Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM

Mwakalinga ni fisadi tu kama mafisadi wengine CCM.

Take that with you rafiki yangu mapinduzi.
Mwafrika,
Kama Mwakalinga ni fisadi, umeshindwaje wewe kumpeleka kisutu?
Mwakalinga ni safi ndio maana hofu na mashaka yamewajaa wanaotumia wimbo wa mafisadi maana hawana sehemu ya kumpata na kutimiza neno kutapatapa wanaamua kuimba yuko nyuma ya mafisadi ili kujikweza kiasa na kurudi kwenye tena kwenye majimbo yao wakati uwezo wa kuwaletea maendeleo wanachi hawana. Tumechoka na nyimbo za kila siku mafisadi!! Mafisadi!! kana kwamba ndio maendeleo. Watu wanalia njaa, wewe unaimba mafisadi tu mpaka siku ya kufa.
Mwakalinga siasa za majungu ya kupikwa hazitampata na atashinda tu, demokrasia itafanya kazi na hakuna mwenye hati miliki ya ubunge Tanzania.
kgwamaka
 

Eeeeh freshi kabisa. Na ukome na huo ufisadi wako
 

Mwafrika,
kwanini usiamini niliyosema mimi mpaka Mwakalinga akanushe? Any way endelea na vijembe vyako, binafsi havinipi shida na naamini hata Mwakalinga havimpi shida.

Nilifikiri tunaelemishana na kuambiana ukweli hapa, kumbe wengine mpo kuendeleza malumbano ambayo hayamsaidii mtu yeyote.
 
Kwa vile kampeni yangu itakuwa ni ya kisasa itabidi nimwajiri Yo Yo kuwa msambaza vipeperushi...

Kwi kwi kwi kwi naona ameingia mitini hana hamu tena na wewe umemnanga mno leo. Lakini ofa hiyo inamfaa sana Yo Yo ataweza.
 

Mtanzania,

Kwa nini unataka nikuamini wewe badala ya yule mwingine? Kama nyie wote (yaani wewe na yule anayetoa tuhuma dhidi ya Mwakalinga) ni second source ya information, kwa nini wewe uaminiwe zaidi ya mwenzako?

Wewe unaweza ukanipuuzia mimi na maneno yangu, ukayaita vijembe au vyovyote vile utakavyo ila nakuhakikishia kuwa hili wingu linalozunguka kampeni yenu ni kubwa sana na inabidi ulisafishe haraka sana.

Hata kama Mwakalinga akishinda Kyela (si ajabu ukichukulia vile Mwakyembe anavyopigwa vita na mafisadi - akiwemo Kikwete mwenyewe), hiyo pekee haiwasilishi picha safi kwa mbunge mpya wa Kyela hapa jamvini. Unless uamue kupuuzia kama vile Chenge, Karamagi, Lowasa na wenzio walivyoamua kupuuzia maoni ya wana JF, kuna kazi kubwa mbele yenu ya kusafisha image yenu.
 
Kwanini useme tumuachie wakati hajasema anagombea tena?

Au ubunge Kyela ni wa KICHIFU au wa KIFALME?

Kasome tena nilichoandika, nimetumia if .... then sentensi. Yaani nimetumia maneno yako mwenyewe kujenga sentensi inayokupinga. Hayo ya kuachiana yametoka kwenye maandishi yako (ulipodai kuwa Kikwete aachiwe miaka 10 ya uraisi).
 

Hao PCCB ni wakuwapuuza,hawana maana...Wanawaachia huru akina Chenge,Mrisho,Rutabanzibwa,Mgonja,Lusata,Lyana,Nyachia na Mrudi ambao wanatajwa katika kashfa za Meremeta na Tangold na kumfuatilia Mtu ambaye anatimiza haki yake ya kikatiba kwa kutaka Uongozi kwa ridhaa ya Wananchi? Huko tunakokwenda inabidi vyombo kama PCCB viangaliwe upya......kwani inaonekana kuna Tabaka la Watu waovu/Mafisadi linalindwa na vyombo hivi vya Usalama wa Umma.
 
Mtanzania;

Check aina na hoja za watu unaowapa maelezo. Hawa haitakiwi hoja ni tukutwanga tu. Mpaka kabla ya kuja wewe na kuweka hoja tulikuwa tunapambana nao na walikuwa hawafurukuti..walikuwa wanatoa VIOJA tu humu.

Hawa dawa ni kuwajibu kwa style yao tu.

Undava undava tu ndio wanataka, ukileta za kuleta unaletewa. Ukileta Hoja unahojiwa.
 
Eeeeh freshi kabisa. Na ukome na huo ufisadi wako
Pole bwana Mwakalinga. Debe tupu haliachi kutika, hata akutumie budozer, hatafua dafu, amepatikanika, maana maendeleo sio maandamano kila siku mandamano utadhani anadai uhuru.
Alimtuma hata jamaa yake Kifukwe aje London ili kukushawishi usije kugombea, lakini aligonga mwamba, hofu imewajaa hao, wanaogopa vivuli vyao.
MAENDELEO KWANZA, Udanganyifu na maandamano baadaye
kgwamaka
 


FairPlayer, vitisho tena?!

Ama kweli mmelipania hili jimbo. Swali kubwa limeanza kunikuna kichwani sasa hivi - Kwa nini Kyela? swali la nyongeza - kwa nini sasa hivi? Swali la nyongeza kwenye nyongeza - kwa nini undava?
 
Kasome tena nilichoandika, nimetumia if .... then sentensi. Yaani nimetumia maneno yako mwenyewe kujenga sentensi inayokupinga. Hayo ya kuachiana yametoka kwenye maandishi yako (ulipodai kuwa Kikwete aachiwe miaka 10 ya uraisi).

Haya mkuu. ILA PUNGUZA TAARABU KIDOGO inaonekana una akili sio kama yule wa vioja; tutashindwa kutofautisha Masanilo, Nyani na wewe.

Asante

FP
 
Haya mkuu. ILA PUNGUZA TAARABU KIDOGO inaonekana una akili sio kama yule wa vioja; tutashindwa kutofautisha Masanilo, Nyani na wewe.

Asante

FP

Tafadhali Mkuu FP usitumie jina langu kwenye mipasho....you have been warned!
 
Nyani Ngabu,

USHAURI WA BURE: Ukitaka kushinda Kyela, basi na wewe nenda Monduli na hapohapo uwe Bariadi Kiroho na kuanza kufanya kampeni. Pitia Igunga na mwaga Kisukuma kwa Rostam Azziz na hapo utakuwa umefikia nusu ya safari.

Ukifika Bariadi Mwaga LAPUTOPU Pentium 75Mhz na RAM 4mbts.

Ili kuupa ushindi wako NGUVU ya kuuwa mtu, basi ongea na Mwakalinga ili akufanyie mpango vitoto vya Kichina. Vikiwafanyia Ngosha Massage ya Kichina, itabidi kuwabebembeleza wengine wampe kidogo Chenge maana itaishia hata yeye Chenge kukupigia kura (so longer mumpitishie Kichina kimoja pale Kempinski). Na hii kazi waweza kumtumia Mange Kimambi maana pale Kempinski wanamfahamu sana.
 
Haya mkuu. ILA PUNGUZA TAARABU KIDOGO

...

FP

Okay mkuu,

Nimeacha. Unajua tena nyie "waanzilishi wa Tanzanet na JF" msije mkanifungia server yangu bure.

Mkuu Mtanzania,

Good luck na kampeni yako. Nakukumbusha kuwa utapuuzia maneno yangu na ya wana JF kwa gharama ya nafasi yako kwa siasa za Tanzania. Ukweli ni kuwa, kuna wingu kubwa sana linazunguka kampeni yako.

Natumaini utafanikiwa kulisafisha bila kutumia undava au serikali kuu na/au ya mkoa wa Mbeya.

Asante na kwaheri kwa sasa.
 
Haya mkuu. ILA PUNGUZA TAARABU KIDOGO inaonekana una akili sio kama yule wa vioja; tutashindwa kutofautisha Masanilo, Nyani na wewe.

Asante

FP

Tokea nijue kuwa unaitwa Fikiraduni sishangai unapoanza kuonyesha rangi zako za kweli.....
 

Mwafrika naombeni niachieni mie.

Kwa sasa ntatoka kidogo niende nyumba ndogo na nikirudi dawa yake itakuwa imeshachemka tayari. Kalichanganya mwenyewe sasa itabidi alinywe yeye na huyo aliyemtuma.

Solomon David na dada yangu Nyamizi (hujambo Ilumbuye) na Mtanzania ntaomba mkiona ujumbe namjibu Mwafrika, tafadhali MSISOME. Nakuheshimuni na sintataka mniweke ndugu yenu kwenye kapu la watu wa hofyo hofyo. Sintatumia matusi, ila kamstari katakuwa kembamba sana na iwe isiwe sintakavuka na kuanza kurusha matusi maana si staili yangu.

Yap. Tutaonana mida ya jioni. Ngoja nikachanje kuni mwenzenu maana Pi Mdogo leo hajisikii vizuri.
 
KUGOMBEA AU KUTOKUGOMBEA

Tulipokuwa Ngorongoro crater tukapigiwa simu na watu mbalimbali kwamba Malafyale kaandika habari ndefu kwamba Mwakalinga yuko Kyela na anaendesha kampeni na kaandika na mengine mengi. Akawaambia hayuko Kyela na badala yake yuko Ngorongoro na familia baada ya kutoka Manyara na kisha kulala Karatu jimboni Dr. Slaa.

Baadaye tukapigiwa simu na mhusika mmoja wa JF, akatusomea article yote. tukamwambia 90% ni uwongo maana mwandishi akakosea hata kijiji anakotoka. Tukawambia hiyo habari ni uwongo kwa zaidi ya asilimia 90 na waamue nini cha kufanya.

Sisi tulienda Kyela Kyela Jumapili tarehe 26/07/2009 na kuanza kukutana na wananchi siku ya Jumatatu na kuwajulisha juu ya dhamira ya Mwakalinga kugombea ubunge mwakani.

Tunashukuru wananchi ambao tulikutana nao na wengi wakashangaa kuona Mwakalinga mwenyewe kumbe ni kijana, hana umbo kubwa, na hana maringo.

Kila tulipopita hicho kitu kilikuwa kinajitokeza. Watu walitegemea kuona bonge la jitu baada ya kulisikia jina lake kwa muda mrefu, lakini wakakuta ni mtu wa kawaida kabisa.

katika utambulisho wake Mwakalinga alikuwa anazungumzia jinsi migogoro ya watu wawili inavyoathiri Kyela, elimu duni wilayani ambayo matokeo yake ni huko mbeleni Kyela kutokuwa na vijana wake wasomi kama ilivyo sasa, kilimo duni, na huduma mbovu za afya.

Pia alikuwa anaelezea jinsi Kyela wanavyoshindwa hata kumtumia mkuu wa majeshi anayetoka Kyela ili kuwahamasisha vijana kwamba wakijituma kwenye shule siku moja wanaweza kuwa kama Mwamunyange, badala yake wanampiga vita hata yeye mpaka kukwamisha baadhi ya shughuli zake pale wilayani. Akifanya jambo wanadai eti anataka kugombea ubunge. Alikuwa anawaambia wananchi kwamba kama kuna wana Kyela wanataka kuleta maendeleo nyumbani ili baadaye wagombee ubunge basi waje tu na yeye atafurahi hata wakiwa 1000.

Pia sehemu zote alikuwa anawaambia kwamba yeye sio mwanasiasa na hataki kuiga tabia za wanasiasa; kwamba yeye strength yake iko kwenye kuchapa kazi, kuwajibika na kuwaambia wananchi ukweli badala ya kuwadanganya majukwaani.

Kumbe siasa nayo ni kazi ngumu sana maana vikao vilikuwa vinaanza saa moja asubuhi mpaka saa sita usiku. Kwa siku tano tukaweza kutembelea kata 19 kati ya 21.

Hayo ndiyo ya Kyela ndugu zangu, ndiyo yamewachanganya watu, badala ya kwenda huko wilayani wakazamia JF na kueneza kila aina ya kashfa.

Nikikumbuka mengine basi nitawaandikieni.

Huko tumeambiwa ahadi za wanasiasa mwaka 2005 mpaka unaficha uso, hivi kweli ni muhimu kuongea mambo ambayo unajua kabisa huwezi kuyatekeleza?

Binafsi nimefarijika na mengi niliyoyaona Kyela, opportunities ziko nyingi ila na umaskini nao umejaa.

Nawahakikishieni mwakani 2010 Kyela kutakuwa na mpambano wa nguvu. Mwakalinga yuko focused na anajua anataka kufanya nini Kyela. Naamini mshindi Kyela itakuwa ni demokrasia kama wahusika wataamua kupambana kwa hoja.

Kyela hakuna vurugu kabisa tofauti na watu wanavyoamini huku JF au Dar. Sisi tuliambiwa eti tutazomewa na kupigwa mawe. Lakini badala yake tuliona vijana wanaotaka kuongea na kutaka kukujua zaidi. Siku ya kwanza tukakuta kijijini wameandaa ulinzi lakini tukakataa na kuwaambi hatudhani kuna watu wanataka kutudhuru. Baada ya ku access security situation na kuona ni wanasiasa wanaikuza tu, baada ya siku ya pili tuliweza kutembea kwa miguu kwenda sehemu mbalimbali pale mjini.

karibuni Kyela wakuu, hakuna vurugu kabisa. Yale ya kifo cha yule kijana yangeweza kutokea sehemu yoyote. Mimi namlaumu Mwakipesile na mkuu wa wawili kwa kushindwa kwao kusimama na kusikiliza malalamiko ya wale vijana. Wakati mwingine solutions za hii migogoro mikubwa ni kuwapa nafasi ya kutoa dukuduku zao. Hata kama walikuwa busy, bado wangeweza kupanga kukutana na wawakilishi wa hao vijana hata jioni.
 

Mwakalinmga ndio Mtanzania

2 - Profanity:
Profanity is not tolerated in the board, some words will be censored, also there is to be no name calling, doing so will give you a warning, and then a ban if you continue.

Kuna ban zaidi ya 20 zinakuja tokana na name calling katika topic hii.

Sheria hii imezingatiwa katika kufanya maamuzi haya:

Nasikitika kwa watakaoathirika na mamauzi haya.

Atakayeendelea kukiuka atapata Server ban and that will be a permanent one.
This is typical Kayanza's words.....yale yale tunawalaumu wanasiasa.....sheria hazifuatiwi kinachobakia ni tisha toto....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…