Mheshimiwa Mtanzania aka Mwakalinga, kwanza nakushukuru kwani umejibu bila lugha ya Kejeli wala matusi. nakutakia kampeni njema, na endelea kujibu hoja hasa zile unazoona zinafaa, kumbuka ni haki ya mpiga kura kupata ukweli.
Viongozi wa leo ni wale ambao wapo tayari kujibu na kusikiliza wanayoyapenda na yale wasiyoyapenda.
Kinepi_nepi,
Tangu hii makala ianze, tumekuwa tukijibu shutuma za kumshambulia Mwakalinga ambazo nyingi hazina hata maana. Mtu anakashifu hata nchi ya Poland aliposomea na wakati huo, kiuchumi ukweli ni kuwa Poland iko mbali saaana kuzidi Tanzania, ni member wa European Union, NATO na ni moja ya nchi chache sana DUNIANI ambazo hazikuathirika sana na HOMA ya Uchumi. Hata shule aliyosomea Mwakalinga, kwa sasa iko kwenye nafasi kama ya 600 katika listi ya Vyuo 4,000 bora duniani.
Ilifika muda sasa tukaanza kutumia Newton's Law of Motions. Mtu akiuliza kistaarabu kama ulivyoandika, hata kama unarudia, tutakujibu na kukuelewesha. Ila akiuliza na kuanza kutoa kashfa kama wewe mwanzo kuwa umesoma between the line na vitu vingine, hapo tulikuwa tunamjibu sawasawa na UPUUZI wake alioulizia. "In Every reaction, there's equal and oposite reaction".Kwa hiyo hapa usitulaumu sisi ila imebidi tuwe tunajibu watu kwa namna hiyo.
Sijui kama wafahamu kuwa mtu kama Kanda2 na Mwafrika ni mtu mmoja? Kibaya zaidi ni kuwa anamfahamu sana Mwakalinga na anafahamu wazi kabisa kuwa Lowassa alikuwa Dodoma bungeni wakati Mwakalinga yuk Arusha kutalii. Ila anakuja hapa kusema kuwa Mwakalinga alikutana na Lowassa Arusha.
Hapo wanakuja sasa WATANI wa kwenye JF. Masanilo, Yo Yo, na Nyani Ngabu ambao wao kila mtu anafahamu kuwa si wa kusikilizwa sana maana utani na wao ni DUGU MOJA.
Nimekujibu hivi kukuonyesha tu kuwa "sisi ni watu na BUSARA zetu". Ila twaweza kuzitumia hizo busara katika kujadili, kusilibana, vijembe, kashfa, kuvuruga thread nk. Sijui kama utakuwa umetuelewa. I hope yes.
Tuendelee kujadiliana bila KUPAKANA matope na wala bila ya kuoneana AIBU pale mtu anapokosea. Ila Kuzuliana siyo vizuri hata kidogo.
Mungu Ibariki JF, Mungu ibariki Tanzania.