Kwa kuongezea wasomi wengi ndiyo walioangusha taifa hili, bali ya elimu tunatakiwa tuwe na wazalendo hasa wenye nia nzuri na nchi yetu! Wakati mwingine huwa nahoji hawa wasomi wanasiasa mbona ni kama wako kwa ajili ya matumbo yao tu? Mifano unaijua sitaki kujaza thread hapaKwa mawazo yangu wanasiasa wetu wengi wako overqualified na elimu zao haziwasaidii kabisa.
Kuna watu kama Mwita Maranya, wamekaa kama vile wanaishi Mombasa, na sauti lainiiii "Sasa huyu kaka Mwakalinga, aliachia nini SUA?" Wee nani hadi akuambie? Watakaomchagua ni Wanakyela na hao ndiyo watapata jibu wakihitaji. Na sidhani wananchi wa kawaida wako interested kufahamu huyu ni Prof. wa umeme wa Upepo au Mhandisi wa Richmonduli. Wao wanaangalia mita kadhaa tu na shida yao ni mtu wa kuwasaidia kutatua maisha yao. Degree nne au tano hapa hazileti maisha mazuri kwa Wanakyela.
Tatizo ni kwamba mleta thread hii alitegemea itapatikana support ya moja kwa moja kutoka kwa members kitu ambacho imekuwa kinyume,alisahau kwamba JF ni 'Home of Great Thinkers'...Kampeni kapigeni huko Bujonde,Ikolo,Kajunjumele,Kasumulu,Ipinda,Tenende,Itungi,Mbugani,Bondeni,Ndandalo n.k na si hapa JF(though we dare to talk openly)
FIRST LADY,kaaaazi kweli kweli!
.Mkulima,
Walau umejibu kwa uwezo wako!
Sidhani kama Masters tatu zinakuwa equivalent na PhD hapa labda nipate msaada!
Kila laheri Mwakalinga
Masa
Balantanda,Balantanda,
Binafsi huwa nasoma posts zako na najua huwa unatoa hoja za maana. Sina tatizo kabisa na maandishi au hoja zako hapa JF hata kama ni kwenye mambo tunayotofautiana.
Hii thread haikuletwa na shabiki wa Mwakalinga, ililetwa na wanaompinga kwa lengo la kumpakazia. Hii imeletwa na Malafyale ambaye ni mtu wa karibu wa Dr. Mwakyembe na yuko maeneo karibu Houston. Huyu mzee hajui lolote kuhusu Kyela maana anaenda kama mtalii. Kuna articles zake nyingi kweli hapa zimejaa wrong information.
Bahati mbaya sisi hatukuwepo na hivyo kufanya habari nyingi za uwongo zisijibiwe on time.
Strategy iliyotumika ilikuwa kuleta watu wao hapa; wajifanye ni wapambe wa Mwakalinga kisha wanaendika habari za kumwangusha Mwakalinga. Ilifanikiwa mwanzoni kwasababu hakukuwa na mtu wa kukanusha.
Mwakalinga hategemei huruma yoyote toka members wa JF na in fact anaamini katika kumkoma nyani Giladi bila kumwangalia usoni. Lakini pia anaamini kwenye hoja zenye data badala ya uzushi.
Mfano ni hiyo ya Malafyale kusema Mwakalinga yuko Kyela anafanya vikao wakati ushahidi wote ukionyesha Mwakalinga wakati huo alikuwa Manyara na Ngorongoro. Au huyo jamaa anasema ametoka kumsindikiza Mwakalinga airport na kwamba alikuwa naye kwenye kampeni Kyela, kumbe ni huyo jamaa wa Yanga ambaye ndiye rafiki wa karibu kuliko wote wa Dr. Bahati nzuri tuliongea naye kwa simu na tukamdanganya kuhusu muda wa kuondoka Dar na yeye akafanya makosa yale yale ya muda. Njia ya mwongo ni fupi kweli kweli.
Nakuhakikishia kwa asilimia 100 kwamba hii thread haikuletwa hapa kumpandisha chati Mwakalinga bali kumshusha. Lakini kama ulivyosema mwenyewe kampeni si hapa JF bali ni kule Kyela na wananchi wa Kyela ndio wataamua.
Kwa kuongezea wasomi wengi ndiyo walioangusha taifa hili, bali ya elimu tunatakiwa tuwe na wazalendo hasa wenye nia nzuri na nchi yetu! Wakati mwingine huwa nahoji hawa wasomi wanasiasa mbona ni kama wako kwa ajili ya matumbo yao tu? Mifano unaijua sitaki kujaza thread hapa
Mas
George Mwakalinga mwana Kyela aliyekuwa anaishi na kufanya kazi kama mtaalaum wa kompyuta nchini UK amewasili Kyela majuzi na tayari ametangaza kuwania ubunge wa wilaya ya Kyela ndani ya CCM!
Mwakalinga ametoka kuongea na wana Kyela sasa hivi kwenye hotel ya kisasa ya Sativa na watu waliokuwepo hapo wanasema hapana shaka Mwakalinga kaletwa Kyela na vigogo ndani ya CCM na serikalini na dhahiri anaungwa mkono na mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mzee Mwakalinga na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Japhet Mwakasumi!
Kwa mujibu wa habari za watu wa Kyela,kama uchaguzi wa kura za maoni ndani ya CCM utafanyila leo kwenye kata 15 zinazounda wilaya hiyo, Mwakalinga na Dr Mwakyembe watashinda kata 6 kila mmoja na kata 3 zikiwa ni "swing states".
Kata ya Kyela mjini,kata ya Matema na kata ya Ngonga sehemu ambapo wana siasa hawa wanapotokea ndiyo kata pekee za"swing states"lkn kata ya Kyela mjini ikianza kuegemea upande wa Mwakalinga na kumpa sasa likely kama anaongoza kwa kata 7 kwa 6 za Dr Mwakyembe!
Bila ubishi kata ya Ikolo,kata ya kajunjumele,kata ya Katumba Songwe,na kata 3 za mashariki ya Kyela hizo zitachukuliwa na Dr Mwakyembe ili hali kata ya Ipinda,kata ya Lusungu,kata ya Makwale na kata 3 kuzunguka upande wa Magharibi hasa kuanzia mpakani mwa Kasumulu na mgodi wa Kiwira zitachukuliwa na Mwakalinga kwa kile wanachosema Dr Mwakyembe kashindwa kazi ya kuwasadia wahanga waliofukuzwa kazi kwenye mgodi huo na vijiji jirani!
Mwakalinga,ambae pia ana vitege uchumi vingi sana wilayani Kyela zikiwemo hotel kubwa za kisasa tayari yupo Kyela,na kaanza kuzunguka kwa kasi vijijini kujinadi kwa wana CCM na kuna kila ukweli kuwa viongozi wa CCM wilayani na mkoani wamebariki kuanza huku kwake kampeni kabla ya muda wake.
Juhudi zinafanywa ili mazungumzo ya Mwakalinga akiwa kyela ambako tayari sasa kafanya ndiyo makazi yake yapatikane na yaletwe hapa ili wana JF wayachambue!
Duh! Hatimaye Joji aka Mtanzania katinga tena ukumbini. Even Iddi Amin and Adolf Hitler had their supporters in thousands if not millions.
NYEPESI NYEPESI.
Wana ukumbi, leo nilipata kuongea na jamaa yake Mwakyembe, ndg Elias Mwanjala ambaye alikuwa mpiga kampeni mkubwa sana 2005 na alitumia pesa zake nyingi kumsaidia Mwakyembe kupata kiti hicho.
Elias anasema kuwa Mwakyembe amemfanyia mambo mabaya sana na baado anaendelea kumnyanyasa.
Anasema alipata nyumba ya National Housing Mikocheni na ndiko anakoishi, basi Mwakyembe alikwenda kumwambia Sitta ili wamnyang'anye ile nyumba.
Anasema naye Sitta akakubali azimio hilo na jamaa ameletewa notice ya kuondoka ile nyumba haraka kwa sababu hasizozijua, na alipofuatilia sana akapata habari kuwa hiyo nyumba anatakiwa kuhamia Sitta.
Anasema Mwakyembe amemwambia kuwa amesikia tetesi kuwa anamuunga mkono Mwakalinga na atamuonyesha lasivyo awaambie wapambe wake wampe kura yeye.
Elias amekimbilia Mahakamani kupinga hiyo notice ambayo haina sababu yoyote ya msingi zaidi ni uonevu tu.
Haya huyo ndiye mpinga ufisadi, haya ni zaidi ya ufisadi.
Kgwamaka
..mjadala huu uwe-confined kuhusu nani kati ya Mwakyembe na Mwakalinga, kwa kushirikiana na wana Kyela wote, yuko ktk nafasi nzuri zaidi kuchochea maendeleo na kuboresha maisha ya wana Kyela.
Dilunga said:Haya ni mawazo ya kinadharia kuliko hali halisi kisiasa. Uchaguzi haushindiki na kushindwa kwa misingi ya nani ana sifa bora zaidi pekee.
Ingekuwa hivyo labda Mwandosya na Salim Salim ndio wangekuwa marais. Lakini kwenye campaign kuna mengi. Salim Salim alipakwa matope na kambi ya Kikwete, akaonekana hafai. Mwandosya alionekana sio "kijana" na CCM stalwart kuliko Kikwete.
Tunapojadili Mwakyembe vs Mwakalinga lazima tuangalie mambo mengine ambayo yanaambatana na kampeni, campaign tactics, na pia jinsi mgombea anakavyojiuza, na kuuzwa na mwenzake, kupakwa matope etc.
Mwakyembe ni campaigner mzuri sana kwa standard za Tanzania, anaweza kuchota watu akili hata akiwa anaongea kwa matusi. Mwakalinga anaweza kuwa bora zaidi lakini Mwakyembe akamwangusha kwa sababu ya u-alwatan na sifa bandia, kambi ya Mwakalinga haiwezi kuyafungia macho haya, yanaweza kutokea. Yatatokea.
Kwi kwi kwi Mwaka 2010 Osama atakuwa Papa wa RC kule Roma, na kule Kyela Mwakalinga atakuwa Mbunge.....
Sikonge nilikuwa nakuona wa maana siku zote lakini tangu tuanze kumjadili rafiki yako Mwakalinga a.ka Mtanzania ndio nimegundua kwamba wewe ni *****.
Wanaume wa shoka mnatujua sana, mi nimezaliwa tu nikawa mwanajeshi hata depo la JWTZ sijaenda lakini nina cheo cha kanali, halafu wewe unazungumza utumbo hapa?
Najua hii inatokana na athari za wasomali na wairan mliochangamana nao huko kwenu sikonge, wameshawaharibu akili. Na sina shaka kabisa kwamba hizo mambo za kulegeza sauti ndio zenu wanaume wa kinyamwezi.
Wee Mwita,
Hilo tusi ulilonitukana kimoyomoyo ***** nasema asante sana. Sijawahi kusifiwa kwa kupewa manyotanyota mengi namna hiyo.
Nilifahamu tangu mwanzo wee kijana wa miondoko ya Mombasa. Sauti lainii na kurembua macho "sasa kaka Mwakalinga, na mimi ntapata LAPUTOPU?". Ehhh Kaza sauti basi, unaongea kama Form one ambaye hajabarehe.
Usivyo na aibu unadhihirisha kabisa wee ni Mombasa line. Haya ya eti "TUNAKUJUA SANA", ebooo, mie simo. Mie namjua mke wangu tu hapa "cheupe dawa wangu, niliyelipa mang'ombe 35".
Hoja ya mwakalinga ni nini? anataka ulaji au uwakilishi. je kyela wamekosa maendeleo kwa sababu DR.mwakyembe ameshindwa kuwawakilisha?au kwa sababu CCM imeshindwa kutekeleza ahadi zake huko kyela? kama ni kwasababu DR.mwakyembe ameshindwa kuwawakilisha ili siamini sana.manaake amekuwa mstari wa mbele na wengi wanajua hilo. Kama ccm imeshindwa Kutekeleza ilani zake basi tutakuelewa sana mwakalinga ukijiunga upinzani. Vinginevyo unatumiwa na mafisadi na kwa hivyo na muunga mkono mchangiaji hapo juu, watu wasome nyaraka za kanisa wakukemee mbali.