Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM

Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM

Jamani mtatoboana macho si tusubili 2010 nani atapita kwenye kura za maoni.
Lakini Mwakalinga si uende CHADEMA kwani lazima usimame CCM huko huko?
 
Wana kyela kuweni macho! kuna usemi mmoja aliwahi kuusema mwanasiasa mmoja hapa Bongo nanukuu "alikwina?" na mimi nauliza tena huyu Mwakalinga au Mtanzania whatever the name, alikwina? hadi leo hii ndio aibuke? hawa sasa ndio mapandikizi wa kisiasa. tuachieni Kyela yetu!
 
This is my honest opinion and I stand to be corrected. I look at politicians with 2 possible angles/spheres of influence. First - in his/her constituency and Second - nationally. Wanasiasa wa TZ wapo ambao wamelala, wengine active ktk mambo yao majimboni, na wengine mambo ya kitaifa, wengine mchanganyiko wa majimboni na mambo ya kitaifa.
Mwakyembe ametetea sana maslahi ya taifa hili, na anajitahidi hata jimboni, sasa anaetaka kumuondoa kweli atuthibitishie kuwa yeye ana nguvu zaidi ya Mwakyembe, na si vinginevyo. Sijui wenzangu mnaopenda kuingia ktk siasa nia yenu inakuwa nini hasa, je ni kupata ubunge tu au kutetea maslahi ya wananchi. Huo ndio uzalendo, sio kuweka historia kuwa ulishawahi kuwa mbunge.

JF has made me grow and understand Tanzania and Tanzanians kwa mapana na marefu

Cant stop reading and learning

MTM
 
Jamani Mtanzania yuko wapi? Anahitajika hapa atupe wasifu wa George, maana Mtanzania anazijua siasa za Kyela!
 
Ila Mods wanafurahisha mbona id ya Mtanzania inashambuliwa sana na mods kuiachia tu lakini za kwangu zote ma mods wanazinyonya kwanini?

Huyu NSESI mbona anataja sana harafu munamwachia tuu ? ama hiyo ndiyo demokrasia?
 
Jamani Mtanzania yuko wapi? Anahitajika hapa atupe wasifu wa George, maana Mtanzania anazijua siasa za Kyela!

Jamani yupo busy si mnakumbuka mtoto wa mzee wa kaya alitaka kufungua harambee ya UVCCM yakatokea matetesi kibao kuwa wanataka kufanya fujo. Yupo busy jamani mwacheni.
 
Jamani mtatoboana macho si tusubili 2010 nani atapita kwenye kura za maoni.
Lakini Mwakalinga si uende CHADEMA kwani lazima usimame CCM huko huko?
Kaka Mwakipesile kamwambia agombee kupitia CCM, na anajua itakuwa rahisi kuunganishwa kwenye network ya RA na EL,siunajua tena mambo ya IT...
 
Hujui unachoongea , mwangunga hana udini wowote ni mtu poa sana yeye ni mwislamu lakini anajichanganya sehemu yoyote ile, kanisani anaingia kwani mumewe ni mkristo na watoto wake wote ni wakristo. acha kuongea kitu usichokijua.
huko si kujichanganya bali ni UJINGA.
 
Kanda2,

Kuna watu humu ndani wanakuamini kwa kila unachokisema.

Hebu leta KAMBA nyingine ya atakachofanya Mwakalinga. Ila leta kamba moja ya OVYO kabisa yaani hata hamnazo aishtukie. Utashangaa humu watu wanavyoirukia na kuanza kusema ni kweli.

Haya, zaidi ya LAPTOP kuzigawa bure kwa Wanakyela, atafanya nini zaidi??
 
Mwakilanga huyu ni mdogo wake na huyu mkuu wa mkoa anayepambana na Mwakimbiye. Wadau hii ni vita ya mkuu wa mkoa na Mwakyembe kwa sababu Mwakyembe ndiye aliyemtoa Mwailanga RC kwenye ubunge Kyele na JK akafanya kosa kumpa ukuu wa mkoa wa Mbeya. Tangu apate ukuu wa mkoa amekuwa akimsumbua sana Mwakyembe hata amewahi kutumia vyombo vya dola kuzuia mikutano ya Mwakyembe huko Kyela. Naomba tufanye liwezekano wana JF wenye uwezo tumkate ngebe huyu kwani ubunge sii wa ukoo.
 
Hawa ndio tunaowaita Watanzania! wanawaza kiwilaya wakati chanzo cha tatizo la umasikini wa watanzania ni hao huko juu wenye kula bila kunawa. Inpofikia hatua ya mtu kuhoji eti kwa nini dereva wa Dr. Mwakyembe anaitwa Msuya ujue hapo kuna tatizo kubwa. SIKULAUMU.

Kugombea ni haki yangu, nikitaka nitakuja na sitokuwa kama nyinyi wa sitaki nataka, mara sitaki mara nataka!!!!!!!

Sisi Kyela tunaelewa Mbunge wetu ni nani na msidhani kuwa ni washamba sana wa kubabaishwa na kuishi Ulaya, wapo vijana wengi tu wa Kyela wenye kuishi Ulaya na Marekani kwa hiyo hilo sio jambo la ajabu kwetu.

Narudia huyo mtu wenu anafanya cheap pilitics na ni kwa sababu kakubali umamluki wa kina Mwakipesile.

Leo hii tunaelezwa eti huko nyuma alishirikiana na Mwakipesile akiwa Mbunge, thubutu! Wote mligwaya mkamuomba Dr. Mwakyembe aende Kyela ili aung'oe mlouita mbuyu wakati huo (Mwakipesile), leo hii mmepata uhuru mnanyanyua midomo kwamba mnaweza.

Subirini 2010 sio mbali na msije kukimbia baada ya kuukosa huo ubunge. Ushauri mdogo tu, msimdangaye jamaa kwa ajili ya kukomba vijisenti vyake anavyosotea huko Ulaya!!!!!

Kumbe Rai ilisema kweli, wapambe wanasubiri kumchuna, na watamchuna kweli akamuulize Thom Mwng'onda!!!!!!

Kumbe baado unaishi miaka ya 2000 iliyopita. Dunia ni kijiji sasa, ULAYA nani kasema? wasiwasi na hofu yako tu.
Nashukuru umejua kuwa watu wa Kyela sio washamba sasa, basi hilo litakuwa fundisho na hukumu nzuri kwa Mwakyembe kwa kuwadanganya kwa ahadi nyingi alizoshindwa kuzitekeleza, na alifanya hivyo kwa kujua wana Kyela wanatasahau, wanakumbuka sana.
Bora wa Ulaya anakula na wa kwao, kuliko wa Tanzania mchoyo.
Hakuna aliyemuomba Mwakyembe kwenda kugombea ubunge, huo ni uongo na ni namna ya kujikweza tu. Yeye tena aliwageuka wenzake ambao walipanga pamoja kuunga kwa pamoja ili wamuunge mkona dada yetu mmoja(Jina nalihifadhi)
Hata mimi napenda kuchunwa na kama unataka njoo, lakini hiyo ni hurka ya mtu na haina uhusiano na maendeleo, point ni kuwa umewafanyia nini wanaKyela uliowaahidi ahadi kibao? 2010 iko karibu na kila mtu atapata hukumu yake kulingana na kile alichotenda.
Amejenga hofu kwa sababu hakuna alichofanya, na hiyo hofu itamfikisha 2010 akiwa naaghaika na hana la kuwaeleza wana Kyela. Ubunge ni miaka 5 kikatiba na wala hakuna mbunge wa maisha, hata kichaa anaweza kuchukua fomu na kugombea. Kama alitaka kuwa wa maisha basi angefanya kazi kyela na sio maandamano kila siku hayo ndio maendeleo? Ndio tatizo la mtu kuwa mweupe.
Aangalie wenzake Tukuyu mashariki, kuko kimya, kisa maendeleo yanaonekana.
Kgwamaka
 
SteveD kafulia mbaya na waraka wake.......yaani ni ile nitoke vipi......alafu kumbe mwakalinga alikuwa kwa ma mvi kudaka mishiko? steveD lazima andike waraka mwingine.....

ha ha ha hah

Hii issue ya kupitia kwa ma mvi aka mzee wa richmonduli aka fisadi kuu la monduli itamwandama Mwakalinga hadi siku atakapoacha siasa. Alifanya makosa sana kisiasa kupitia huko.
 
- Mkulu Kanda2, na wewe ubarikiwe na Mungu wa Mbinguni strong point, katika demokrasia makini kama JF kila member hurusha maoni yake inakubalika, lakini at the end of the day huwa tunatafakari what is important kwa taifa, siasa ni mchzo mchafu sana na ninaamini kwamba Mwakalinga George, anaelewa vizuri sana hilo,

- Ninamshauri tu awe cool na makini, nimeongea naye jana na leo pia, amesharudi Dar kutoka Kyela, na ataondoka keshokutwa kurudi UK, aliwasili Dar wiki tatu zilizopita, akaenda Arusha kuona familia na kutembelea mbuga za wanyama, akaruka kwenda Zanzibar kuendelea na utalii, baadaye akarudi Dar, kabla ya kwenda Kyela, ambako alirudi Dar jana usiku.

- DK kama George, siku zote katika siasa ni lazima kuwa na maadui na marafiki, na washabiki sasa maadui wa DR, automatically wanakuwa washabiki wa George, na maadui wa George automatically wanakuwa washabiki wa DR, na maadui wa DK wanafahamika sana, sasa isiwe sababu ya kumchafua George, kama ambavyo tumekwisha sikia tayari na hizo kampeni chafu.

- Ni haki ya kila member hapa kusema anachotaka, lakini kumkashifu mpaka kumvua nguo member mwenzetu, tena kwa habari za kusaidikika it is beyond JF's civilization, maana ninaamini siku zote JF tunasimamia masilahi ya taifa, na tunaamini kwamba no one knows better kama a pure JF member, binafsi ninawaheshimu wote wawili kwa heshima sawa kabisa yaani George na DK, ninaamini wote ni vichwa na watawasaidia sana wananchi wa Kyela na mawazo yao ya maendeleo, na ninawatakia heri katika kampeni zinazokuja, tutasubiri kusikia kutoka pande zote mbili kabla ya kuamua wapi pa ku-support tena kwa 100%.

Respect.

Field Marshall Es!
Tuko pamoja mkuu wangu. nimewabana YOYO NA Mwafrika WAMEKUJA na chuki zao za kidini ili nisimpe support kamanda Mwakalinga yaani mtu anaona wivu kuona mtu wa JF kawa mbunge.
Mwakalinga Oyeeeee!!! wenye wivu wajinyonge.
 
Ila Mods wanafurahisha mbona id ya Mtanzania inashambuliwa sana na mods kuiachia tu lakini za kwangu zote ma mods wanazinyonya kwanini?

Huyu NSESI mbona anataja sana harafu munamwachia tuu ? ama hiyo ndiyo demokrasia?
Kitendo cha Mwakalinga kuitumia JF kwenye kampeni zake kinafaa kupigwa vita na wote wanaoitakia mema JF,hakina future nzuri!!!
 
Tuko pamoja mkuu wangu. nimewabana YOYO NA Mwafrika WAMEKUJA na chuki zao za kidini ili nisimpe support kamanda Mwakalinga yaani mtu anaona wivu kuona mtu wa JF kawa mbunge.
Mwakalinga Oyeeeee!!! wenye wivu wajinyonge.

Umewabana kina nani? ha ha ha haha ...

Nani ajinyonge kwa Mwakalinga kugombea? Mimi nimekupa ushauri tu kuwa wana Kyela wengi hawatakubaliana na hoja zako zilizojaa udini na chuki kwa wakristo. Huo mpango wenu wa kuibadili Tanzania kuwa Tanzanistani hautauza vizuri Kyela.

Otherwise .... wewe endelea kumshangilia Mwakalinga kadri utakavyo maana hata Lowasa alipokelewa kwa shangwe kijijini kwao.
 
Mwakilanga huyu ni mdogo wake na huyu mkuu wa mkoa anayepambana na Mwakimbiye. Wadau hii ni vita ya mkuu wa mkoa na Mwakyembe kwa sababu Mwakyembe ndiye aliyemtoa Mwailanga RC kwenye ubunge Kyele na JK akafanya kosa kumpa ukuu wa mkoa wa Mbeya. Tangu apate ukuu wa mkoa amekuwa akimsumbua sana Mwakyembe hata amewahi kutumia vyombo vya dola kuzuia mikutano ya Mwakyembe huko Kyela. Naomba tufanye liwezekano wana JF wenye uwezo tumkate ngebe huyu kwani ubunge sii wa ukoo.

Mkuu,

Hayo majina mbona umechanganya hata haijulikani unaandika nini?
 
Ila Mods wanafurahisha mbona id ya Mtanzania inashambuliwa sana na mods kuiachia tu lakini za kwangu zote ma mods wanazinyonya kwanini?

Huyu NSESI mbona anataja sana harafu munamwachia tuu ? ama hiyo ndiyo demokrasia?

Wewe nawe huchoki kulia lia hapa jamvini?
 
Mtoto wa Kikwete azua balaa kwa Mwakyembe

• Kundi la vijana lapanga kumfanyia vurugu kwenye harambee

na Moses Ng'wat, Mbeya

HARAMBEE ya kuchangisha fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), wilayani Kyela, mkoani hapa, iliyopangwa kufanyika juzi, imeshindwa kufanyika kutokana na kile kinachodaiwa kuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo, mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete, kushindwa kufika.

Habari za uhakika kutoka ndani ya umoja huo wilayani Kyela, zilidai kuwa Ridhiwani ambaye ni mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa, akiwakilisha Mkoa wa Pwani, alishindwa kufika kwenye hafla hiyo iliyopangwa kufanyika katika ukumbi wa Kyela Business Center (KDF), kwa madai ya kuwapo kwa kundi la vijana lililopanga kufanya vurugu, kwa sababu za kisiasa.

Vyanzo vyetu vya habari kutoka Kyela, vinadai kuwa kundi hilo la vijana ambalo halijulikani liko upande gani, lina hofu kuwa harambee hiyo ilikuwa na lengo la kumjenga mmoja wa vijana (jina limehifadhiwa), anayedaiwa kutaka kuwania kiti cha ubunge katika jimbo hilo ambalo kwa sasa linashikiliwa na Mbunge machachari bungeni, Dk. Harrison Mwakyembe.

Kwa mujibu wa habari hizo, Ridhiwani alitarajia kufika katika ukumbi huo majira ya saa mbili za usiku juzi, lakini licha ya vijana kuwapo kwa wingi wakimsubiri mgeni huyo rasmi, hakuweza kutokea na hakuna sababu zilizotolewa na kusababisha harambee hiyo ishindwe kufanyika.

Ilipofika majira ya saa nne usiku, minong'ono ilianza kuzagaa ndani ya ukumbi huo kwamba huenda mtoto huyo wa Rais Kikwete, alishindwa kufika kutokana na taarifa za kiusalama kwamba kuna kundi lililoandaa vurugu ili harambee hiyo isifanyike kwa hofu za kisiasa.

Baadhi ya wanachama wa UVCCM, waliozungumza na Tanzania Daima kwa sharti la kutotaja majina yao, walisema baada ya kukwama kufanyika kwa harambee hiyo, kuliibuka makundi mawili ndani ya ukumbi huo, moja likifurahia kutofika kwa Ridhiwani, likiamini kuwa limeshinda, huku jingine likihuzunika kwa kutofanyika kwa shughuli hiyo.

Hata hivyo kundi lililokerwa na kushindwa kufika kwa Ridhiwani, lilielekeza lawama zake kwa uongozi wa jumuiya hiyo kwamba haukuwa na uhakika na kitu walichokiandaa na kwamba hiyo ni ishara ya uongozi huo kushindwa kutekeleza majukumu mbalimbali ya umoja huo, ikiwamo kushindwa kuwashawishi vijana kuachana na siasa za makundi katika wilaya hiyo.

Akizungumzia hali hiyo, Mwenyekiti wa UVCCM, mkoani Mbeya, Reginald Msomba, alikiri kuwapo kwa ziara ya Ridhiwani mkoani mwake kwa ajili ya kuwa mgeni rasmi kwenye harambee hiyo ya kuchangia fedha kwa ajili ya miradi ya vijana wilayani Kyela.

Alisema yeye kama mwenyekiti wa Umoja huo, alipewa taarifa za ziara hiyo kwamba Julai 31, mwaka huu, alitakiwa ampokee mjumbe huyo wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana Taifa kutoka mkoani Pwani ili kwenda naye Kyela kwa ajili ya shughuli hiyo.

Kwa kweli jambo hilo lilikuwapo ndugu mwandishi, lakini mimi nilishangaa kutompokea mgeni huyo ambaye tulikuwa tuongozane naye hadi Kyela, lakini hadi majira ya jioni hakutokea na mimi nilipewa taarifa za kuelekea huko bila maelezo mengine," alisema Msomba bila kufafanua alikokuwa akipata maelekezo hayo.

Alipotakiwa kueleza sababu za kuahilishwa ghafla kwa ziara hiyo wilayani Kyela, alisema yeye hawezi kulizungumzia hilo kwa kuwa liko nje ya uwezo wake, na kuongeza kwamba watu waliopaswa kulizungumzia ni viongozi wa umoja huo Wilaya ya Kyela.

Juhudi za kumpata Mwenyekiti wa UVCCM Kyela, Hanta Mwakifuna, kwa njia ya simu kutoka Kyela zilifanikiwa, lakini hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo, hususan sababu za kushindwa kufika kwa mgeni rasmi Ridhiwani Kikwete.

Mimi sidhani kama kuna haja ya suala hili kupelekwa kwenye vyombo vya habari, kwa kuwa hata utaratibu wa kumualika hatukuufanya kupitia vyombo vya habari, naomba unielewe kuwa shughuli haikufanyika na sasa tunaangalia jinsi ya kuandaa upya, sihitaji kukuambia kama alifika au hakufika," alisema.

Alipotakiwa kuelezea iwapo kushindwa kufika kwa Ridhiwani kumekwamisha malengo ya umoja huo wilayani Kyela, mwenyekiti huyo alisema lengo lao halikutimia, na kusisitiza kuwa wanajipanga upya kumwita kwa ajili ya harambee hiyo.

Kuhusu tetesi za kuwapo kwa kundi lililopanga kumfanyia vurugu mgeni huyo kwa sababu za kisiasa, Mwakifuna alikanusha taarifa hizo, kwa madai kuwa si sahihi.

Alisema hafikiri kama kuna vijana waliochochewa kufanya vurugu, kwa kuwa kazi hiyo ililenga kufanikisha uchumi wa miradi ya vijana wa chama hicho.
Taarifa hizo ni za kisiasa tu na hazihusiki kwa namna yoyote na kutofika kwa Ridhiwani," alisema bila kutaja sababu nyingine iliyomfanya Ridhiwani kutofika kwenye harambee hiyo.

Alisisitiza kuwa harambee hiyo itafanyika katika tarehe itakayopangwa upya. Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, UVCCM wilayani Kyela katika harambee hiyo walitarajia kukusanya zaidi ya sh milioni 155, ambapo hadi kufikia juzi, walikuwa wamekusanya sh milioni 21.9, zilizochangwa na watu mbalimbali, wakiwamo vijana wa umoja huo kutoka kata zote 21 za wilaya hiyo.

Ah sasa nimeamini kuwa huyu Mwakalinga anatumiwa na mafisadi. Yaani hadi mtoto wa Kikwete alikuwa aje kumpigia kampeni? No wonder Kanda2 yuko kwenye kampeni timu ya Mwakalinga hapa JF. Yale yale ya kuigeuza Tanzania iwe Tanzanistani.
 
[QUOTE=Kyala Gwamaka ,Kumbe baado unaishi miaka ya 2000 iliyopita. Dunia ni kijiji sasa, ULAYA nani kasema?

Mwakalinga a.k.a Mtanzania kasema sifa yake kubwa ni kukaa Ulaya muda mrefu.

Bora wa Ulaya anakula na wa kwao, kuliko wa Tanzania mchoyo.

Duh...kumbe ni njaa tu ndiyo inayokusumbua mnyakyusa mwenzangu,tungebishana sana kume sababu yenyewe ni hii.

Yeye tena aliwageuka wenzake ambao walipanga pamoja kuunga kwa pamoja ili wamuunge mkona dada yetu mmoja(Jina nalihifadhi)

Hakika unamawazo tegemezi sana,mnasubiri kubebwa tu,kwanini huyo dada asingegombea mwenyewe mpaka asubiri Dr ambebe?inaonyeshwa huo ushirika wenu mtakatifu hauna nguvu na ndio maana mnakuwa mnalilialilia fadhira,kama alivyoshinda 2005 bila ushirika wenu ndivyo itakavyotokea 2010.

point ni kuwa umewafanyia nini wanaKyela uliowaahidi ahadi kibao? 2010 iko karibu na kila mtu atapata hukumu yake kulingana na kile alichotenda.

Hahiitaji kuwa na akili saaana kujua kuwa Mwakyembe katimiza wajibu wake vizuri kama Mbunge makini,wenye mawazo ya kimatonya shauri yenu.....

Ndio tatizo la mtu kuwa mweupe.

Ni jukumu la Wanakyela kujudge kati ya Mwakyembe na Mwakalinga/Mwakipesile nani mweupe.

Aangalie wenzake Tukuyu mashariki, kuko kimya,

Nani kakuambia Rungwe Mashariki kuko kimya?fuatilia tena source zako..

Kwa wapambe wa mtindo wa Gwamaka,kaaazi kwelikweli......
 
Back
Top Bottom