East Africa + Bunge la Muungano ni miaka mingapi?
Au utasema ni vyeo tofauti? OK.
Naomba niulize wakati nakubaliana na wewe kuwa ni vyeo tofauti.
Mwakyembe ametangaza kugombea tena Kyela?
Naona sasa zimeanza kurushwa namba za kuonesha uwezo wa kifedha wa Mwakalinga. Kama Mwakalinga ana pesa hizi zote na miradi yote hii, je ni kwa nini anataka kuwa mbunge wa Kyela?
Kwa nini asisaidie tu kama kina Bill Gates wanavyofanya bila kuingia kwenye siasa?
Mtanzania una jibu? Nafasi yako hapa ya kuelezea sera na sababu ya kutaka kuwa mbunge wa Kyela. Nimekurushia bonge ya soft question la ki-charlie Rose.
Mwafrika;
Swali zuri. Unapomaliza shule(yoyote) unaanza kazi ya chini, other things remain constant unapanda ngazi kwa ngazi, mpaka ufikie kuwa president wa kampuni inaweza kuchukua hata miaka 20. Hapo sina tatizo na wewe. Ndo issue kama ya Kikwete.
Dr miaka kumi inatosha, kwakweli tuweni na tamaduni ya kuachiana madaraka, hii ya akina Mugabe sio sahihi.
Mi nimeangalia kwa upana sio kwa issue hii ya Mwakyembe vs Mwakalinga
Mwakalinga kawekeza karibu dola 1 milion$ Kyela. Mwakyembe alikuwa awekeze Singida na akiwa na RA. Sasa basi kama wewe huna hizo 1m. na unaona donge, then go hang your self.
Hongera sana ndugu Mwakalinga kwa kuonyesha nia yako ya kugombea jimbo la Kyela. Majimbo hayajapigwa chapa ya mtu na kwa demokrasia ya Tanzania mtu yeyote yule anaweza kugombea uongozi au uwakilishi wa wananchi ili mradi wananchi wakubali sera zake na pia hizo sera ziwanufaishe.
Maneno matupu hayavunji mfupa. Go Mwakalinga go, usihofu wala kuogopa vitisho kwamba eti kuna mkono wa fisadi kwenye uamuzi wako huo ama vyovyote vile iwavyo.
Nakuombea kila la heri ndugu Mwakalinga, siasa za majungu na kukatishana tamaa Tanzania zifikie mwisho.
Mwanzoni mmetueleza hapa kwamba sababu ya kumleta mwakalinga kugombea jimbo la kyela ni kutaka aliletee maendeleo(nadhani mmeridhishwa na maendeleo yake binafsi; hoteli, ukumbi na mazagazaga mengine) sasa tena unapodai utamaduni wa kuachiana madaraka mbona hueleweki?
kwahiyo ni kweli kwamba mwakyembe ameleta maendeleo kyela isipokuwa mnacholilia ni utamaduni wa kuachiana madaraka!
Fataki yupo wapi?, ningependa aje apambane na Mtanzania ana kwa ana.
Najua upo bize mkuu na mastrategy ila usikimbie sana, Siku hizi hata kwenye simu unaweza kuingia kwenye net. Ndo maana tunataka viongozi wa kisasa wanaoenda na wakati.
Pole FATAKI dakika zina tick tick tick tick..
Mwakalinga ni fisadi tu kama mafisadi wengine CCM.
Take that with you rafiki yangu mapinduzi.
In order to take that with me, nionyeshe vielelezo vya kuonyesha kuwa ndugu Mwakalinga ni fisadi.
Zaidi ya hilo ningeshukuru kama ungeweka jina la mtu ambaye si fisadi anayeweza kugombea ubunge jimbo la Kyela.
Nyani,
Hukui tu?
1. Kuwa mwana ccm (chama cha mafisadi) ni ufisadi.
2. Ukiwa mwana chama wa chama cha wanywa damu (unakuwa mnywa damu)
Jamani tufike sehemu tufanye hitimisho tupige kura za maoni.
Wangapi wanamuunga mkono MWAKALINGA?
Wangapi wanamuunga mkono MWAKYEMBE?
Katika waraka(mwongozo) wa Mwakipesile kwa wanakyela, unaotumika kumnadi Mwakalinga kuna mambo ishirini yanayotajwa(waraka ambao umewekwa hapa JF na mdau mmoja) kwa ajili ya kuwaongoza wanakyela kumchagua bw.Mwakalinga.
Kusaidia kupeleka walimu wa sekondari kyela wakati akiwa anasoma chuo kikuu wakati Mwakyembe akiwa mhadhiri hakutoa msaada wowote.
Waraka aka mwongozo unasema Mwakyembe amewekeza dar, kajenga nyumba kubwa kuzidi hata mafisadi, na wewe hapa tena unarudia maneno yale yale ya mwongozo wa mwakipesile.
Katika hali kama hii utawezaje kutuaminisha kwamba bw.Mwakalinga hayuko kambi moja na mwakipesile?
unajua hata kama mwaka 2005 mwakalinga na mwakyembe walikuwa kambi moja sio suala la ajabu mwaka 2010 mwakalinga na mwakipesile kuwa kambi moja kwakuwa tayari mwakalinga hayuko pamoja na mwakyembe.
kwangu mimi hiyo siyo hoja ya msingi ya kuwafanya mwakipesile na mwakalinga wasishirikiane.
Mimi najiunga mkono mwenyewe MASANILO maana nami nitagombea huko sijaweka wazi tu!
teh teh teh na wewe unawahaidi nini wazawa huko? Je utawapelekea condomu bure?
Ukitaka msaada p'se nione
Sijaona waraka wa Mwakipesile, naomba jisaidie link yake maana sikuwepo wiki nne.
teh teh teh na wewe unawahaidi nini wazawa huko? Je utawapelekea condomu bure?
Ukitaka msaada p'se nione