alikuwa bado hajazama kwenye dibwi la Uchafu. Hao Akina RC, EL RA, Mwaitenda et al lazima kuna agenda ya siri ambayo yeye Mtanzania na timu yake hawajaliona. Ni hatari sana kuwapa madaraka watu wa namna hii, muda mwingi watautumia kuridhisha hao mabwana waliomweka madarakani kuliko wananchi waliompigia kura....Ujinga mtupu wapambe wake wanajaza hapa, anaishi ughaibuni, sasa wale watanzania waliozaliwa ughaibuni itakuwaje? waweke CV yake hapa, na amwage sera zake ataeleweka, sina chuki naye wala sihitaji kumjua, ila gear ya reverse anayoitumia kuondokea ataharibu gari lake.

Kuwa na kajihotel (sijui hata kama inahadhi ya 1 star hotel) kuwa grocery aka supermarket mnajua maana ya supermarket ? wanakyusa bwana !! imekuwataabu kwa wapambe nuksi, mara kata zote kachukua ....nani kakwambia wewe kenge (sorry nimechukia) mara hakuna engineer wa tel Tanzania, my a.s.s hakuna mbunge engineer pumba tupu jamani. Baada ya kubanwa ooohh alipitia Monduli kusalimu shemejie mfiwa, eti Lowassa alikuwa Dodoma nani kakwambia? Unategemea George ni Zuzu hata akipotoka akubali, kwa taarifa tuna jua hata kiini cha mazungumzo yake na Mzee wa Thailand Lowassa

Give us a break wakuu

Mas
 
Kalengama ni mwongo na hatukumbuki kuwa na mwandishi wa habari kama huyo Kyela!

Ni hulka ya binadamau kusahau, hakuna kosa mlilofanya hapo!
 
Mwafrika, mawazo yako yanaelekeana na yule mpumbavu Kalengama kwa kudai kuwa Mafisadi wako karibu na Mwakalinga. Kalengama ni mwongo na hatukumbuki kuwa na mwandishi wa habari kama huyo Kyela!

Embu fikiria kidogo mkuu.....kama suala ni upumbavu, tuwe wakweli hapa ...hivi kati yako na Kalengamab nani Mpumbavu zaidi?

Kalengamab anakwambia amekuwa na Mwakalinga tangia ameingia hapa Tz two weeks ago, akaenda naye huko wilayani Kyela kama mwandishi, amemsindikiza leo Air port kukwea pipa, wamemweleza uhusiano kati ya Mwakipesile na EL, Ridhiwani na RA na ameonekana kutokubaliana kirahisi kutoka kny mikono ya Mwakipesile kwasababu wapo very close.....!

Hajasema yeye ni mwandishi kutoka Kyela...au waandishi wote wa habari wanatoka Kyela bosi?

Wewe unakuja na kusema tu mwenzio mpumbavu bila hata kutoa hoja yeyote ....kama sio Mpumbavu bana!
 
Sijaona jipya? huyo mwakalinga kama anataka kugombea ubunge si afanye hivyo tu, kwani si mdigo mwenzetu!!! alaaaaa!!!

lakini hana jipya na kama ni kweli basi anatafuta cheap popularity kwa kuonesha kushindana na Dr. Mwakyembe. Ningemuona wa maana zaidi kama angesema anataka jimbo lenye mbunge Fisadi kama jimbo la r.a au jimbo la rich wa monduli n.k
 
Kimsingi, ntaongea kirefu zaidi kesho! Ila kwa sasa...huyu Bwana Mwakalinga nadhani atapoteza saana na ni bora achague jimbo lingine kabisa!

Sisi kama wanamapinduzi na wanaharakati harakatini, lazima tuseme kuwa, Mwalinga ni mali na aweza kuwa zao la ufisadi mwingine.

Anaishi Ulaya sawa, amejuaje matatizo ya Kyela huyu, watu wanapigana wanauana, watu hamzungumzii hali hii, mnapigiana mapande ya uongozi tu kwa ajili ya 2010!

Trsut me people, mshaurini, na ofcoz namshauri Mwakalinga, aendelee na miradi yake ya ukandarasi, nadhani inamfaa, hana haiba ya kisiasa. Jamani hana marafiki wa kumshauri huyu?

Nipende kuwashukuru kwa kunisoma..kesho ntakuja na mambo mazito zaidi kuonesha namna ambavyo Mwakalinga ni zao la ufisadi.

See you poeple.
Hosana Juu Mbinguni.
DSM
 
 
Location: Dar es Salaam
Posts: 1
Thanks: 0
Thanked 0 Times in 0 Posts

Hawa member wapya balaa...jina la zamani nani vile? Karibu JF, tunasubiri data zaidi!
 

Nakushukuru Mkuu. Huyu Kapela nahisi namfahamu pamoja na kutumia jina tofauti,ni wale wasanii wa kisiasa wilayani Kyela ambao hawana msimamo kabisa. Akija Mwakyembe wapo, Mwakalinga wapo! Wao wanajali fedha tu! Undumila kuwili ni ajira!

Kwa kuwa amenitukana na hajaanza leo huyu jamaa, basi mimi sasa namwaga analysis yangu ya kweli kuhusu huyu "Mbunge Mtarajiwa", potelea mbali. Nataka nimwonyeshe kuwa anayoyajua na mimi nayajua!
Mwakalinga ameweza kupita Kata zote za Kyela kupima upepo. Kwa ujumla upepo si mzuri sana kinyume cha matarajio. Tutake tusitake bado wananchi hawajamkinai Mbunge wao. Aidha, viatu vya Mwakyembe ni vikubwa mno kwa Mwakalinga ambaye ana tabia tofauti kabisa na mpinzani wake: si mcheshi, si mvumilivu wa mawazo tofauti, hana uzoefu wa kisiasa (anaamini mno watu. Anaamini hata matapeli wa kisiasa akina Kapela alimradi wamemsifia), hana upeo wa kutosha wa elimu kufanya tathmini halisia na kusoma alama za nyakati na, kwa kifupi, ana papara.
Alipofika tu, kosa kubwa alilofanya ni kumhakikishia kila mtu aliyekuwa karibu yake kuwa anaungwa mkono na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mwakipesile pamoja na wapambe wake wakubwa: Nawab Mulla, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa na Cornel Apson Mwang’onda, aliyekuwa Mkuu wa Usalama wa Taifa. Alidhani kwa kufanya hivyo, atakubalika zaidi!
Amefanya vikao kadhaa na wazee hao ambao kabla ya kuja kwake walikwenda mbio sana kuwatangazia wananchi wa Kyela kuwa “Mkombozi wa Kyela Anakuja”! Ilibidi Mwakipesile azue ziara ya kiserikali ya “uongo na kweli” wilayani Kyela mwezi uliopita ili kumsafishia njia George Ambwene Mwakalinga kwa kukutana na madiwani wote wanaomsikiliza, wenyeviti na makatibu wa CCM wa Kata na viongozi wa UVCCM, UWT na WAZAZI wilaya ya Kyela.
Wote mnajua kuwa ziara ya Mwakipesile ikachafuliwa na vurugu za Kyela ambazo kwa kiasi kikubwa zilisababishwa na Polisi na yeye mwenyewe kuendekeza sana visasi hadi kuwajibu vibaya wananchi waliokuwa na hasira. “Leo ndiyo mnanijua; nendeni kwa huyo Mbunge wenu mkamlalamikie!”
Kundi la Mwakipesile liko kazini siku nyingi, kumsifia Mwakalinga na kumponda Mwakyembe. Linapewa posho nzuri sana. Kampeni hii inaendelea Kyela, Mbeya na Dar es Salaam. Kyela inaongozwa na jamaa mmoja wanamwita Makete; Dar es Salaam na jamaa anayeitwa Mwanjala na Mbeya na Mkuu wa Mkoa mwenyewe. Wote tulikutana Kyela alipokuja Mwakalinga! Kama si kweli, basi Kapela abishe!
Katika kampeni hii kila kundi linaongozwa na “mwongozo maalum” ulioandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambao una hoja 20. Vilevile si siri, Kapela anajua, fedha inatoka kwa Rostam kupitia kwa RC. Ndiyo maana kundi la washikaji ni kubwa. Wengi wao hawamtaki Mwakalinga, kwa sababu hawamjui vizuri, ila wanaitaka pesa yake!
Baada ya muda si mrefu nitawatumia mwongozo huo wa Mkuu wa Mkoa ambao Mwakalinga anaufuata kama biblia, kitu ambacho ni kosa kubwa!
 
kalengamab

Mungu baba akulinde sana uendelee kutupa hiki....ni wazi dogo Mwakalinga anasukumwa na Mafioso nyuma yake!
 
Mwongozo wa Mkuu wa Mkoa wa uendeshaji kampeni ya Mwakalinga, ambao kila mpambe wa Mwakipesile anao na sisi akina yakhe tunao, ni huu hapa:

"1. George ameanza kusaidia Kyela tokea alipokuwa mlimani kama mwanafunzi, wakati hakuwa na uwezo kabisa. Yeye na wenzake waliungana pamoja kuchangia walimu wanafunzi ili waje wafundishe shule za secondary Kyela wakati wa likizo. Wakati huo Mwakyembe alikuwa mlimani, alikuwa hana msaada, hata mikutano alikuwa hahudhurii na alikuwa anajulikana kama anatoka Rungwe.


2. Toka George aanze kazi kila mwaka hutumia mshahara wa mwezi mmoja kusaidia jamii mbalimbali Kyela zikiwemo shule, wanafunzi ambao wamekwama na matatizo mengine kama vile kuwasaidia walimu kudai mafao yao pamoja na wafiwa kufuatilia malipo ya waume zao wanao waliofariki.

3. Mpaka sasa George kishasaidia karibu kila kata na anaendelea kusaidia kadri mungu anavyompa uwezo.

4. George anapinga ugomvi na migawanyiko ya watu na anataka kuisaidia Kyela ili iweze kupiga hatua mbele kwenye maendeleo kuliko hata wilaya kama Rungwe ambayo haina utajiri kama Kyela. Baada ya uchaguzi anataka kuonana na watu wa makundi yote na kuwakutanisha pamoja kwa faida ya Kyela.

5. George amesoma, ametembea dunia, anajuana na watu wengi ambao watakuwa muhimu sana huko mbeleni wakati akitekeleza mipango yake ya kuiendeleza Kyela. Kwa mfano Kyela radio FM imetolewa na UN kupitia shirika la elimu, sayansi na utamaduni. Na sasa yuko mbioni kuanzisha tawi la Open University Kyela ili kila mwana Kyela anayetaka aweze kusoma mpaka uwezo wake utakapoishia.

6. Huko nyuma alipoona wana Kyela wanahangaika kwenye mikopo aliweza kuwashawishi PRIDE kutoka Tukuyu ili waje Kyela. Na mpaka leo PRIDE wanashukuru maana wamegundua soko la Kyela ni kubwa. Tunaamini wana Kyela wengi wamefaidika.Mpango wa baadaye ni kuungana na wana Kyela wengine kufungua bank ya wana Kyela ili wananchi waweze kujipatia mikopo na ushauri wa uhakika kwa faida yao .

7. George Ulaya ana kazi ya maana sana na ambayo kipato chake ni zaidi ya mara mbili ya ubunge.familia ilikuwa inataka aendelee kukaa huko na kuachana na siasa za majungu huku nyumbani. Lakini George ameamua kurudi baada ya usanii wa Mheshimiwa na amekubali pato lake litashuka sana lakini yuko tayari kuwatumikia wana Kyela kwa moyo wote kama ambavyo ameweza kuitumikia familia yake kwa muda mfupi na mpaka kufanikiwa kufungua kampuni kama KBC kwa kutumia pesa zake kwa miaka 10 tu ambayo amekuwa kazini.

8. George anataka kuzibadili shule na hospitali hasa ya Kyela ili ziwe za kisasa, kununua na kuomba vifaa kama magari ya wagonjwa na mashine za kutibia kutoka sehemu mbalimbali. Pia kuleta watu wa kujitolea kutoka nje kusaidia shule na hospitali ili ziwe na ubora na kupunguza vifo vya watoto na wanawake kama ilivyo sasa. George anataka kukomesha mambo ya kwenda Igogwe na Tukuyu kutibiwa, badala yake hospitali zetu zitakuwa bora hata zaidi.

9. George hataki ukubwa na muda wote anaishi maisha ya kawaida. Hahitaji
Shangingi na pesa za shangingi akipata anataka zitumike kununua magari ya wagonjwa kwa faidi ya jamii yote.

10.George amesaidia kuwaamsha vijana wa Kyela kwa kuwaletea ukumbi wa kisasa, kuona mipira kwenye TV kubwa na mpaka sasa vijana wa Kyela hawababaishwi tena na vijana wengine toka Dar. Huko mbele anataka kuimarisha huduma zingine mbalimbali kwa faida ya Kyela.

11. Kupitia KBC vijana wote wamekuwa wakipata vibarua KBC na kupata mahitaji yao muhimu. Lengo huko mbele ni kuimarisha ajira kwa vijana. Kwamba huko mbele anataka kusimamia mafunzo ya VETA na kuwapa vijana misaada ili wakajiajiri mijini, kuwasaidia vijana wanaotaka kujiunga na jeshi. Atakuwa wa kwamza kwenda kumpigia magoti Mwamunyange ili vijana zaidi waende jeshini, pia atasaidia vijana kujiunga na jeshi la polisi.

12.George anataka kurudi kwasababu ana uchungu na Kyela, anataka kusaidia Kyela akiwa bado kijana na nguvu zake badala ya kurudi uzeeni. Anataka wote waliosoma na kubaki Dar wawe na uhusiano na nyumbani, wajenge nyumbani, wasaidie nyumbani, matokeo yake vijana watapata kazi huku nyumbani. Waambie George anataka kuwasiliana na kila mwana Kyela ili kuwashawishi wafanye kitu chochote nyumbani ikiwemo kuwasaidia wazazi wao na wadogo zao.

13. Mheshimiwa hana uchungu na Kyela na alikuja Kyela baada ya kuwaogopa wale maprofesa kule Rungwe. Ndio maana muda wote anashinda Tukuyu.

14. Mheshimiwa anapoteza muda na Wachaga ambao wameendelea zamani huku kwake hakuna kitu, vijana wanahangaika bila ajira. Kwamba yeye Mwakyembe anachotaka ni uwaziri ndio maana kila sehemu anazunguka na waandishi wa habari ili wakuze jina lake.

15. Hata vita vya ufisadi na Richmond , data nyingi alipewa na akina George kutoka kwenye mitandao yao . mitandao ndio iliibua Richmond . Mwanzoni bunge walipuuza lakini watu wa mitandao wakazidisha nguvu na kutoa scandal zao mpaka bunge lilipokubali kuchunguza. Waambie George ni mdau mzuri kwenye mitandao ya Watanzania inayopinga ufisadi na viongozi wabaovu.

16. Mheshimiwa amekuwa mbunge miaka 9. ikiwa ni pamoja na bunge la East Afrika lakini hakuna alichofanya Kyela na badala yake kajenga jumba kubwa Dar ambali ni la anasa kuliko majumba ya mafisadi. Kwamba hata nyumba ya kwao Ikolo yeye hakai, ile alijenga ili tu kuwadanganya wana Kyela kwamba anatoka Kyela.

17. Mheshimiwa anakosana na kila mtu, hata George hakutaka kugombea sasa lakini Mheshimiwa anatumia ubunge wake kuikwamisha hata KBC. Alitumia akina Kifukwe kukwamisha CRDB kufungua branch KBC, alijaribu kuzuia radio isije Kyela na anapinga vijana wanaotaka kuendeleza Kyela.

18. Badala ya kuwapelekea wananchi maendeleo yeye anapeleka disco ili wacheze na kuambukizana ukimwi zaidi.

19. Anapenda makuu, daraja lililojengwa na jeshi tayari analiita daraja la kwake. Nyerere aliongoza miaka yote bila hata nyumba moja kuitwa jina lake. Angalau hilo daraja angeita daraja la Mwamunyanga.George hataki kabisa kutukuza jina lake na badala yake anatukuza Kyela, ndio maana kwenye kila kitu ameweka Kyela badala ya jina lake.

20. Mheshimiwa ameshindwa hata kushughulikia suala la maji na mabomba ya Wascandinavia badala ya kushughulikia ili yatoke maji, yeye ameyaacha na anashinda Dar, hajui hata Kyela kuna tatizo gani. Wapambe zake kazi kupeleka umbea tu."
 
- Irrelevant.

You betcha

- Another irrelevant, nilisema hakuna ushaidi wa kumtosa Masha na uwaziri, zaidi ya majungu na chuki za watu kama wewe, matokeo Masha bado ni waziri na anaelekea kwenye urais, na there is nothing you can do!

Wow ... kwa hiyo unasimama na Masha sasa. Kwa hiyo ufisadi wa Masha ni majungu tu ya watu kama mimi?

Hili ni jipya hapa jamvini (haichukui muda kuleta yote uliyoandika hapa baada ya Masha kuonekana fisadi na mchovu).


Na huyo mnafiki anayeuma huku na huku ni nani? Unaweza kumtaja?


- The little I know kuhusu George ninamuamini sana so far, nimeongea na Kifukwe na Kasyanju, watu wa karibu sana na DK, kuna mtu aliyedai George anajenga bara bara ya lami Kyela, hawa wakathibitisha kuwa ni uongo wa mchana.

Haya bado ni maneno yako binafsi ... sio ukweli mtupu au sio?

- George ana advantage moja kubwa sana nayo ni maadui wengi wa DK, ambao automatically wanakuwa washabiki wa George, kwa hiyo asisumbuliwe na kelele za mlango.

Yeah, advantage nyingine ya George ni kuungwa mkono na mafisadi. Kama vile mafisadi wa serikali ya Kikwete walisema kuwa kelele za wapinzani wake ni kelele za mlangoni, sitashangaa George naye akisema the same thing - ndege wenye mabawa yanayofanana huruka pamoja

Respect

FMEs!

Ushauri mzuri sana huu kwa George, wapuuzie wana JF kwa vile wao hawaamui nani awe mbunge wa Kyela. Kama vile Kikwete na Mramba na Lowasa na Rostam Azizi wanavyotakiwa kuwapuuzia wana JF kwa vile sio wao tu wanaoamua nani awe mbunge au kiongozi wa serikali.

Respect kwako pia
 
kweli mwakyembe kiboko mpaka wameamua kumtafutia blogger kutoka ulaya aje kushindana nae
inaonekana jamaa aliposema yeye ni muanzilishi wa JF mafisadi wakaona huyu ndio anafaa kabisa kuchuana na mwakyembe

binafsi kama ningekuwa napiga kura ningempigia mwakyembe na ni kwa sababu moja tu, amesimama mbele ya hawa wanyanyanyasaji wawili EL na RA, yaani ukiwakosea hawa ndani ya ccm ni kama vile gharika....
yani hawa jamaa wawili (EL & RA) wamewachafua sana watu kwa mfano SAS, magufuli, mwandosya na kumnyanyasa nape na wengine wengi (na bado puppet kibao JF wanawashabikia kwa hela ya soda) du!

anyway kuna ma puppet wa kutosha kule bungeni and we dont need anymore
mwakalinga another puppet in the making
 
Mwakalinga safari njema, ila fanya hima wale watu wako wa kampeni wachuje wanayosema, nawe uwe mwangalifu, silaha sasa zinakueekea.
Inakuwa ngumu kuchuja kama umeshalamba laptop na kuna ahadi ya kupata nyingine
 
Nakushukuru Mkuu. Huyu Kapela nahisi namfahamu pamoja na kutumia jina tofauti,ni wale wasanii wa kisiasa wilayani Kyela ambao hawana msimamo kabisa. Akija Mwakyembe wapo, Mwakalinga wapo! Wao wanajali fedha tu! Undumila kuwili ni ajira!

staili yako ya uandishi kwamba ,wewe mwandishi na blah blah kibao wengi tulijua ndo huko unaelekea.

Yani mbinu inayotumiwa sasa nikujaribu kumuunganisha Mwakalinga na kambi za watu waliopoteza dira halisi ili mpate kumchafua Mwakalinga.

Huyu lowasa kuhusu eti Mwakalinga yuko naye beneti ni uzushi tu amabo ulianza baada ya mtego wa kwanza kufeli kwamba Mwakalinga alikuwa tayari kelya akifanya kampeni na Invisible alipokuja na jibu la kwamba jamaa yuko Arusha basi wenye roho zao za korosho ndo wakadakia eti ameenda kwa lowasa tangu hapo ndio wavumishi wa mambo waliposhikilia.

Pigeni kampeni safi na siza kuchafuna ,mtu anayediriki kumchafua mwenzako ili ajipatie madaraka hakika hana nia njema kabisa na taifa ,mtu mwenye nia njema huwezi lazimisha uongozi ili uwaongoze. Kumchafua mwenzako ni dalili tosha ya dhamila ya mhusika husika.
 
Mwongozo wa Mkuu wa Mkoa wa uendeshaji kampeni ya Mwakalinga, ambao kila mpambe wa Mwakipesile anao na sisi akina yakhe tunao, ni huu hapa:

Ebwana ndiyo,

siasa za mbeya kweli tamu saaana.

kama huu mwongozo ndiyo anautegemea kwa ajili ya kumng'oa Mwakyembe, atakuwa amechemsha vibaya mno.

Halafu huu mbona sio mwongozo! haya ni majungu tu mbona hakuna chochote cha maana!

Kama hii ndiyo hekima ya Mwakipesile basi Mbeya bado safari ndefu sana kupiga hatua za kimaendeleo, ndio maana hata miradi mikubwa na mizuri kama uwanja wa ndege wa Songwe upo upo tu kama kambi ya wakimbizi.

Halafu kusema kweli hata kama mwakalinga ni mwenzetu hapa JF na tunahitaji kumuunga mkono ili afanikiwe kuingia mjengoni, sharti ajiepushe na watu wachafu.

Hakuna namna yeyote ataweza kusimamia maslahi ya watu wa kyela na Tanzania kwa ujumla kama nyuma yake ana support ya mafisadi.

Kila siku hapa tunamnyoshea vidole JK ameshindwa kuwachukulia hatua mafisadi kwa kuwa ndio waliombeba hadi kuingia magogoni, kwahiyo hatuwezi kutegemea lolote jipya toka kwa Mwakalinga kama anabebwa na fisadiz.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…