Samwel
JF-Expert Member
- Mar 25, 2007
- 224
- 8
Shalom,
Nilikuwa nakuona kuwa wewe ni KASUKU wa Mwakyembe. Ila kama utakuwa unachangia maneno namna hii, basi mkulu Yesu atakuwa nawe. Mie mwenyewe nilishasema wazi kabisa kuwa "au ntamsifia Mwakalinga na kama kuna sehemu kaenda kombo, basi ntamwandikia yeye moja kwa moja na hapa nikifika nikute wanamsulubu, basi ntakula bati.
Mkuu nashukuru sana kufahamu ukweli wa Mwakyembe wa upande mwingine kuwa "Mwakyembe hana msaada kwa ndugu zake". Sasa sijui JIRANI zake na watu wa mbali inakuwaje?
MWAKYEMBE KUHUTUBIA UWANJA WA MWAKANGALE LEO MCHANA.
Mbunge wa Kyela dr Harison Mwakyembe leo atahutubia wananchi wa kyela katika uwanja wa mpira wa miguu wa Mwakangale hapa mjini kyela.
Dr Mwakyembe alifika jana usiku na kulala nyumbani kwao Tukuyu na Baadaye leo ataingia mjini kyela na kuhutubia wananchi wa kyela.
Kama alivyo mheshimiwa mwakyemba,ameongozana na waandishi wa habari wa mengi.wandishi wa magazeti ya majira na Tanzania Daima.
Hivi karibuni, Dr Mwakyembe,amekuwa akiyatumia sana magazeti ya mengi katika siasa zake na ata anaposafiri ,anaongozana na wandishi wa magazeti ya mengi. Mengi ambaye anajulikana kama fisadi nyangumi na mmoja kati ya mafisadi walio saidia kuia Bank ya NBC na baado anamfadhili mtu ambaye anasema anapambana na mafisadi.
Wafuasi wa mwakyembe watasafiri hadi Usare ambako mheshimiwa huyo atapokelewa na kupewa pole na ajali iliyompata.
Moja ya vitu ambavyo,mwakyembe anategemea kuvifanya hapa wilayani ni kupita kila kata na kuchinja ng'ombe yeye na wafuasi wake na uku akisimikwa kama chifu wa kinyakyusa na kupewa pole kwa ajali.Mwakyembe anafanya hivyo ili kujaribu kuuzuia upepo mkali wa siasa unaomkabili hapa wilayani kyela.
Swali kwa wanakyela liko palepale,Je hayo ndiyo maendeleo amabayo wana kyela wanayahitaji?
Nitaendelea kuwajulisha kila kinachoendelea kutokea hapa kyela