Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM


Mkandara,

Baada ya uchaguzi wa mwaka 2005, Mwakyembe alikuwa na uhakika wa kuwa Waziri kama asante ya kazi yake nzito aliyoifanya (tutaiandika mwakani kabla ya uchaguzi). Akawa anajiona yeye tayari ni MATAWI. Mbinu nyingi sana zilifanywa ili ashinde.
Baada ya uchaguzi kuisha, watu walimwambia Mwakyembe aende akapatane na Mwakipesile na ugomvi wa uchaguzi uishe. Kumbuka hiyo ilikuwa baada ya uchaguzi na Mwakipesile was NO BODY. Mwakyembe akarusha maneno yake ya "yeye msomi hawezi ongea na LOOSER). Juhudi zote za kuhakikisha uhasama wa uchaguzi unaisha hazikufua dafu.

Imepita miezi kadhaa, Mwakipesile kaula. Alivyorudi Mbeya, kituo chake cha kwanza kikawa Kyela. Hapo ndiyo ukawa ugomvi wao na uhasama umeanza for good maana sasa wote ni WABABE na hamuna wa kusalimu amri. Hili tulilijadili hata kule kwenye ile makala ya Mwakyembe. Je hadi leo hii kashafanya juhudi yoyote kumaliza ugomvi? SIDHANI.

Mwakalinga alipokuwa Kyela, alifika kila sehemu na kuonana na watu wa aina mbalimbali hadi wale wa Mkwakyembe kama Semfukwe, Mwanjala, nk. Alifika hadi kwenye hoteli ambayo Mwakyembe hulala. Ila nina uhakika Mwakyembe hajawahi hata kukanyaga KBS.
Mkandara, nimalize kwa kusema SUBIRA yavuta heri. Mwakani tutaandaa na kuwapasha habaro zote sitokeazo Kyela. Tutajitahidi tuweke mambo yote huko wazi na ikiwezekana Kyela FM (Radio) itakuwa inapatikana ONLINE.
Bila kujali nani mshindi, Kyela inaweka MSINGI IMARA wa Demokrasia.
 
Baada ya uchaguzi wa mwaka 2005, Mwakyembe alikuwa na uhakika wa kuwa Waziri kama asante ya kazi yake nzito aliyoifanya
Wapishi wengi huaharibu mchuzi wapi na lini Mh Dr Harrison Mwakyembe alitangaza atakuwa waziri? tupe uthibitisho...... Ama akina RA wamemwahidi Mtanzania aka Mwakalinga Uwaziri?
 

Mzee una point sana. I salute you!
 
Wapishi wengi huaharibu mchuzi wapi na lini Mh Dr Harrison Mwakyembe alitangaza atakuwa waziri? tupe uthibitisho...... Ama akina RA wamemwahidi Mtanzania aka Mwakalinga Uwaziri?


Taarabu.........

Mwaga points kama Sikonge hapo juu
 
Huwezi ziona kama umevaa miwani mida hii!you dunno kinachoendelea hapa....kindly close ur bowl.

Masanilo aka Shalom,

Watu wameshakushutia kwamba una chuki binafsi na Mwakalinga. Labda ndio unalinda ile nafasi ya jina lako kutoka kwenye report ya Richmond na pia nimesoma mahali kwamba ulitambulishwa kwa spika.

Umeulizwa mara nyingi hapa Mwakalinga kafisadi nini? kamdhulumu nani? kamwibia nani? Umeshindwa kutoa hata mfano mmoja kuonyesha Mwakalinga ni fisadi, badala yake unaimba wimbo tu kama Kasuku kakutana na Lowassa huku unajua hajawahi kukutana na Lowassa.

Sisi tunajua Mwakyembe walifungua kampuni moja na Rostam kabla ya kukorofishana. Tunajua Mwakyembe alihalalisha mauji ya Zanzibar mwaka 2001 kumbe anafukuzia ubunge wa East Africa. Tunajua aliwaficha wajumbe Tukuyu na kuwapa rushwa wakati wa uchaguzi wa 2005. Tunajua alipewa na Rostam milioni 5 kutoka EPA sawa na wagombea wengine wa CCM kwa ajili ya uchaguzi wa 2005.

Pia tunasema mazuri aliyoyafanya ikiwemo kusoma ile report ya Richmond ambayo ilikuwa na mafanikio makubwa ya yeye na kamati yake.


Kuna mengine mengi yapo ila kama alivyosema Sikonge, muda ukifika yatatolewa.
 
Last edited:

Tatizo hapa ni kwamba wewe umetumwa na mtanzania wakati mimi hata mwakyembe simjui vizuri kwa sura ila naijua kazi yake anayofanya.

Pia nakuonea huruma kwa kuwa mnapoteza muda wenu mwingi sana kutafuta Id za watu huyiu sijui ni shalom, sijui Mwanakijiji ana majina mengi humu wakati hayo hayasaidii kuonyesha kuwa mwakalinga is his own man.

Huu muda unapoteza ungeutumia kwenye vitu vya maana hata kuwa na huyu mkeo unayejuta sasa kuwamfahamu!

Mimi nakula kumi kwa kuendelea kunifananisha na masanilo kwani ni bora zaidi kuliko ungeniita mtanzania mzee wa taklima za lap top na mahotel mjini kyela.
 

Hivi yule mtoto wa Khadija Kopa aliyefariki aliyekuwa bingwa wa kuimba TAARABU alikuwa anaitwa nani vile?
 
Masanilo aka Shalom,

Watu wameshakushutia kwamba una chuki binafsi na Mwakalinga. Labda ndio unalinda ile nafasi ya jina lako kutoka kwenye report ya Richmond na pia nimesoma mahali kwamba ulitambulishwa kwa spika.

Introduction


Swali zuri na umeonyesha UKOMAVU wako kwenye kujenga hoja na sio kuimba mashairi, HONGERA. Hili hawatalijibu MILELE


FACT. Halitapingwa maana ni la kweli. Watazunguka zunguka weeeee...

Pia tunasema mazuri aliyoyafanya ikiwemo kusoma ile report ya Richmond ambayo ilikuwa na mafanikio makubwa ya yeye na kamati yake.

GOOD, UKOMAVU mwingine unathamini michango na ku recognise DR Mwakyembe alichofanya. Wao hawawezi, wataendelea kubeza tu (Taarabu)

Kuna mengine mengi yapo ila kama alivyosema Sikonge, muda ukifika yatatolewa.

Hitimisho zuri.

Sasa subiri akina Omari KOPA waje!
 
Leo Dr. Mwakyembe amesema kuongezeka kwa budget ya taifa kufikia 9.51 trillion shillings ni matokeo ya vita yake yeye dhidi ya mafisadi. Anasema huko nyuma pesa zote zilikuwa zinachotwa na mafisadi lakini sasa kwasababu amepiga sana kelele na mafisadi wameanza kuogopa ndio maana budget ya mwaka huu imeweza kuwa na fedha nyingi kuliko miaka ya nyuma.

Anasema mafisadi wametenga bilioni nne kwa ajili ya kumwangusha yeye Kyela, na bilioni nne zingine kwa ajili ya kumwangusha spika Sitta.

Pia bado anawahusisha mafisadi kwenye ajali yake.

Inaelekea kaanza kupata somo la JF; kasema Mwakipesile ni mtu mzuri na hana matatizo yoyote, wenye matatizo ni wapambe wake. Anasema yeye anafanya naye kazi vizuri kabisa. Jana alipokuwa Matema alikuwa anamshambulia Mwakipesile huyo huyo kwamba kamletea Mamluki kutoka nje ya nchi.

Mwakalinga inaelekea umemtisha sana mheshimiwa wetu, sijui kama hata usiku haweweseki na jina lako. Hataji jina lako lakini kila mwenye akili anajua anamwongelea nani. Leo alikuwa kule kwa Mwakalinga kata ya Katumba Songwe, baadaye alitembelea kata ya Ngonga.


Leo tumefanikiwa ku record hiyo hotuba yake, kama ufundi hautanigonga basi tutaweza kuwatumieni kesho maana sasa wacha nikapate Kimpumu changu.


Haya ndiyo ya Kyela yetu.
 
Mhhh,kazi ipo mwaka huu...jua ndo kwanzaa lachomoza...Yaani hapa kila mtu anakuja na lolote mradi tu ampambe bosi wake..Naomba Mungu ajitokeze mtu mwingine kabisa kugombea Ubunge wa Kyela ili kama vp hawa wote wawili wapigwe chini
 
Nafikiri hata wakati wa Campaign ukifika hapo mwakani kazi itakuwa rahisi sana....Mmeyasema mengi hapa,Yapo ya Uongo na mengine ya ukweli mkubwa,Ukumbi huu ni chanzo kizuri cha Campaign kwa Wagombea wote wawili.....Tumeijua Kyela kuanzia Ipyana mpaka Itungi Port...Tunangoja tu mwanzo wa Campaign rasmi.

Lakini na sisi watu wa JF ni lazima tujue kuwa Siasa haina Qualification ili mradi tu ufikie umri wa mtu mzima na kujua kusoma na kuandika,kuna kashfa nyingi hapa, na kuna kundi la watu wanafikiri siasa ina wenyewe....Mtanzania yeyote Mtu mzima na mwenye akili timamu ana haki ya Kikatiba kugombea uongozi wowote..ili mradi tu apate ridhaa ya anaowaomba kura.Tujifunze kuheshimiana na tuache kabisa mashambulizi binafsi kwa hawa ndugu zetu (Mwakyembe/Mwakalinga)...Tujadili nini kinatakiwa kufanyika ili kuinua hali ya maisha ya Wanakyela...Tujifunze kukubali kutofautiana.
 

Mwawado,

Mkuu umenena yote hapo juu. Tunasubiri wakati ufike na kama mungu atatupa uhai basi kazi ianze ki kweli kweli.

Binafsi naona hii thread imekuwa na manufaa makubwa, strategy ya mashambulizi iko wazi, sasa ni kuandaa majibu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…