KUGOMBEA AU KUTOKUGOMBEA
Tulipokuwa Ngorongoro crater tukapigiwa simu na watu mbalimbali kwamba Malafyale kaandika habari ndefu kwamba Mwakalinga yuko Kyela na anaendesha kampeni na kaandika na mengine mengi. Akawaambia hayuko Kyela na badala yake yuko Ngorongoro na familia baada ya kutoka Manyara na kisha kulala Karatu jimboni Dr. Slaa.
Baadaye tukapigiwa simu na mhusika mmoja wa JF, akatusomea article yote. tukamwambia 90% ni uwongo maana mwandishi akakosea hata kijiji anakotoka. Tukawambia hiyo habari ni uwongo kwa zaidi ya asilimia 90 na waamue nini cha kufanya.
Sisi tulienda Kyela Kyela Jumapili tarehe 26/07/2009 na kuanza kukutana na wananchi siku ya Jumatatu na kuwajulisha juu ya dhamira ya Mwakalinga kugombea ubunge mwakani.
Tunashukuru wananchi ambao tulikutana nao na wengi wakashangaa kuona Mwakalinga mwenyewe kumbe ni kijana, hana umbo kubwa, na hana maringo.
Kila tulipopita hicho kitu kilikuwa kinajitokeza. Watu walitegemea kuona bonge la jitu baada ya kulisikia jina lake kwa muda mrefu, lakini wakakuta ni mtu wa kawaida kabisa.
katika utambulisho wake Mwakalinga alikuwa anazungumzia jinsi migogoro ya watu wawili inavyoathiri Kyela, elimu duni wilayani ambayo matokeo yake ni huko mbeleni Kyela kutokuwa na vijana wake wasomi kama ilivyo sasa, kilimo duni, na huduma mbovu za afya.
Pia alikuwa anaelezea jinsi Kyela wanavyoshindwa hata kumtumia mkuu wa majeshi anayetoka Kyela ili kuwahamasisha vijana kwamba wakijituma kwenye shule siku moja wanaweza kuwa kama Mwamunyange, badala yake wanampiga vita hata yeye mpaka kukwamisha baadhi ya shughuli zake pale wilayani. Akifanya jambo wanadai eti anataka kugombea ubunge. Alikuwa anawaambia wananchi kwamba kama kuna wana Kyela wanataka kuleta maendeleo nyumbani ili baadaye wagombee ubunge basi waje tu na yeye atafurahi hata wakiwa 1000.
Pia sehemu zote alikuwa anawaambia kwamba yeye sio mwanasiasa na hataki kuiga tabia za wanasiasa; kwamba yeye strength yake iko kwenye kuchapa kazi, kuwajibika na kuwaambia wananchi ukweli badala ya kuwadanganya majukwaani.
Kumbe siasa nayo ni kazi ngumu sana maana vikao vilikuwa vinaanza saa moja asubuhi mpaka saa sita usiku. Kwa siku tano tukaweza kutembelea kata 19 kati ya 21.
Hayo ndiyo ya Kyela ndugu zangu, ndiyo yamewachanganya watu, badala ya kwenda huko wilayani wakazamia JF na kueneza kila aina ya kashfa.
Nikikumbuka mengine basi nitawaandikieni.
Huko tumeambiwa ahadi za wanasiasa mwaka 2005 mpaka unaficha uso, hivi kweli ni muhimu kuongea mambo ambayo unajua kabisa huwezi kuyatekeleza?
Binafsi nimefarijika na mengi niliyoyaona Kyela, opportunities ziko nyingi ila na umaskini nao umejaa.
Nawahakikishieni mwakani 2010 Kyela kutakuwa na mpambano wa nguvu. Mwakalinga yuko focused na anajua anataka kufanya nini Kyela. Naamini mshindi Kyela itakuwa ni demokrasia kama wahusika wataamua kupambana kwa hoja.
Kyela hakuna vurugu kabisa tofauti na watu wanavyoamini huku JF au Dar. Sisi tuliambiwa eti tutazomewa na kupigwa mawe. Lakini badala yake tuliona vijana wanaotaka kuongea na kutaka kukujua zaidi. Siku ya kwanza tukakuta kijijini wameandaa ulinzi lakini tukakataa na kuwaambi hatudhani kuna watu wanataka kutudhuru. Baada ya ku access security situation na kuona ni wanasiasa wanaikuza tu, baada ya siku ya pili tuliweza kutembea kwa miguu kwenda sehemu mbalimbali pale mjini.
karibuni Kyela wakuu, hakuna vurugu kabisa. Yale ya kifo cha yule kijana yangeweza kutokea sehemu yoyote. Mimi namlaumu Mwakipesile na mkuu wa wawili kwa kushindwa kwao kusimama na kusikiliza malalamiko ya wale vijana. Wakati mwingine solutions za hii migogoro mikubwa ni kuwapa nafasi ya kutoa dukuduku zao. Hata kama walikuwa busy, bado wangeweza kupanga kukutana na wawakilishi wa hao vijana hata jioni.