Hivi ninyi mnaompigia debe huyo Mwakalinga mmeshajiuliza AMESHAWAFANYIA NINI WAPIGA KURA WA JIMBO HILO badala ya hadithi za ATAFANYA HIKI NA KILE?
Siasa za kuangalia personality ya mtu zimechangia sana kutufikisha hapa tulipo.Badala ya kuangalia uwezo wa mtu (kwa kipimo cha aliyokwisha accomplish kwa eneo husika au taifa) watu wanaangalia sura (like ilivyokuwa kwa JK),upole,kuishi ughaibuni,idadi ya digrii (including za vyuo feki) na upuuzi mwingine kama huo.
Jiulize: Amekufanyia nini na sio untarajia atakufanyia nini.Huu sio wakati wa kucheza karata-tatu za kisiasa,we need people who are truly committed to kuangamiza ufisadi na mafisadi.Na hata kama ana mapungufu,Mwakyembe has shown a way.What about Mwakalinga?
Mlalahoi,
Mwakyembe ni SHUJAA wa Taifa. Mwakyembe ni kama Kikwete wa Tanzania. Nchi za nje anafahamika na kupendwa na kuheshimika sana ila Watanzania tunafaidika nini na huo umaarufu wake. Kutusaidia kumuweka Hasheem Thabeet kwenye NBA? Kukutana na Obama kwanza? Kusuluhisha ugmvi wa Kenya na Zimbabwe?
Watanzania wanasota na maisha kila siku iendayo kwa Mungu. akina mama wanajifungulia kwenye makorido. What a mess.
Hivyo ndivyo ilivyo kwa Kyela. Mwakyembe na umaarufu wake kitaifa, Kyela hajafanya kitu cha maana. Wapambe wake wanasema kajenga daraja wakati JWTZ wanataka kuling'oa maana ni lao na Mwakyembe anatambia kuwa ni yeye kalijenga na wala hampi asante Mwamunyange. Kagombanisha au kugombana na watu wengi tu. Hata huyo Mwanjala na kumwita Mjomba, bado kakosana na kijana wake.
Mwakalinga yeye hadi leo hii anafanya vitu vyake. Ana duka, ukumbi wa mkutano, computer centre (mtu wa IT asiwe na hii, ingelikuwa aibu), hotel na takataka nyingine ambazo hadi sasa ziko zinajengwa. Na hivi karibuni atafungua Radio FM. Radio na miradi yote anaiita KYELA na si MWAKALINGA. Hizo zote zinatoa ajira kwa watu kibao kuanzia ujenzi wake hadi watumishi wa ndani.
Mwakalinga si FISADI. Mwakalinga si mfanya biashara. Ni mfanyakazi wa kampuni la HUAWEI huko UK. Mshahara wake sehemu kubwa kila mwezi huwa unaishia Kyela. Kwa uwezo na nyenzo yake ndogo kaweza kufanya hivi vitu na ana imani akipata UBUNGE ataweza kuwa na nguvu zaidi ya kidola ya kuwasaidia Wanakyela.
Wapambe wa Mwakyembe wameyaona mafanikio hayo. Hata Mwakipesile aliyaona na matokeo yake akaanza kuipiga vita Kyela Busness centre akifikiri Mwakalinga afanya hivyo ili agombee ubunge- Mwakalinga hakugombea. Mwakyembe pia aliposhinda, pamoja na kwamba familia ya Mwakalinga walimsaidia kwenye uchaguzi, pia na yeye akaanza kuwapiga vita. Lazarusmtindi alituambia kuwa wale vijana wanne walimpiga kiongozi mwenzao walikuwa wametumwa na Mwakalinga. Ulipofanyika uchunguzi, ikabidi Mwakyembe aombe msamaha kwani ndiye alisababisha huo ugomvi.
Hii thread tangu ianze, tumekuwa tukijibu mapigo tu bila ya kushambulia mtu. Ila nakuahidi kitu kimoja, kuna siku itafika hapo mwakani, na sisi tutaanza kushambulia. Leo hii ni zamu yenu. Pakeni na msilibe saana. Ohh, jamaa fisadi, ohh hajafanya kitu, ohhh hiki ohh kile. Dawa yatokota jikoni na ukifika muda tutaipakua na kuwawekea mezani. Tutawakumbusha watu nini Mwakyembe aliahidi na nini kafanya. Na tutaangalia Mwakalinga, nini ALIWAAHIDI na nini kafanya. Hapo wana Kyela wataamua na kutenganisha Pumba na Mchele. Vinginevyo hapa tunafurahisha genge maana wengi wao humu si wapiga kura.