Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,584
- 6,136
Mkuu mbona hii imekaa kinyume?...Haya si ndio ya Palestina na Israel..unataka tuamini kisichowezekana..
Ikiwa hapa kijiweni tu imefikia hivyo je ikija fikia ushindi. Sasa ya Mwakipesile aloshinda ndio mkorofi au aliyeshindwa! iweje tuone aliyeshindwa ndiye mzuri wakati uwezekano mkubwa wa uhasama hutokana na mtu aliyeshindwa! Mshindi siku zote hatafuti adui ila ushindi unaweza kukuletea maadui..na kama tujuavyo Ufahari na majitambo ya Mwakyembe ndio yamemletea maadui Lowassa ni mmoja wao. Hapa inanipa shida sana kuamini kwamba Mwakyembe ni mbaya kiasi hicho kwa jamii yetu.
Mkandara,
Baada ya uchaguzi wa mwaka 2005, Mwakyembe alikuwa na uhakika wa kuwa Waziri kama asante ya kazi yake nzito aliyoifanya (tutaiandika mwakani kabla ya uchaguzi). Akawa anajiona yeye tayari ni MATAWI. Mbinu nyingi sana zilifanywa ili ashinde.
Baada ya uchaguzi kuisha, watu walimwambia Mwakyembe aende akapatane na Mwakipesile na ugomvi wa uchaguzi uishe. Kumbuka hiyo ilikuwa baada ya uchaguzi na Mwakipesile was NO BODY. Mwakyembe akarusha maneno yake ya "yeye msomi hawezi ongea na LOOSER). Juhudi zote za kuhakikisha uhasama wa uchaguzi unaisha hazikufua dafu.
Imepita miezi kadhaa, Mwakipesile kaula. Alivyorudi Mbeya, kituo chake cha kwanza kikawa Kyela. Hapo ndiyo ukawa ugomvi wao na uhasama umeanza for good maana sasa wote ni WABABE na hamuna wa kusalimu amri. Hili tulilijadili hata kule kwenye ile makala ya Mwakyembe. Je hadi leo hii kashafanya juhudi yoyote kumaliza ugomvi? SIDHANI.
Mwakalinga alipokuwa Kyela, alifika kila sehemu na kuonana na watu wa aina mbalimbali hadi wale wa Mkwakyembe kama Semfukwe, Mwanjala, nk. Alifika hadi kwenye hoteli ambayo Mwakyembe hulala. Ila nina uhakika Mwakyembe hajawahi hata kukanyaga KBS.
Mkandara, nimalize kwa kusema SUBIRA yavuta heri. Mwakani tutaandaa na kuwapasha habaro zote sitokeazo Kyela. Tutajitahidi tuweke mambo yote huko wazi na ikiwezekana Kyela FM (Radio) itakuwa inapatikana ONLINE.
Bila kujali nani mshindi, Kyela inaweka MSINGI IMARA wa Demokrasia.