Mwongozo wa Mkuu wa Mkoa wa uendeshaji kampeni ya Mwakalinga, ambao kila mpambe wa Mwakipesile anao na sisi akina yakhe tunao, ni huu hapa:
"1. George ameanza kusaidia Kyela tokea alipokuwa mlimani kama mwanafunzi, wakati hakuwa na uwezo kabisa. Yeye na wenzake waliungana pamoja kuchangia walimu wanafunzi ili waje wafundishe shule za secondary Kyela wakati wa likizo. Wakati huo Mwakyembe alikuwa mlimani, alikuwa hana msaada, hata mikutano alikuwa hahudhurii na alikuwa anajulikana kama anatoka Rungwe.
2. Toka George aanze kazi kila mwaka hutumia mshahara wa mwezi mmoja kusaidia jamii mbalimbali Kyela zikiwemo shule, wanafunzi ambao wamekwama na matatizo mengine kama vile kuwasaidia walimu kudai mafao yao pamoja na wafiwa kufuatilia malipo ya waume zao wanao waliofariki.
3. Mpaka sasa George kishasaidia karibu kila kata na anaendelea kusaidia kadri mungu anavyompa uwezo.
4. George anapinga ugomvi na migawanyiko ya watu na anataka kuisaidia Kyela ili iweze kupiga hatua mbele kwenye maendeleo kuliko hata wilaya kama Rungwe ambayo haina utajiri kama Kyela. Baada ya uchaguzi anataka kuonana na watu wa makundi yote na kuwakutanisha pamoja kwa faida ya Kyela.
5. George amesoma, ametembea dunia, anajuana na watu wengi ambao watakuwa muhimu sana huko mbeleni wakati akitekeleza mipango yake ya kuiendeleza Kyela. Kwa mfano Kyela radio FM imetolewa na UN kupitia shirika la elimu, sayansi na utamaduni. Na sasa yuko mbioni kuanzisha tawi la Open University Kyela ili kila mwana Kyela anayetaka aweze kusoma mpaka uwezo wake utakapoishia.
6. Huko nyuma alipoona wana Kyela wanahangaika kwenye mikopo aliweza kuwashawishi PRIDE kutoka Tukuyu ili waje Kyela. Na mpaka leo PRIDE wanashukuru maana wamegundua soko la Kyela ni kubwa. Tunaamini wana Kyela wengi wamefaidika.Mpango wa baadaye ni kuungana na wana Kyela wengine kufungua bank ya wana Kyela ili wananchi waweze kujipatia mikopo na ushauri wa uhakika kwa faida yao .
7. George Ulaya ana kazi ya maana sana na ambayo kipato chake ni zaidi ya mara mbili ya ubunge.familia ilikuwa inataka aendelee kukaa huko na kuachana na siasa za majungu huku nyumbani. Lakini George ameamua kurudi baada ya usanii wa Mheshimiwa na amekubali pato lake litashuka sana lakini yuko tayari kuwatumikia wana Kyela kwa moyo wote kama ambavyo ameweza kuitumikia familia yake kwa muda mfupi na mpaka kufanikiwa kufungua kampuni kama KBC kwa kutumia pesa zake kwa miaka 10 tu ambayo amekuwa kazini.
8. George anataka kuzibadili shule na hospitali hasa ya Kyela ili ziwe za kisasa, kununua na kuomba vifaa kama magari ya wagonjwa na mashine za kutibia kutoka sehemu mbalimbali. Pia kuleta watu wa kujitolea kutoka nje kusaidia shule na hospitali ili ziwe na ubora na kupunguza vifo vya watoto na wanawake kama ilivyo sasa. George anataka kukomesha mambo ya kwenda Igogwe na Tukuyu kutibiwa, badala yake hospitali zetu zitakuwa bora hata zaidi.
9. George hataki ukubwa na muda wote anaishi maisha ya kawaida. Hahitaji
Shangingi na pesa za shangingi akipata anataka zitumike kununua magari ya wagonjwa kwa faidi ya jamii yote.
10.George amesaidia kuwaamsha vijana wa Kyela kwa kuwaletea ukumbi wa kisasa, kuona mipira kwenye TV kubwa na mpaka sasa vijana wa Kyela hawababaishwi tena na vijana wengine toka Dar. Huko mbele anataka kuimarisha huduma zingine mbalimbali kwa faida ya Kyela.
11. Kupitia KBC vijana wote wamekuwa wakipata vibarua KBC na kupata mahitaji yao muhimu. Lengo huko mbele ni kuimarisha ajira kwa vijana. Kwamba huko mbele anataka kusimamia mafunzo ya VETA na kuwapa vijana misaada ili wakajiajiri mijini, kuwasaidia vijana wanaotaka kujiunga na jeshi. Atakuwa wa kwamza kwenda kumpigia magoti Mwamunyange ili vijana zaidi waende jeshini, pia atasaidia vijana kujiunga na jeshi la polisi.
12.George anataka kurudi kwasababu ana uchungu na Kyela, anataka kusaidia Kyela akiwa bado kijana na nguvu zake badala ya kurudi uzeeni. Anataka wote waliosoma na kubaki Dar wawe na uhusiano na nyumbani, wajenge nyumbani, wasaidie nyumbani, matokeo yake vijana watapata kazi huku nyumbani. Waambie George anataka kuwasiliana na kila mwana Kyela ili kuwashawishi wafanye kitu chochote nyumbani ikiwemo kuwasaidia wazazi wao na wadogo zao.
13. Mheshimiwa hana uchungu na Kyela na alikuja Kyela baada ya kuwaogopa wale maprofesa kule Rungwe. Ndio maana muda wote anashinda Tukuyu.
14. Mheshimiwa anapoteza muda na Wachaga ambao wameendelea zamani huku kwake hakuna kitu, vijana wanahangaika bila ajira. Kwamba yeye Mwakyembe anachotaka ni uwaziri ndio maana kila sehemu anazunguka na waandishi wa habari ili wakuze jina lake.
15. Hata vita vya ufisadi na Richmond , data nyingi alipewa na akina George kutoka kwenye mitandao yao . mitandao ndio iliibua Richmond . Mwanzoni bunge walipuuza lakini watu wa mitandao wakazidisha nguvu na kutoa scandal zao mpaka bunge lilipokubali kuchunguza. Waambie George ni mdau mzuri kwenye mitandao ya Watanzania inayopinga ufisadi na viongozi wabaovu.
16. Mheshimiwa amekuwa mbunge miaka 9. ikiwa ni pamoja na bunge la East Afrika lakini hakuna alichofanya Kyela na badala yake kajenga jumba kubwa Dar ambali ni la anasa kuliko majumba ya mafisadi. Kwamba hata nyumba ya kwao Ikolo yeye hakai, ile alijenga ili tu kuwadanganya wana Kyela kwamba anatoka Kyela.
17. Mheshimiwa anakosana na kila mtu, hata George hakutaka kugombea sasa lakini Mheshimiwa anatumia ubunge wake kuikwamisha hata KBC. Alitumia akina Kifukwe kukwamisha CRDB kufungua branch KBC, alijaribu kuzuia radio isije Kyela na anapinga vijana wanaotaka kuendeleza Kyela.
18. Badala ya kuwapelekea wananchi maendeleo yeye anapeleka disco ili wacheze na kuambukizana ukimwi zaidi.
19. Anapenda makuu, daraja lililojengwa na jeshi tayari analiita daraja la kwake. Nyerere aliongoza miaka yote bila hata nyumba moja kuitwa jina lake. Angalau hilo daraja angeita daraja la Mwamunyanga.George hataki kabisa kutukuza jina lake na badala yake anatukuza Kyela, ndio maana kwenye kila kitu ameweka Kyela badala ya jina lake.
20. Mheshimiwa ameshindwa hata kushughulikia suala la maji na mabomba ya Wascandinavia badala ya kushughulikia ili yatoke maji, yeye ameyaacha na anashinda Dar, hajui hata Kyela kuna tatizo gani. Wapambe zake kazi kupeleka umbea tu."