Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM

All is good, ila hii ya kugombea kupitia CCM ndio imeniacha hoi kabisa!!

Anataka kushinda ndio maana anagombea kupitia CCM...

Ila wewe public office usahau kabisa maana ile soo ya yule mdada wa Kinyiramba utalazimika kujibu tena.
 
Duu kweli Watanzania kiboko,

Kwa wale wote wanaompaka Mwakalinga, niseme kitu kimoja.

Watu wa Kyela wanafahamu mchango wake huyu jamaa tangu miaka hiyo yuko Secondary na hadi leo hii ni mfanyakazi wa kutegemewa na Wachina. (Wachina na uchapa kazi wao na akili zao, hapa wamenyoosha mikono na kumkubali jamaa).
Kaaamua arudi nyumbani kusaidia ZAIDI watu wake, MANENO KIBAOOO.

Kama una kiroho chepesi, unaweza kujibakia zako UK. GAM, makelele ya Chura yasikutishe. Muda ukifika, jitangaze kikwelikweli. Jenga WWW yako na kuweka Picha na video zako ili wenye wivu humu JF WAJINYONGE.

Kama kuna mtu anafikiri Mwakalinga anahitaji pesa ya Lowassa, basi inabidi uwahi Mirembe. Hata huyo mwandishi asiyempenda, kaandika kuwa ana kazi nzuri. Sasa kama boss wake huko anakosugua sufuria anamlipa vizuri na hadi akajenga "KIJIHOTELI", anahtaji kweli pesa za Lowassa?

GAM kama umeamua kugombea, tutakuwa tayari kukusaidia kwani tunafahamu uwezo wako. Wengine tulitegemea ufanye hivi zamani lakini ukawa ngangari. Kyela wakikukataa, njoo SIKONGE.
 
Mkamap,
Mkuu wangu Mwakeyembe alikuwa mwenyekiti wa tume waliofanya uchunguzi na kuijenga ile report sii kwamba waliletewa na Takukuru au chombo kingine.. Inawezekana sana kuwa JF tuliwasaidia sana ktk kufuatilia lakini mambo mengi hayakuwa wazi kwa wananchi na hakika report ile kama ungejua ilivyotakiwa kuzimwa usingezungumza kitu kabisa..Mwakyembe kwa ujeuri wake baada ya kukamilika tu alimpelekea mkulu jambo ambalo linapingana kabisa na report zilizotangulia na walivyotegemea wengi, hivyo huyu jamaa anajenga Uadui kwa mengi..
 

- Maneno mazito sana hayo, ubarikiwe tu mkuu na Mungu wa Mbinguni na kesho asubuhi nitafanya mazungumzo marefu sana na George kwa ajili ya tathmini na ili kumpa huu ujumbe mzito na makini sana kwa sababu na ni ukweli kwa 100%, na George anauhitaji sana especially now.

Respect.

Field Marshall Es!
 
- Una maana huyu jamaa anayepeleka wazungu wa Brooklyn Kyela, badala ya kwao Mwakaleli, ili awe mpambe wa DK, au?

Respect.

Field Marshall Es!

FMes,

Ndiyo huyo kabisaaa, yaani Mwakalinga mwingine wa JF (Na nyie Wanyakyusa watani zangu mmekuwa too much humu ndani, khaa!!!)

Pia wana ki-WWW chao cha kuvutia wawekezaji. Heri hata wangelimuomba George awafanyie ule ukurasa wao ili uwe na kichwa na miguu. Nafahamu George angelifanya hata kama kwa kusubiri kidogo.

Huwezi vutia wawekezaji kwa mistari 10. Wawezekaji wanakuwa na wanasheria wao na hao wanamuda mrefu sana wa kusoma. Ukiandika mistari 10 na bila maelezo zaidi, unaonekana tayari ni tapeli fulani. Nashangaa kama kweli anapata wawekezaji au analeta MITAPELI.
 


Hizo unazosema yawezekana kabisa si kweli.Hiyo report ya mwakyembe tayari mwanakijiji alikuwa ameshainyanyambua humu hakuna alichoongeza.Alinyonya tu humu na kupewa go ahead kwenda kuisoma hakuna alichofanya zaidi ya hicho.

Kama unahistoria nzuri kuna mzee mmoja humo bungeni ndiye miaka yote huwa analipuwa mabomu na kuwashusha mawaziri vyeo vyao toka enzi hizo kama akina Simba nk.kama hiyo ni case mbona humuiti huyo mzee kuwa ni shujaa wako.? unless ur racist.
 
Mkamap,
Mkuu iweke hiyo report ya Mwanakijiji...
Sikiliza Mwanakijiji wakati anampigia simu Lowassa ilikuwa maswala ya wanafunzi wa Urusi, ndilo lilikuwa janga kubwa la mapambano kati ya Mwanakijiji na Lowassa sio swala la Richmond.
Ila nakubali kwamba JF na hasa vijana wa Houston ndio walitushtua wengi kutuonyesha kwamba Richmond ilikuwa shirika feki na halikusajiliwa Texas tena basi watu wanaohusika wote tunawajua na wengine hawapo ktk list mzima...
Tokea hapo ndipo tulipoanza kufuatilia kwa ukaribu zaidi na hakuna kati yetu aliyejua vikao vyote vya baraza la mawaziri na kile kilichokubaliwa huko, hawa wakubwa kina Lowassa na Msabah wakazikiuka sheria hizo..
Wewe ulijua kuwa Msabah ni bangusilo kabla ya report ya Mwakyembe!..Ulifahamu maamuzi ya baraza la mawaziri na hata kuhusika kwa RA ktk deal zima kama ilivyobainika kwamba Dowans wanatumia address ya RA.. Mkuu acha hizo kama humpendi mtu sema tu, lakini nachofahamu mimi kwetu siye Wabongo msema ukweli ni mshenzi ingawa kipenzi cha Mungu.
Hapendwi mtu kwa kazi zake bali Upedejee wake..
 

MkapaP,

Kwani Mkandara ni Mzungu au Mwaarabu? May be ni Kimacho au Indian.

Kama Mkandara ni Mpingo, hawezi kuwa ni RACIST. Au huyo Mzee si MPINGO?
Naona mkuu, umekaa na Wazungu hadi ukiona UNYASI unafikiri NYOKA.
 

Mkuu
fuatilia vizuri hiyo ishu hadi kuja kuundwa hiyo kamati kila kitu kilikuwa tayari kinajulikana ,humu jf kila kitu kilikuwa kimeshaanikwa, Slaa tayari alikuwa ameshapanda jukwaani na makabrasha yote kuhusu hiyo kitu.

Alichofanya Mwakyembe ni kuisoma tu hiyo report kitu ambacho hata mtoto mdogo mwenye uwezo wa kusoma angekifanya.Nimekuuliza mbona mzee Ndakaya humuiti kuwa shujaa wako?
 
MkapaP,

Kwani Mkandara ni Mzungu au Mwaarabu? May be ni Kimacho au Indian.

Kama Mkandara ni Mpingo, hawezi kuwa ni RACIST. Au huyo Mzee si MPINGO?
Naona mkuu, umekaa na Wazungu hadi ukiona UNYASI unafikiri NYOKA.

Wee vipi Sikonge kwani nsansa umekwishaiva? Mkandara ni homeboy hata ninapopishana naye mawazo naamini ni mawazo ya kujenga kule kwetu ,maana siku hizi nansio imeporomoka sana ktk uzarishaji wa machungwa na viazi lazima tutafute njia mbadala wa tatizo letu common mie na Mkandara.

Sikonge wewe hujui waafrika tuko maracist balaa kuliko wazungu tofauti ni kwamba hatuna nyezo tu ndio maana tunaficha mbawa.
 
Mkamap,
Hapana,
Alichofanya Mwakyembe ni kuthibitisha kuwa kweli kile ambacho wengine walidhani kuwa tetesi au uzushi. The aunthetication was very important.
 

Mkuu Dilunga,

Umeongea point moja kubwa sana. Sina hakika kama info hizo zinaweza kuwa zimetoka kwa Mwakalinga mwenyewe. Kama zimetoka kwa Mwakalinga mwenyewe basi huo unaweza kuwa mwanzo mbaya, maana sioni umuhimu wowote wa hayo maelezo in relation to kugombea Ubunge.

Pili, inaonekana Bwana Mwakalinga ana wapambe wengi sana hapa ambao wanamfahamu kwa karibu na hivyo wanapokuwa wanampamba wanasema mpaka mambo yasiyo ya maana ambayo yakiandikwa magazetini yanaweza kuwa na negative impact kwake ama yanaweza kuwapa mwanya washindani wake na hivyo kummaliza kirahisi.

Kwa hiyo Mwakalinga anatakiwa kuwa-control wapambe wake maana kinachoandikwa hapa JF utakikuta kiko kwenye magazeti.

Hoja ya kuacha kazi nzuri Ulaya na kurudi Tanzania kuja kugombea Ubunge ilikuwa ni moja ya hoja zilizojadiliwa sana wakati watu wanajadili uzalendo wa Mh. Masha alipodai kwamba aliacha kazi US ili akatumikie wananchi. Kuna watu walienda mbali zaidi mpaka wakaleta hata speech ambayo Masha aliitoa kwa vijana waliokuwa wamepata scholarship za kwenda kusoma nje ya Tanzania.
 
Mkamap,
Duh mkuu wangu kweli umenishika pazuri.. Nansio tena, inauma mkuu inauma sana. Nadhani bila shaka wana Kyela wanaumia kama navyoumia mimi.. Kwa mfano huo wala sina la kusema - Mwakalinga juu!..
Hata hivyo wakuu zangu sasa tukimfagilia wote huyu jamaa yetu si kijiwe kitakosa chachu zake jamani?..
 
Wakuu bado mimi cjaipata kwa undani Cv ya huyu mwanaJF ktk masula ya siasa kama anauwezo wa kupambana na mafisadi kama jamaa wa sasa ajaribu ila kama ni kutafuta ulaji aachane na hiyo kitu.
Wakuu hata mm kama nitawahi kurudi mwakani nina mpango wa kugombea MUFINDI KASKAZINI kwa yule mzee!
Tuombeane, Mwakalinga ameanza na wengine tupo nyuma yako mwana!
 
Mkamap,
Mkuu Mwakyembe hakusoma hiyo report kama ilivyoandikwa JF hata kidogo.. mimi ninayo kumbukumbu nzuri sana ktk mambo mengi yanayotokea hapa. Kifupi ni kwamba tulijua kwa uhakika mengi ambayo yalizungumzwa lakini sii kwa kina kile.. Kisha basi kuna scandal gani ambayo haitangulia kuzungumzia hapa JF....Hivi kweli leo mtu akisimama na kuzungumza madudu ya Mkapa na Kiwira tutamhesabu kama ni msomaji tu..Hata kama report hiyo itamfikisha Mkapa mahakamani! jamani jamani hivi kweli akili yako inakwambia Lowassa amepoteza nafasi ile kwa sababu ya Dr. Slaa na Mwanakijiji!
Mkuu wangu Dr. Slaa issue yake kubwa ilikuwa EPA na Mafisadi wote kwa ujumla.. Richmond ni cha mtoto ktk hoja zote za Dr.Slaa na hakutumia muda wake mwingi kuhoji Richmond..

Na nani katika viongozi wa CCM ameweza kufanya hivyo.. scandal ya Richmond nani zaidi ya Mwakyembe ameweza kusema kwa uwazi kwamba Lowassa na viongozi wengine wote wawajibishwe! hata iwe kwa kusoma maandishi..Huyo Hosea alikana ufisadi ndani ya Richmond na hata JK mwenyewe bado hakubali Lowassa alikuwa na makosa..
Ingekuwa rahisi hivyo Mwakyembe asingechukiwa mkuu wangu, picha kati yake na Lowassa haziwivi na Lowassa atakuwa mjinga mkubwa sana kumchukia mtu ambaye alikuja soma tu taarifa..
Tena basi kwa nini mmemshika shati Mwakyembe azungumze mengine zaidi ambayo hakuyasema yangekiangusha chama ikiwa kweli tayari mnayafahamu..Leo hii hayupo bungeni watu wanapumua tena vizuri sana..Ajali wasipate wao ila wale wanatuthamini sisi na maslahi ya Taifa..Acheni jamani haki yake mpeni....
 
Mkandara ume eleweka kwa wenye uelewa mzuri hapa ndani.
 
GAM kama umeamua kugombea, tutakuwa tayari kukusaidia kwani tunafahamu uwezo wako. Wengine tulitegemea ufanye hivi zamani lakini ukawa ngangari. Kyela wakikukataa, njoo SIKONGE.

Jimbo la Sikonge mpaka dakika hii halina mtu, Nkumba ameshindwa kazi na mwakani sijui kama atapita maana God Father wake walimtema kwenye uchaguzi wa CCM mwaka juzi. Kwa hiyo nominations za CCM itakuwa kama vile wanasukuma mlevi, japo kuna dogo mmoja yuko Tume ya Mipango naona kasi yake ya kutembelea huko ni kubwa sana na bado ana usongo na Nkumba ili kulipa kisasi cha kuchezewa mchezo mchafu kwenye kura za maoni mwaka 2005.

Ukikubali kwenda kugombea basi mimi nitakuwa mpiga debe wako, utaniachia barabara ya kwenda Mibono na vijiji vyote vya huko.
 
Mwakalinga hata kama kajiandaa lakini ameshindwa kusoma nyakati.chati ya Mwakyembe bado iko juu sana Tanzania,naamini hata huko Kyela kutokana na ripoti ya richmond.Utake usitake Mwakyembe ni jasiri na shujaa na ana kubwa la kujiuza kwa wana kyela hata kama unaamini hajafanya lolote jimboni kwake.Mwakalinga kumshinda Mwakyembe ni ndoto na hivi sasa CCM walivyobadili utaratibu wa kura za matawi.Simkatishi tamaa but i bet Mwakyembe agombee kwa Chadema na Mwakalinga kwa CCM hapo hapo kyela bado Mwakyembe atashinda.
Haya kila la heri ndugu Mwakalinga katika kukivaa hicho kigogo!
 

Hivi CCM ilikuwepo wakati Watanganyika na baadae Watanzania walikpokuwa wanatolewa utumwani na pia wakati wa kujipatia uhuru?

Hivi CCM inajengwa na sera (tunazodai ni safi hata kama hatuzijui), majengo (waliyolazimishwa kuchangia watanzania na sasa yanauzwa kwa bei ya soko kwa watanzania haohao) na vikolombwezo vingine na sio wanachama wake? Je mienendo yao haihusiani na chama chao?

Hivi hili janga la ufisadi ndani ya CCM linahusu wale 'mafisadi' maarufu tu wa katika ngazi ya kitaifa ambao ni wazi CCM imekuwa na kigugumizi cha kudeal nao na sio kuanzia ngazi za mitaa, vitongoji, kata, wilaya na mikoa ambao kumejaa vigogo na vishoka watenda maovu?


Haya ni baadhi tu ya maswali ambayo hujitokeza kichwani mwangu nisikiapo kuna watu bado wanajipa moyo kuwa CCM kama chama hakina tatizo lolote kama KADA nambari wani hapa anapojaribu kueleza...

Ukada kazi......

omarilyas
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…