Niwapeni mchapo mwingine, mujue siasa za Kyela zilipofikia.
Kama mnakumbuka kuna katibu wa CCM wa wilaya alipigwa na vijana baada ya kuwatuhumu kwamba wamehongwa pesa na Mwakalinga kupitia kwa diwani Mahenge (diwani wa Kyela mjini).
Kuna kiongozi mmoja wa chama wa wilaya aliongea na Mwakalinga kwa simu na kumtuhumu kuhusika na hizo vurugu. Mwakalinga akasema yeye hahusiki na wala hawajui hao vijana na pia yeye sio mtu wa kuchochea vurugu na badala yake anaheshimu kutofautiana kwa hoja. Wakashindana hapo, nafikiri huyo kiongozi aliendelea kuamini hivyo.
Sasa juzi, Mwakalinga alikuwa anatoka kijijini kwao, kuja mjini. Diwani Mahenge akawa anaenda kijiji hicho kwenda kukutana na wazazi (yeye pia ni mwenyekiti wa jumuia ya wazazi).
Kijana tuliyekuwa naye kwenye gari letu akasema lile pale mbele ni gari la Mahenge. Ikabidi tusimame na Mwakalinga akateremka. Kwenye gari la Mahenge kulikuwa na watu wawili, aliyekuwa anaendesha gari alikuwa amevaa tisheti na mwingine alikuwa amevaa nguo za CCM.
Mwakalinga bila kujua akaenda kumsalimia yule aliyekuwa amevaa nguo za CCM akidhani ndiye diwani Mahenge. Yule jamaa akasema hapana sio mimi na diwani Mahenge ni huyu, akimwonyesha aliyekuwa amevaa tisheti. Ikabidi Mwakalinga aombe msamaha sana kwa makosa hayo. Mahenge akasema hakuna tatizo.
Kumbe Mahenge akawa amefurahi sana; huyo jamaa aliyekuwa naye kumbe alikuwa katika watu waliokuwa wanasema Mahenge amekutana na Mwakalinga kwa siri mwezi March 2009 na kupewa pesa ambazo zimechangwa na mafisadi. Walipoondoka tu yule jamaa akawa wa kwanza kuomba msamaha na kusema Majungu ya Kyela yamenishinda yaani kumbe wewe ulikuwa hufahamiani na Mwakalinga?
Baadaye hata kiongozi wa CCM ambaye huko nyuma alimtuhumu Mwakalinga akatupigia simu na kuomba msamaha pia. Mwakalinga akamwambia akitaka aangalia hata passport maana Mwakalinga alikuwa TZ mara ya mwisho January 2008.
Hiyo habari ilienea Kyela kwa muda mfupi sana, watu wakaanza kusema wameumbuka kwa uzushi.