Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM

Kyela 2010: Mwakyembe Vs Mwakalinga kupitia CCM

Hahahaaa Mnigeria alikukunja shati akakunyenyua juu hadi ukawa unasimamia vidole utadhani Michael Jackson anacheza wimbo wa Thriller.

Nikaona Mkuu macho yamekutoka kaa mjusi kabanwa na Mlango. Ilibidi Ngosha nitumie ubabe wangu kukuokoa na Kipigo cha Mbobo huyu.

Next time you must be careful na vya watu. Anza kujitegemea na usikalie visenti vya Mwakyembe, maana utakufa masikini, Mwafika weee!!!!

*** Baada ya muda, simu inaingia*****

.... harooo sukaka (nick name ya morani1)..

mpiga simu -- wewe sukaka nipe waziri mkuu
morani1 -- wasiri mkuu hayupo nani mwensangu?
mpiga simu -- Mwakipesile hapa kwani umenisahau
Morani1 -- Samahani msee, ........ gghahggjfhgjhhhhaggffffggg

----baada ya kimya na kelele zisizoeleweka--

Morani1 (kwa mbali) -- fureghiii fureghiiiiii fureghiiii msee yuko wapi

----- sauti kwa mbali zisizoeleweka.

Lowasa - waziri mkuu hapa na raisi mtarajiwa wa Tanzania.

*** itaendelea****
 
Nakushukuru Mkuu. Huyu Kapela nahisi namfahamu pamoja na kutumia jina tofauti,ni wale wasanii wa kisiasa wilayani Kyela ambao hawana msimamo kabisa. Akija Mwakyembe wapo, Mwakalinga wapo! Wao wanajali fedha tu! Undumila kuwili ni ajira!

Kwa kuwa amenitukana na hajaanza leo huyu jamaa, basi mimi sasa namwaga analysis yangu ya kweli kuhusu huyu "Mbunge Mtarajiwa", potelea mbali. Nataka nimwonyeshe kuwa anayoyajua na mimi nayajua!
Mwakalinga ameweza kupita Kata zote za Kyela kupima upepo. Kwa ujumla upepo si mzuri sana kinyume cha matarajio. Tutake tusitake bado wananchi hawajamkinai Mbunge wao. Aidha, viatu vya Mwakyembe ni vikubwa mno kwa Mwakalinga ambaye ana tabia tofauti kabisa na mpinzani wake: si mcheshi, si mvumilivu wa mawazo tofauti, hana uzoefu wa kisiasa (anaamini mno watu. Anaamini hata matapeli wa kisiasa akina Kapela alimradi wamemsifia), hana upeo wa kutosha wa elimu kufanya tathmini halisia na kusoma alama za nyakati na, kwa kifupi, ana papara.
Alipofika tu, kosa kubwa alilofanya ni kumhakikishia kila mtu aliyekuwa karibu yake kuwa anaungwa mkono na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mwakipesile pamoja na wapambe wake wakubwa: Nawab Mulla, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa na Cornel Apson Mwang’onda, aliyekuwa Mkuu wa Usalama wa Taifa. Alidhani kwa kufanya hivyo, atakubalika zaidi!
Amefanya vikao kadhaa na wazee hao ambao kabla ya kuja kwake walikwenda mbio sana kuwatangazia wananchi wa Kyela kuwa “Mkombozi wa Kyela Anakuja”! Ilibidi Mwakipesile azue ziara ya kiserikali ya “uongo na kweli” wilayani Kyela mwezi uliopita ili kumsafishia njia George Ambwene Mwakalinga kwa kukutana na madiwani wote wanaomsikiliza, wenyeviti na makatibu wa CCM wa Kata na viongozi wa UVCCM, UWT na WAZAZI wilaya ya Kyela.
Wote mnajua kuwa ziara ya Mwakipesile ikachafuliwa na vurugu za Kyela ambazo kwa kiasi kikubwa zilisababishwa na Polisi na yeye mwenyewe kuendekeza sana visasi hadi kuwajibu vibaya wananchi waliokuwa na hasira. “Leo ndiyo mnanijua; nendeni kwa huyo Mbunge wenu mkamlalamikie!”
Kundi la Mwakipesile liko kazini siku nyingi, kumsifia Mwakalinga na kumponda Mwakyembe. Linapewa posho nzuri sana. Kampeni hii inaendelea Kyela, Mbeya na Dar es Salaam. Kyela inaongozwa na jamaa mmoja wanamwita Makete; Dar es Salaam na jamaa anayeitwa Mwanjala na Mbeya na Mkuu wa Mkoa mwenyewe. Wote tulikutana Kyela alipokuja Mwakalinga! Kama si kweli, basi Kapela abishe!
Katika kampeni hii kila kundi linaongozwa na “mwongozo maalum” ulioandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambao una hoja 20. Vilevile si siri, Kapela anajua, fedha inatoka kwa Rostam kupitia kwa RC. Ndiyo maana kundi la washikaji ni kubwa. Wengi wao hawamtaki Mwakalinga, kwa sababu hawamjui vizuri, ila wanaitaka pesa yake!
Baada ya muda si mrefu nitawatumia mwongozo huo wa Mkuu wa Mkoa ambao Mwakalinga anaufuata kama biblia, kitu ambacho ni kosa kubwa!

1. Wananchi bado hawajamkinai Mwakyembe, sasa woga wa nini?

2. Hata kama anaamini sana watu na kutapeliwa, wee inakuuma nini? Mwisho si pesa za Rostam Aziz na Lowassa au tuseme pia kuwa ni zao.

3. Upeo wa elimu yake uko chini? Je Wa Mwakyembe uko juu? Juzi anasema wananchi wa Mara waishitaki Barick Gold badala ya kwenda kuwasaidia waishitaki BG? Sasa elimu yake anaitumiaje? Kuanzisha umeme wa UPEPO Sindida na Rostam Azziz? Kama unabisha muulize Dr. Slaa.

4. Mwakipesile aliondolewa ubunge kwa msaada mkubwa sana wa Mwakalinga. Mwakipesile pia aliipiga vita KBS. Leo hii eti kawa mtetezi? I can sence the missing link somewhere.

5. Wazee walikwenda mbio sana, speed gani hiyo? Duu, hao wazee waenda mbio nataka niwaone na mbio zao za sanaaa....

6. Kwa hiyo huo mwongozo umetoka kwa RC, wee umeupitia na kuu-PIMP aka tunning na kutupakulia hapa. Sasa kama umeandikwa na RC, inamhusu nini Mwakalinga? Aliyekuwa anamtumia TAKURURU ninani? Mbona hiyo hujaiandika hapa? Haya, kesho Mwakalinga tunaye hapa na mtu mzima utaaibika. Watu kama nyie ni kuwabana kwa point tu.

Mwisho ni kuwa kama wewe ni kweli ulikuwa kambi ya Mwakalinga, usingelikuja kumpaka hapa namna hiyo. Kama ungelikuwa na lako jambo basi ungelisema hukohuko na haswa mbele yake. Watu wanaokuja kuandika hapa kwa kutumia majina FEKI na huku ulikuwa na mtu hapo Mbeya siku zote kwangu mie huwa nawaona ni ma-FISI fulani hivi. Ni tabia za wanaume wa Mombasa au maneno ya akina mama huko nyuma ya nyumba. Wee Mwanaume mzima unamuogopa mwanaume mwenzio, tena unasema jamaa anaamini sana watu. Si ungelimwambia basi na wewe maoni yako na si kuja hapa kubwabwaja na unategemea watu wenye akili zetu tukuamini? Watakuamini adui zake Mwakalinga na rafiki zake Mwakyembe. Next time ukumbuke wimbo huu hapa chini:

[ame="http://www.youtube.com/watch?v=d6FwaKlKlb0"]YouTube - Broadcast Yourself.[/ame]
 
Mtoto wa Kikwete azua balaa kwa Mwakyembe

• Kundi la vijana lapanga kumfanyia vurugu kwenye harambee

na Moses Ng'wat, Mbeya

HARAMBEE ya kuchangisha fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), wilayani Kyela, mkoani hapa, iliyopangwa kufanyika juzi, imeshindwa kufanyika kutokana na kile kinachodaiwa kuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo, mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete, kushindwa kufika.

Habari za uhakika kutoka ndani ya umoja huo wilayani Kyela, zilidai kuwa Ridhiwani ambaye ni mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa, akiwakilisha Mkoa wa Pwani, alishindwa kufika kwenye hafla hiyo iliyopangwa kufanyika katika ukumbi wa Kyela Business Center (KDF), kwa madai ya kuwapo kwa kundi la vijana lililopanga kufanya vurugu, kwa sababu za kisiasa.

Vyanzo vyetu vya habari kutoka Kyela, vinadai kuwa kundi hilo la vijana ambalo halijulikani liko upande gani, lina hofu kuwa harambee hiyo ilikuwa na lengo la kumjenga mmoja wa vijana (jina limehifadhiwa), anayedaiwa kutaka kuwania kiti cha ubunge katika jimbo hilo ambalo kwa sasa linashikiliwa na Mbunge machachari bungeni, Dk. Harrison Mwakyembe.

Kwa mujibu wa habari hizo, Ridhiwani alitarajia kufika katika ukumbi huo majira ya saa mbili za usiku juzi, lakini licha ya vijana kuwapo kwa wingi wakimsubiri mgeni huyo rasmi, hakuweza kutokea na hakuna sababu zilizotolewa na kusababisha harambee hiyo ishindwe kufanyika.

Ilipofika majira ya saa nne usiku, minong'ono ilianza kuzagaa ndani ya ukumbi huo kwamba huenda mtoto huyo wa Rais Kikwete, alishindwa kufika kutokana na taarifa za kiusalama kwamba kuna kundi lililoandaa vurugu ili harambee hiyo isifanyike kwa hofu za kisiasa.

Baadhi ya wanachama wa UVCCM, waliozungumza na Tanzania Daima kwa sharti la kutotaja majina yao, walisema baada ya kukwama kufanyika kwa harambee hiyo, kuliibuka makundi mawili ndani ya ukumbi huo, moja likifurahia kutofika kwa Ridhiwani, likiamini kuwa limeshinda, huku jingine likihuzunika kwa kutofanyika kwa shughuli hiyo.

Hata hivyo kundi lililokerwa na kushindwa kufika kwa Ridhiwani, lilielekeza lawama zake kwa uongozi wa jumuiya hiyo kwamba haukuwa na uhakika na kitu walichokiandaa na kwamba hiyo ni ishara ya uongozi huo kushindwa kutekeleza majukumu mbalimbali ya umoja huo, ikiwamo kushindwa kuwashawishi vijana kuachana na siasa za makundi katika wilaya hiyo.

Akizungumzia hali hiyo, Mwenyekiti wa UVCCM, mkoani Mbeya, Reginald Msomba, alikiri kuwapo kwa ziara ya Ridhiwani mkoani mwake kwa ajili ya kuwa mgeni rasmi kwenye harambee hiyo ya kuchangia fedha kwa ajili ya miradi ya vijana wilayani Kyela.

Alisema yeye kama mwenyekiti wa Umoja huo, alipewa taarifa za ziara hiyo kwamba Julai 31, mwaka huu, alitakiwa ampokee mjumbe huyo wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana Taifa kutoka mkoani Pwani ili kwenda naye Kyela kwa ajili ya shughuli hiyo.

Kwa kweli jambo hilo lilikuwapo ndugu mwandishi, lakini mimi nilishangaa kutompokea mgeni huyo ambaye tulikuwa tuongozane naye hadi Kyela, lakini hadi majira ya jioni hakutokea na mimi nilipewa taarifa za kuelekea huko bila maelezo mengine," alisema Msomba bila kufafanua alikokuwa akipata maelekezo hayo.

Alipotakiwa kueleza sababu za kuahilishwa ghafla kwa ziara hiyo wilayani Kyela, alisema yeye hawezi kulizungumzia hilo kwa kuwa liko nje ya uwezo wake, na kuongeza kwamba watu waliopaswa kulizungumzia ni viongozi wa umoja huo Wilaya ya Kyela.

Juhudi za kumpata Mwenyekiti wa UVCCM Kyela, Hanta Mwakifuna, kwa njia ya simu kutoka Kyela zilifanikiwa, lakini hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo, hususan sababu za kushindwa kufika kwa mgeni rasmi Ridhiwani Kikwete.

Mimi sidhani kama kuna haja ya suala hili kupelekwa kwenye vyombo vya habari, kwa kuwa hata utaratibu wa kumualika hatukuufanya kupitia vyombo vya habari, naomba unielewe kuwa shughuli haikufanyika na sasa tunaangalia jinsi ya kuandaa upya, sihitaji kukuambia kama alifika au hakufika," alisema.

Alipotakiwa kuelezea iwapo kushindwa kufika kwa Ridhiwani kumekwamisha malengo ya umoja huo wilayani Kyela, mwenyekiti huyo alisema lengo lao halikutimia, na kusisitiza kuwa wanajipanga upya kumwita kwa ajili ya harambee hiyo.

Kuhusu tetesi za kuwapo kwa kundi lililopanga kumfanyia vurugu mgeni huyo kwa sababu za kisiasa, Mwakifuna alikanusha taarifa hizo, kwa madai kuwa si sahihi.

Alisema hafikiri kama kuna vijana waliochochewa kufanya vurugu, kwa kuwa kazi hiyo ililenga kufanikisha uchumi wa miradi ya vijana wa chama hicho.
Taarifa hizo ni za kisiasa tu na hazihusiki kwa namna yoyote na kutofika kwa Ridhiwani," alisema bila kutaja sababu nyingine iliyomfanya Ridhiwani kutofika kwenye harambee hiyo.

Alisisitiza kuwa harambee hiyo itafanyika katika tarehe itakayopangwa upya. Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, UVCCM wilayani Kyela katika harambee hiyo walitarajia kukusanya zaidi ya sh milioni 155, ambapo hadi kufikia juzi, walikuwa wamekusanya sh milioni 21.9, zilizochangwa na watu mbalimbali, wakiwamo vijana wa umoja huo kutoka kata zote 21 za wilaya hiyo.


Huyu Ridhiwani itabidi atafute kazi nyingine ya kufanya na sio Kyela kupigia kampeni mafisadi wenzake.
 
Mwongozo wa Mkuu wa Mkoa wa uendeshaji kampeni ya Mwakalinga, ambao kila mpambe wa Mwakipesile anao na sisi akina yakhe tunao, ni huu hapa:

"1. George ameanza kusaidia Kyela tokea alipokuwa mlimani kama mwanafunzi, wakati hakuwa na uwezo kabisa. Yeye na wenzake waliungana pamoja kuchangia walimu wanafunzi ili waje wafundishe shule za secondary Kyela wakati wa likizo. Wakati huo Mwakyembe alikuwa mlimani, alikuwa hana msaada, hata mikutano alikuwa hahudhurii na alikuwa anajulikana kama anatoka Rungwe.


2. Toka George aanze kazi kila mwaka hutumia mshahara wa mwezi mmoja kusaidia jamii mbalimbali Kyela zikiwemo shule, wanafunzi ambao wamekwama na matatizo mengine kama vile kuwasaidia walimu kudai mafao yao pamoja na wafiwa kufuatilia malipo ya waume zao wanao waliofariki.

3. Mpaka sasa George kishasaidia karibu kila kata na anaendelea kusaidia kadri mungu anavyompa uwezo.

4. George anapinga ugomvi na migawanyiko ya watu na anataka kuisaidia Kyela ili iweze kupiga hatua mbele kwenye maendeleo kuliko hata wilaya kama Rungwe ambayo haina utajiri kama Kyela. Baada ya uchaguzi anataka kuonana na watu wa makundi yote na kuwakutanisha pamoja kwa faida ya Kyela.

5. George amesoma, ametembea dunia, anajuana na watu wengi ambao watakuwa muhimu sana huko mbeleni wakati akitekeleza mipango yake ya kuiendeleza Kyela. Kwa mfano Kyela radio FM imetolewa na UN kupitia shirika la elimu, sayansi na utamaduni. Na sasa yuko mbioni kuanzisha tawi la Open University Kyela ili kila mwana Kyela anayetaka aweze kusoma mpaka uwezo wake utakapoishia.

6. Huko nyuma alipoona wana Kyela wanahangaika kwenye mikopo aliweza kuwashawishi PRIDE kutoka Tukuyu ili waje Kyela. Na mpaka leo PRIDE wanashukuru maana wamegundua soko la Kyela ni kubwa. Tunaamini wana Kyela wengi wamefaidika.Mpango wa baadaye ni kuungana na wana Kyela wengine kufungua bank ya wana Kyela ili wananchi waweze kujipatia mikopo na ushauri wa uhakika kwa faida yao .

7. George Ulaya ana kazi ya maana sana na ambayo kipato chake ni zaidi ya mara mbili ya ubunge.familia ilikuwa inataka aendelee kukaa huko na kuachana na siasa za majungu huku nyumbani. Lakini George ameamua kurudi baada ya usanii wa Mheshimiwa na amekubali pato lake litashuka sana lakini yuko tayari kuwatumikia wana Kyela kwa moyo wote kama ambavyo ameweza kuitumikia familia yake kwa muda mfupi na mpaka kufanikiwa kufungua kampuni kama KBC kwa kutumia pesa zake kwa miaka 10 tu ambayo amekuwa kazini.

8. George anataka kuzibadili shule na hospitali hasa ya Kyela ili ziwe za kisasa, kununua na kuomba vifaa kama magari ya wagonjwa na mashine za kutibia kutoka sehemu mbalimbali. Pia kuleta watu wa kujitolea kutoka nje kusaidia shule na hospitali ili ziwe na ubora na kupunguza vifo vya watoto na wanawake kama ilivyo sasa. George anataka kukomesha mambo ya kwenda Igogwe na Tukuyu kutibiwa, badala yake hospitali zetu zitakuwa bora hata zaidi.

9. George hataki ukubwa na muda wote anaishi maisha ya kawaida. Hahitaji
Shangingi na pesa za shangingi akipata anataka zitumike kununua magari ya wagonjwa kwa faidi ya jamii yote.

10.George amesaidia kuwaamsha vijana wa Kyela kwa kuwaletea ukumbi wa kisasa, kuona mipira kwenye TV kubwa na mpaka sasa vijana wa Kyela hawababaishwi tena na vijana wengine toka Dar. Huko mbele anataka kuimarisha huduma zingine mbalimbali kwa faida ya Kyela.

11. Kupitia KBC vijana wote wamekuwa wakipata vibarua KBC na kupata mahitaji yao muhimu. Lengo huko mbele ni kuimarisha ajira kwa vijana. Kwamba huko mbele anataka kusimamia mafunzo ya VETA na kuwapa vijana misaada ili wakajiajiri mijini, kuwasaidia vijana wanaotaka kujiunga na jeshi. Atakuwa wa kwamza kwenda kumpigia magoti Mwamunyange ili vijana zaidi waende jeshini, pia atasaidia vijana kujiunga na jeshi la polisi.

12.George anataka kurudi kwasababu ana uchungu na Kyela, anataka kusaidia Kyela akiwa bado kijana na nguvu zake badala ya kurudi uzeeni. Anataka wote waliosoma na kubaki Dar wawe na uhusiano na nyumbani, wajenge nyumbani, wasaidie nyumbani, matokeo yake vijana watapata kazi huku nyumbani. Waambie George anataka kuwasiliana na kila mwana Kyela ili kuwashawishi wafanye kitu chochote nyumbani ikiwemo kuwasaidia wazazi wao na wadogo zao.

13. Mheshimiwa hana uchungu na Kyela na alikuja Kyela baada ya kuwaogopa wale maprofesa kule Rungwe. Ndio maana muda wote anashinda Tukuyu.

14. Mheshimiwa anapoteza muda na Wachaga ambao wameendelea zamani huku kwake hakuna kitu, vijana wanahangaika bila ajira. Kwamba yeye Mwakyembe anachotaka ni uwaziri ndio maana kila sehemu anazunguka na waandishi wa habari ili wakuze jina lake.

15. Hata vita vya ufisadi na Richmond , data nyingi alipewa na akina George kutoka kwenye mitandao yao . mitandao ndio iliibua Richmond . Mwanzoni bunge walipuuza lakini watu wa mitandao wakazidisha nguvu na kutoa scandal zao mpaka bunge lilipokubali kuchunguza. Waambie George ni mdau mzuri kwenye mitandao ya Watanzania inayopinga ufisadi na viongozi wabaovu.

16. Mheshimiwa amekuwa mbunge miaka 9. ikiwa ni pamoja na bunge la East Afrika lakini hakuna alichofanya Kyela na badala yake kajenga jumba kubwa Dar ambali ni la anasa kuliko majumba ya mafisadi. Kwamba hata nyumba ya kwao Ikolo yeye hakai, ile alijenga ili tu kuwadanganya wana Kyela kwamba anatoka Kyela.

17. Mheshimiwa anakosana na kila mtu, hata George hakutaka kugombea sasa lakini Mheshimiwa anatumia ubunge wake kuikwamisha hata KBC. Alitumia akina Kifukwe kukwamisha CRDB kufungua branch KBC, alijaribu kuzuia radio isije Kyela na anapinga vijana wanaotaka kuendeleza Kyela.

18. Badala ya kuwapelekea wananchi maendeleo yeye anapeleka disco ili wacheze na kuambukizana ukimwi zaidi.

19. Anapenda makuu, daraja lililojengwa na jeshi tayari analiita daraja la kwake. Nyerere aliongoza miaka yote bila hata nyumba moja kuitwa jina lake. Angalau hilo daraja angeita daraja la Mwamunyanga.George hataki kabisa kutukuza jina lake na badala yake anatukuza Kyela, ndio maana kwenye kila kitu ameweka Kyela badala ya jina lake.

20. Mheshimiwa ameshindwa hata kushughulikia suala la maji na mabomba ya Wascandinavia badala ya kushughulikia ili yatoke maji, yeye ameyaacha na anashinda Dar, hajui hata Kyela kuna tatizo gani. Wapambe zake kazi kupeleka umbea tu."

USHAURI WA BURE KWA MWAKALINGA:

(1) Katika siasa, jifunze kuepuka "personal attacks" ambazo ni rahisi wewe mwenyewe kugeuziwa kibao maana historia yako George mwenyewe ina mushkeri kidogo. Tusibishane, tumesoma wote! Mwakalinga kumbuka daima kuwa: "Ukiwa unaishi kwenye nyumba ya kioo, achana na tabia ya kutupia mawe watu wengine!" Mwongozo au hoja namba 1 hapo juu, achana nayo kabisa maana inaongelea mambo ya UDSM ambako George hukumaliza masomo!

(2) Hoja namba 13-20 ni hoja za chuki binafsi za Mwakipesile zinazotukuza ukabila na majungu na kuwaingiza watu wengine (akina Kifukwe n.k.) kwenye suala lisilowahusu. George ndugu yangu : NENDA KWENYE HOJA"!

(3) Ukirejea tena Bongoland, epuka takrima na events za kuchinja ng'ombe n.k. nyama hiyo itakujakutokea puani! Alfred (unamfahamu) anasema mlichinja ng'ombe kuwafanyia karamu wananchi wa Kata ya Katumba Songwe unakotoka. Leo kakulinda Mwakipesile, kesho hatakuwepo!

(4) Ulitoa kauli Katumba Songwe kuwa umetumwa kumwondoa Mwakyembe. Pengine mwenzetu amekaa mno Ulaya! Hoja kama hiyo ni suicidal mbele ya safari!

(5) There are times brother unajisahau sana na kuwatetea akina Lowassa, Rostam na Mwakipesile ili mradi unamponda Mwakyembe. Staili hii kwa Kyela na sehemu zingine Tanzania ni kujimaliza mwenyewe!

(6) Achana na wapigadebe wa Mwakipesile, tafuta wa kwako! Hizo ndo real politics. Pengine huelewi kuwa Mwakipesile kapoteza kabisa mvuto wa kisiasa Kyela, pamoja na wafuasi wake wote! Ukikaa karibu sana nao,na wewe utaambukizwa ugonjwa huo wa kukosa mvuto! Utaambukizwa madhambi yao!

(7) Ni vema kumjua mshindani wako! Mwakyembe, utake usitake, ni msomi mzuri kukupita na alipata kura asilimia 93 uchaguzi uliopita. Suala la msingi hapa ni kushusha kukubalika kwa Mwakyembe kufikie angalau asilimia 45 ili bnrother uweze kupeta. Usiendeshe kampeni as if unashindana na mgeni mwenzako kwenye siasa!

( Kumbuka - huwezi kumshinda Mwakyembe kwa hoja za jumla jumla ambazo wananchi wana majibu nazo. Kwa mfano, huwezi kusema hakuna maendeleo ya elimu wakati taarifa za Serikali zinasema: mwaka 2005 kulikuwa na shule nane ( tu za Sekondari za Serikali na sasa ziko shule 23 za Sekondari za Serikali. Shule ya 23 ya Ndobho inamaliziwa!

-Huwezi kumshinda Mwakyembe kwa kuongelea nyumba yake Dar es Salaam wakati wewe unaishi London!

-Huwezi kumshinda Mwakyembe kwa kumlaumu ati ana dereva Mchagga badala ya Mnyakyusa (ingawa Msuya ni Mpare), huo ni ukabila! Kama ni hivyo mbona unawatukuza akina Lowassa na Rostam ambao siyo Wanyakyusa? Mbona akina Mwandosya na Mwakyusa wana madereva wasio Wanyakyusa?

-Huwezi kumshinda Mwakyembe kwa kuongelea daraja moja tu wakati madaraja mapya zaidi ya saba yamejengwa katika kipindi chake, na hilo moja unaloliongelea Mwakalinga, Jeshi lenyewe lilitoa tamko (wewe ukiwa London ukila kuklu kwa mrija) kuwa liliombwa na Mbunge wa Kyela. Ndiyo maana hata Mwakipesile alizuiwa na Jeshi kulifungua!

- Huwezi kumshinda Mwakyembe kwa kusema aligombea ubunge (mwongozo na.13) kwa kumwogopa Mwandosya na Mwakyusa. Hoja hiyo ni ya kitoto na haiingii akilini kwa kuwa kila mtu, anayeishi Tanzania, anajua kuwa marafiki wakubwa wa Mwakyembe ni Mwandosya na Mwakyusa!

- Huwezi kumshinda Mwakyembe kwa kutunga ngonjera kwenye JF za kumtukana. Unapoteza muda, stick to issues man! Ndiyo maana mpaka leo jamaa hajakujibu wala kusema lolote kuhusu wewe. Amekuacha ujimalize mwenyewe!

Safari Njema!
 
Katika siasa, jifunze kuepuka "personal attacks" ambazo ni rahisi wewe mwenyewe kugeuziwa kibao maana historia yako George mwenyewe ina mushkeri kidogo. Tusibishane, tumesoma wote! Mwakalinga kumbuka daima kuwa: "Ukiwa unaishi kwenye nyumba ya kioo, achana na tabia ya kutupia mawe watu wengine!" Mwongozo au hoja namba 1 hapo juu, achana nayo kabisa maana inaongelea mambo ya UDSM ambako George hukumaliza masomo!

Thanks mazee, kumbe ndo Kisa cha Kukimbilia Poland.....mwaga data kachokoza nyuki kwenye mzinga akitegemea mbio.....
 
Fataki,

Ujumbe wako umekaa kimashaka-mashaka.

Mwakalinga alimazia UDSM na utaratibu wa masomo wakati huo ni kuwa ilikuwa inabidi wanafunzi wa kilimo wahamie SUA - Morogoro. Na hapo akahamia SUA kama unavyoona kwenye historia yake na huko ndiko akaacha na kwenda zake Poland.

Hayo maelezo yako hapo juu ni USHAURI mzuri. Ila umetumia Mwongozo alioandika Mwakipesile (nina imani kambi ya Mwakyembe wameubadilisha kidogo ili uwe mtamu kwa wapinzani wa Mwakalinga) na kuutuma hapa. Sasa umeandika MANENO kibaoo wakati hayo Mwakalinga hajaandika wala hajaagiza waandike. Sasa hivi Wapinzani wa Mwakyembe wanajipa kazi ya kumpigia debe Mwakalinga, na hii si kuwa WANAMPENDA, la hasha. Wao wanataka kumuondoa Mwakyembe. Hata kama ungelikuwa wee FATAKI, basi wangelikupigia kura. Hata kama ni Lowassa au RA, bado wangelimpigia debe. Hilo lipo kama umeme unapopita, basi kunatokea Magnetic field. Au gari linapopita kwenye barabara za vumbi, vumbi hutimka.

Kama kweli wataka kumwandikia ushauri, basi soma jumbe zake za zamani, mfahamu ni mtu wa aina gani na hapo sasa muandikie ushauri wako. Kwa leo nakujibu kwa heshima sana msomi wetu.

NB: Kwa taarifa yako ni kuwa USHINDI wa Mwakyembe ulijumuisha msaada wa Mwakalinga. Mdogo wake Mwakalinga alikuwa na Mwakyembe from day 1 ya kampeni. Zaidi nikuambie kuwa Mwakyembe na Mwakaliga, wanafamiana zaidi ya unavyodhani. Sasa ukisikia Mwakipesile anamsaidia Mwakalinga, aliyesaidia kumtoa kwenye ubunge, INAINGIA AKILINI??
 
You betcha



Wow ... kwa hiyo unasimama na Masha sasa. Kwa hiyo ufisadi wa Masha ni majungu tu ya watu kama mimi?

Hili ni jipya hapa jamvini (haichukui muda kuleta yote uliyoandika hapa baada ya Masha kuonekana fisadi na mchovu).



Na huyo mnafiki anayeuma huku na huku ni nani? Unaweza kumtaja?




Haya bado ni maneno yako binafsi ... sio ukweli mtupu au sio?



Yeah, advantage nyingine ya George ni kuungwa mkono na mafisadi. Kama vile mafisadi wa serikali ya Kikwete walisema kuwa kelele za wapinzani wake ni kelele za mlangoni, sitashangaa George naye akisema the same thing - ndege wenye mabawa yanayofanana huruka pamoja



Ushauri mzuri sana huu kwa George, wapuuzie wana JF kwa vile wao hawaamui nani awe mbunge wa Kyela. Kama vile Kikwete na Mramba na Lowasa na Rostam Azizi wanavyotakiwa kuwapuuzia wana JF kwa vile sio wao tu wanaoamua nani awe mbunge au kiongozi wa serikali.

Respect kwako pia

- Mkuu ninakusikia sana, ila I am looking forward kuona mijadala yenye masilahi kwa wananchi wa jimbo la Kyela, ninasubiri kusikia vision ya George, maana ya DK ninaifahamu tayari katika miaka kumi ya ubunge wake toka EAC, mpaka huko Kyela hasa zaidi taifa. Ninaiheshimu sana kazi yake kwa taifa letu, lakini lazima niwe mkweli sijui chochote kuhusu kazi yake jimboni, zaidi ya kuwaisikiliza sana hao maluteni wake, wawili.

- George, itafika wakati itabidi aseme kujibu maswali muhimu kwamba ni kwa nini anataka ubunge wa Kyela na sio jimbo lingine?, kwa nini anataka kumtoa mbunge shujaa wa taifa kama DK? kwa nini anafikiri anaweza kuwapelekea Kyela mazuri kuliko mbunge wao wa sasa? Je mbunge wa sasa amefanya mangapi mazuri na mangapi mabaya? Kama mbunge shujaa kama DK ameshindwa yeye atawezaje? Na maswali mengine mengi muhimu kwa taifa pia, ni majibu ya maswali kama haya ndio yatawasadiai wananchi Kyela na sisi wengine, kuliko hizi lows ninaziona humu.

- Kampeni hazijaanza, lakini hii tunaita part gazeti au trailer imeshaanza, na heshima kwa George kwa kuli-freeze taifa na JF for almost a week sasa, saafi sana na ataingia kwenye vitabu vya historia ya taifa kwa ujasiri wa kusimama na kusimamia principles. Ndio maana huko nyuma nilisema kwamba huu uchaguzi utakua wa Century na watakaofaidika ni wananchi wa Kyela hivi vichwa viwili vikitwangana.

- La George kuwa fisadi, bado ninalikataa sijaona sababu ya msingi, kama ni kukutana alianza kukutana na the right hand man wa DK, tena aliyemfuata London, silioni hili likipigiwa kelele hapa, Mwakipesile hamjui George, lakini yes ni adui namba moja wa DK, sheria haimzuii kumshabikia George na hata kumfanyia kampeni on his own ili kushindana na adui wake hilo linaeleweka, kwamba eti George anahusika directly na Mwakipesile au Lowassa, nimewauliza sana wale watu wa DK, ambao binafsi ninawaaminia sana inapokuja masuala ya kampeni za DK na George huko Kyela, infact mmojawao alinihakikishia kuwa George akimshinda mtu wake DK, basi yeye atahamia Malawi na kuomba uraia huko, now that is deep royalty kwa kiongozi, as opposed na hizi blah blah humu,

- Alisema alisikia kuwa George anajenga bara bara ya lami Kyela kwa kusaidiwa na mafisadi, hasa Lowassa lakini alikwenda haraka sana huko na kuhakikisha kwamba sio kweli, na nimamumini sana huyu aliyeniambia haya, sasa hawa wawili wakiniambia kwamba George ameanza kuwa fisadi basi wala sina sababu ya kumuuliza George kama ni kweli au uongo, hawa ni watu tunaheshimiana sana, so far wamesema mengi mazuri na mabaya ya George as a candidate wa jimbo lao, lakini la kushirikiana na mafisadi hawajalisema na ninawaamini sana hasa inapokuja interest ya uongozi wa
DK huko jimboni.

- Ushauri wangu kwa George, ni do not panic maana sasa umeingia siasa za taifa na hasa kwa kumgusa shujaaa wa taifa, haya ya JF ni madogo sana kulinganisha na ya mbele zaidi, hizi za JF ni za kawaida ingawa kuna mengine ni mazuri sana kwake kuyakariri, hasa ule ushauri wa Dilunga kwamba ifike time George ndiye awe the owner wa message yake na awe muangalifu sana na vibaka. Huna sababu yoyote ya kuhangaika kujibu hizi shutuma zisizo na kichwa wala miguu, be yourself watu ni watu tu maana ukiingalia vizuri sana hii thread utajionea mwenyewe some of the so called you "friends" wakivua ngozi zao rasmi, ndio maana hata viongozi wetu huteseka sana na siasa zetu Tanzania maana this is how we are, lakini yasikusumbue yachukulie kama changamoto.

Miwsho I am looking forward kuiona na binafsi kushiriki mijadala serious kwa ajili ya wananchi wa Kyela, pindi tu hizi blah blah zikiisha, zitaisha tu karibuni si unajua sisi wabongo na kipya kinyemi, soon tuta get down to serious business, otherwise ninamtakia safari njema kurudi "nyumbani" na pia ninamuombea sana kwa Mungu DK, amsalimishe na majaribu ya waovu wasiomtakia mema na ninawaombea sana wananchi wa Kyela kuwa waangalifu katika kutafakari hii situation, ambayo kama hawako makini itawaletea kimbembe sana, maana this thing is for real.

Mjadala mwema wananchi wenzangu wa JF, ila hapa ninaweka kalamu chini na huu mjadala. Na JF idumu where we dare! nafikiri hata George atajionea mwenyewe humu nyani alivyopigwa giladi, tena bila kumuangalia usoni ikiwa mchana kweupeee! I love JF!

Respect.

FMEs!
 
Thanks mazee, kumbe ndo Kisa cha Kukimbilia Poland.....mwaga data kachokoza nyuki kwenye mzinga akitegemea mbio....

Masa
Mwakalinga alisoma agricultural engineering..tafuta utaratibu wakati huo ilkuwaje,alimaliza UDSM na akaenda sokoine badaye akatimkia Poland
 
Ufisadi unaanza na fikra halafu vitendo. Ila huwezi kukataa kwamba wewe sio fisadi wakati tayari umesha anza kutumia fedha za kifisadi, na kama fedha hizo ndizo zinakupeleka dodoma then hilo ni zao la kifisadi linakwenda kutimiza wajibu wa mafisadi na kutetea mafisadi kusafisha mafisadi na kushiriki ufisadi. Tusitegemee mtoto wa chatu atakuwa kondoo.

Ukiangalia washiriki, washauri, na wale wote wapambe wa karibu wa huyu mmbunge wenu mtarajiwa ni wale mapapa wa ufisadi. Je kwenye ile pay back debt collection iliyoanzishwa uingereza kwa kufungua makampuni hewa yakijifanya yanaidai tanzania na kuiibia nchi fedha nyingi za kigeni watu wakishirikiana na kundi la mafisadi waliopo nchini ni wangapi walishiriki wakiwa ndani na nje ya nchi. Kweli ndoa hii yaweza kuvunjwa hasa pale wanapotaka kujenga kibanda???????????????

Ama kweli mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, basi na masikini aibiwe ila si mpaka kumvunjia kibanda chake .......
 
USHAURI WA BURE KWA MWAKALINGA:
Ndiyo maana mpaka leo jamaa hajakujibu wala kusema lolote kuhusu wewe. Amekuacha ujimalize mwenyewe!
Safari Njema
!

- Ahsante sana mkuu FATAKI, loud and clear kwa wenye masikio na macho kama mimi, duh Fataki bwana baabu kubwa!

Respect.

FMES!
 
kalengamab said:
6. Huko nyuma alipoona wana Kyela wanahangaika kwenye mikopo aliweza kuwashawishi PRIDE kutoka Tukuyu ili waje Kyela. Na mpaka leo PRIDE wanashukuru maana wamegundua soko la Kyela ni kubwa.
Sometimes the Best Man for the job is a Woman! Loh! jamani jamani, kalengamab kwa hoja hapo juu unanadisha, unauza au unamsiliba George aonekane mshirika wa makupe na wanyonyaji?!
 
Naomba mwongozo, hivi ni kweli Mwakalinga alienda Arusha-Munduli kukutana na Lowassa, na kama ni kweli je yeye ndiye kundi la hao ambao walimtuma?

Mimi si-kwamba nataka kumchafua Mwakalinga ila nachotaka ni kuweka mambo sawa na ku-vet mtu ambaye anafaa kwa ajili ya Tanzania na watanzania ambao tmekuwa tukilia na kuliwa urithi wetu na kundi dogo.

Ni ukweli kwamba kundi la mafisadi wamepanga kuingiza mamluki wao bungeni kwa ajili ya mambo yao.

sasa Mwakalinga tayari yupo karibu sana na hao mafisadi, ndio wanaomsaidia na ndio washauri wake. Kinachoniuma zaidi sote tumekuwa tukipiga kelele kuhusu hawa mafisadi na tukitaka wasulubiwe.

Sasa mizizi ya ufisadi imeota na imetapakaa kweli kweli. Ni lazima tuelezane ukweli mapema kwani tusipokata kizazi fisadi jitihada zetu zitakuwa za bure.

Mwakalinga njoo weka uhusiano wako na akina Lowasa na nini mlikubaliana Uingereza na huko Arusha. Je nia yao na yako nini, ni vingapi tayari mmeshirikiana kuliangamiza taifa la watu masikini, je fedha unazotumia kwenye kampeni sizo rasmi zimetoka wapi? Kumbuka ufisadi ni utashi na kama unao kwishnei.
 
Suleiman Daudi,

Pole sana Mkuu kama una shida na uandishi huu.

Nimeamua nikijibu kwa kuona kuwa wee utakuwa mgeni bado na hapa JF kuna kitu kinaitwa KUSOMA NDANI YA MISTARI. Ntaomba sana tena sana uanze kuzoea uandishi wangu. Huwa mara nyingi ninachanganya mchele na Pumba. Mwakalinga ananifahamu kwa hilo na huwa hapati shida na huu mwendo wangu.

Mara nyingi nikiona mtu kaandika UPUPU, basi na mie huwa namjibu UPUPU. Hamna haja ya kumuelewesha mtu anayeanza kwa kusema NASIKIA na baadaye anaaanza kushutumu.

Haya maneno yako ya mwisho kuwa WAZEE wa Kyela watafute pamba, kwa leo nayaacha bila comment kwa sababu tu naona wee bado mgeni. Na ndiyo maana nakuandikia ujumbe wa heshima namna hii.

Kwa Taarifa yako mie naitwa Mwana Itimba wa Sikonge. Mwakalinga George yuko UK anakofanya kazi na ambaye nafikiri umesoma kuwa yuko safarini leo kwenda UK kutoka Tanzania kwa likizo. Ukifuatilia vizuri makala ya Mwakalinga kugombea UBUNGE na jinsi ilivyoshabikiwa hiyo makala, utagundua UMAARUFU na busara za jamaa. Vinginevyo, watu wasingekaliana kooni namna hiyo.

Kama ndiyo ningelikuwa mie hapa Mnyamwezi nataka kugombea na Mwakyembe jimbo la Kyela, hata kama mafisadi wangelikuwa wamenipa pesa, unafikiri Genge la wapinzani lingelikuwa kubwa namna hiyo? Kama kuna mtu kasababisha watu wajadili jumbe nyingi namna hiyo kwa siku moja, basi lazima ujuwe kuwa jamaa kajiandaa vizuri. Labda kwa taarifa yako lazima ujuwe kuwa wapambe fulani walikaa na kuamua kumtuma mtu aende hadi UK kwenda kumuomba jamaa asigombee ubunge. Kama angelikuwa mtu wa kaundika pumba kama zangu, basi asingeliwanyima jamaa usingizi.

Nafikiri umenielewa na utaendelea kufaidi hizi habari ambazo wengine milele tunaziandika nusu siriasi na nusu joki.

Mkuu Sikonge,

asante kwa maelezo mazuri na asante kwa kunikaribisha. Nitakubali kutofautiana nawe kuwa lugha kama hiyo uliyotumia hapo ambayo kwa namna moja au nyingine unaengelea gender ya mtu kwa namna ya udhalilishaji (kikwapa cha msichana) sidhani kama inalingana na maandishi yanayosomeka kwenye moja ya threads hapo juu zilizo-stick.

Huwezi kuwa kwa upande mmoja unaomba watu kulichukulia jamvi hili siriasi lakini kwa wakati huo huo wewe ukiwa mmoja wa wale wanaolidhalilisha. Kama hiyo ndiyo njia mpya ya kuchangia hapa JF, basi nitaungana nawe kuendeleza jokes na utani na matusi muda mwingine ili kufurahisha baraza. Lakini kama nia ni kujenga forum yenye nguvu, basi lugha za udhalilishaji kama hizi sioni kama zinafaa kuendelezwa.

Nakubaliana kutofautiana nawe kwenye hili.
 
Fataki,

Ujumbe wako umekaa kimashaka-mashaka.

Mwakalinga alimazia UDSM na utaratibu wa masomo wakati huo ni kuwa ilikuwa inabidi wanafunzi wa kilimo wahamie SUA - Morogoro. Na hapo akahamia SUA kama unavyoona kwenye historia yake na huko ndiko akaacha na kwenda zake Poland.

Hayo maelezo yako hapo juu ni USHAURI mzuri. Ila umetumia Mwongozo alioandika Mwakipesile (nina imani kambi ya Mwakyembe wameubadilisha kidogo ili uwe mtamu kwa wapinzani wa Mwakalinga) na kuutuma hapa. Sasa umeandika MANENO kibaoo wakati hayo Mwakalinga hajaandika wala hajaagiza waandike. Sasa hivi Wapinzani wa Mwakyembe wanajipa kazi ya kumpigia debe Mwakalinga, na hii si kuwa WANAMPENDA, la hasha. Wao wanataka kumuondoa Mwakyembe. Hata kama ungelikuwa wee FATAKI, basi wangelikupigia kura. Hata kama ni Lowassa au RA, bado wangelimpigia debe. Hilo lipo kama umeme unapopita, basi kunatokea Magnetic field. Au gari linapopita kwenye barabara za vumbi, vumbi hutimka.

Kama kweli wataka kumwandikia ushauri, basi soma jumbe zake za zamani, mfahamu ni mtu wa aina gani na hapo sasa muandikie ushauri wako. Kwa leo nakujibu kwa heshima sana msomi wetu.

NB: Kwa taarifa yako ni kuwa USHINDI wa Mwakyembe ulijumuisha msaada wa Mwakalinga. Mdogo wake Mwakalinga alikuwa na Mwakyembe from day 1 ya kampeni. Zaidi nikuambie kuwa Mwakyembe na Mwakaliga, wanafamiana zaidi ya unavyodhani. Sasa ukisikia Mwakipesile anamsaidia Mwakalinga, aliyesaidia kumtoa kwenye ubunge, INAINGIA AKILINI??

Hii Mkuu Sikonge,

Inabidi hapa nikubali kuwa unamfahamu sana huyu Mwakalinga. Nilikuwa naona kama unatania kwa kujitaja kuwa wewe ndiye Mwakalinga ila baada ya kusoma haya, imebidi nikubali kuwa mwenzangu unamfahamu vilivyo sana huyu ndugu. Ni vizuri sana kustick na mwenzako ambaye yaonekana unakila linalohitajika kwa ufahamu wa maisha yake ya shule na kikazi.
 
Fataki,
Mkuu shukran sana tena basi inabidi Mwakalinga akusome na akuelewe kwamba unamtakia mema na sii kinyume.. Kwa wanao kusoma vinginevyo ndio tunarudi kule kuleeeee - sisi Miafrika Ndivyo Tulivyo.
 
(7) Ni vema kumjua mshindani wako! Mwakyembe, utake usitake, ni msomi mzuri kukupita na alipata kura asilimia 93 uchaguzi uliopita. Suala la msingi hapa ni kushusha kukubalika kwa Mwakyembe kufikie angalau asilimia 45 ili bnrother uweze kupeta. Usiendeshe kampeni as if unashindana na mgeni mwenzako kwenye siasa!

(8) Kumbuka - huwezi kumshinda Mwakyembe kwa hoja za jumla jumla ambazo wananchi wana majibu nazo. Kwa mfano, huwezi kusema hakuna maendeleo ya elimu wakati taarifa za Serikali zinasema: mwaka 2005 kulikuwa na shule nane (8) tu za Sekondari za Serikali na sasa ziko shule 23 za Sekondari za Serikali. Shule ya 23 ya Ndobho inamaliziwa!

-Huwezi kumshinda Mwakyembe kwa kuongelea nyumba yake Dar es Salaam wakati wewe unaishi London!

-Huwezi kumshinda Mwakyembe kwa kumlaumu ati ana dereva Mchagga badala ya Mnyakyusa (ingawa Msuya ni Mpare), huo ni ukabila! Kama ni hivyo mbona unawatukuza akina Lowassa na Rostam ambao siyo Wanyakyusa? Mbona akina Mwandosya na Mwakyusa wana madereva wasio Wanyakyusa?

-Huwezi kumshinda Mwakyembe kwa kuongelea daraja moja tu wakati madaraja mapya zaidi ya saba yamejengwa katika kipindi chake, na hilo moja unaloliongelea Mwakalinga, Jeshi lenyewe lilitoa tamko (wewe ukiwa London ukila kuklu kwa mrija) kuwa liliombwa na Mbunge wa Kyela. Ndiyo maana hata Mwakipesile alizuiwa na Jeshi kulifungua!

- Huwezi kumshinda Mwakyembe kwa kusema aligombea ubunge (mwongozo na.13) kwa kumwogopa Mwandosya na Mwakyusa. Hoja hiyo ni ya kitoto na haiingii akilini kwa kuwa kila mtu, anayeishi Tanzania, anajua kuwa marafiki wakubwa wa Mwakyembe ni Mwandosya na Mwakyusa!

- Huwezi kumshinda Mwakyembe kwa kutunga ngonjera kwenye JF za kumtukana. Unapoteza muda, stick to issues man! Ndiyo maana mpaka leo jamaa hajakujibu wala kusema lolote kuhusu wewe. Amekuacha ujimalize mwenyewe!
Safari Njema!
point tupu........
 
USHAURI WA BURE KWA MWAKALINGA:

(1) Katika siasa, jifunze kuepuka "personal attacks" ambazo ni rahisi wewe mwenyewe kugeuziwa kibao maana historia yako George mwenyewe ina mushkeri kidogo. Tusibishane, tumesoma wote! Mwakalinga kumbuka daima kuwa: "Ukiwa unaishi kwenye nyumba ya kioo, achana na tabia ya kutupia mawe watu wengine!" Mwongozo au hoja namba 1 hapo juu, achana nayo kabisa maana inaongelea mambo ya UDSM ambako George hukumaliza masomo!

(2) Hoja namba 13-20 ni hoja za chuki binafsi za Mwakipesile zinazotukuza ukabila na majungu na kuwaingiza watu wengine (akina Kifukwe n.k.) kwenye suala lisilowahusu. George ndugu yangu : NENDA KWENYE HOJA"!

(3) Ukirejea tena Bongoland, epuka takrima na events za kuchinja ng'ombe n.k. nyama hiyo itakujakutokea puani! Alfred (unamfahamu) anasema mlichinja ng'ombe kuwafanyia karamu wananchi wa Kata ya Katumba Songwe unakotoka. Leo kakulinda Mwakipesile, kesho hatakuwepo!

(4) Ulitoa kauli Katumba Songwe kuwa umetumwa kumwondoa Mwakyembe. Pengine mwenzetu amekaa mno Ulaya! Hoja kama hiyo ni suicidal mbele ya safari!

(5) There are times brother unajisahau sana na kuwatetea akina Lowassa, Rostam na Mwakipesile ili mradi unamponda Mwakyembe. Staili hii kwa Kyela na sehemu zingine Tanzania ni kujimaliza mwenyewe!

(6) Achana na wapigadebe wa Mwakipesile, tafuta wa kwako! Hizo ndo real politics. Pengine huelewi kuwa Mwakipesile kapoteza kabisa mvuto wa kisiasa Kyela, pamoja na wafuasi wake wote! Ukikaa karibu sana nao,na wewe utaambukizwa ugonjwa huo wa kukosa mvuto! Utaambukizwa madhambi yao!

(7) Ni vema kumjua mshindani wako! Mwakyembe, utake usitake, ni msomi mzuri kukupita na alipata kura asilimia 93 uchaguzi uliopita. Suala la msingi hapa ni kushusha kukubalika kwa Mwakyembe kufikie angalau asilimia 45 ili bnrother uweze kupeta. Usiendeshe kampeni as if unashindana na mgeni mwenzako kwenye siasa!

( Kumbuka - huwezi kumshinda Mwakyembe kwa hoja za jumla jumla ambazo wananchi wana majibu nazo. Kwa mfano, huwezi kusema hakuna maendeleo ya elimu wakati taarifa za Serikali zinasema: mwaka 2005 kulikuwa na shule nane ( tu za Sekondari za Serikali na sasa ziko shule 23 za Sekondari za Serikali. Shule ya 23 ya Ndobho inamaliziwa!

-Huwezi kumshinda Mwakyembe kwa kuongelea nyumba yake Dar es Salaam wakati wewe unaishi London!

-Huwezi kumshinda Mwakyembe kwa kumlaumu ati ana dereva Mchagga badala ya Mnyakyusa (ingawa Msuya ni Mpare), huo ni ukabila! Kama ni hivyo mbona unawatukuza akina Lowassa na Rostam ambao siyo Wanyakyusa? Mbona akina Mwandosya na Mwakyusa wana madereva wasio Wanyakyusa?

-Huwezi kumshinda Mwakyembe kwa kuongelea daraja moja tu wakati madaraja mapya zaidi ya saba yamejengwa katika kipindi chake, na hilo moja unaloliongelea Mwakalinga, Jeshi lenyewe lilitoa tamko (wewe ukiwa London ukila kuklu kwa mrija) kuwa liliombwa na Mbunge wa Kyela. Ndiyo maana hata Mwakipesile alizuiwa na Jeshi kulifungua!

- Huwezi kumshinda Mwakyembe kwa kusema aligombea ubunge (mwongozo na.13) kwa kumwogopa Mwandosya na Mwakyusa. Hoja hiyo ni ya kitoto na haiingii akilini kwa kuwa kila mtu, anayeishi Tanzania, anajua kuwa marafiki wakubwa wa Mwakyembe ni Mwandosya na Mwakyusa!

- Huwezi kumshinda Mwakyembe kwa kutunga ngonjera kwenye JF za kumtukana. Unapoteza muda, stick to issues man! Ndiyo maana mpaka leo jamaa hajakujibu wala kusema lolote kuhusu wewe. Amekuacha ujimalize mwenyewe!
Safari Njema!
He he he.
Kweli wewe ni fataki.

Hayo madaraja saba ulijenga wewe?
 
MWAKYEMBE KUCHINJA NG'OMBE KILA KATA.

Mbunge wa Kyela Harison Mwakyembe kwa kushirikiana na jamaa zake wenye ufinyu wa mawazo Ally Kinanasi (Shemeji wa wilaya) na Emmanuel Mwamulinge (Kinundu) watapita kila kata huku wakichinja ng'ombe na kula na wananchi kwa lengo la kuubadili upepo mkali unaomkabili

Habari zilizotapatikana sasa hivi hapa mjini kyela zinasema, upepo sio mzuri tena kwa mheshimiwa huyo baada ya kukimbiwa na madiwani na watendaji wa kata karibia wote wakimtuhumu kwa tabia yake ya kusabisha migongano ndani ya chama na wilaya nzima ya kyela na hivyo maendeleo ya wilaya ya kyela kuzidi kushuka.

Mwakyembe kwa kushirikiana na Ally Kinanasi na Emanuel kinundu,watakuwa wanapita kila kata na kuchinja ng'ombe na huku mwakyembe akisimikwa upya kama chief wa kinyakyusa kwa kisingizio cha kwamba watu wanampa pole na ajali

Habari zinasema mwakyembe ameona upepo sio mzuri kwake na ameona aitumie nafsi ya ajali aliyopata kama kisingizio cha kusafisha jina lake.

Wapambe wa mwakyembe wamekuwa wakikutana kila siku usiku na kukaa kwa muda mrefu huku wakijipanga jinsi ya kununua hizo ngo'mbe kila kata.

Katika mkutano mkuu wa Halmashauri ya ccm wilayani kyela uliofanyika mapema mwaka huu kujadili vurugu, zilizopelekea kupigwa kwa Katibu wa ccm wilaya, Mwakyembe aliambiwa wazi wazi na madiwani kuwa hawamtaki na kama kunauwezakano ajuzuru. Ni mbunge wa kwanza kuambiwa na madiwani kwa kipindi kidogo alichoongoza.

Mwakyembe ana jina kubwa sana kitaifa, lakini hapa wilayani kapoteza dira na mwelekeo. Kikubwa sana ni ile tabia yake ya dharau na kusababisha migongano mingi sana ndani ya jamii ya kyela.
 
He he he.
Kweli wewe ni fataki.

Hayo amdaraja saba ulijenga wewe?

Yalijengwa Mwakyembe kwa kushirikiana na JWTZ(Gen. Mwamunyange)

Na ndio sababu ya Mwakipesile kususia kwenda kwenye ufunguzi wa madaraja hayo.
 
Back
Top Bottom