Malafyale
Platinum Member
- Aug 11, 2008
- 13,833
- 11,173
Mkuu Jilala,
Kwenye siasa huwa hakuna permanent enemy wala friend, ndio maana Mwakyembe na Mwanjala walikuwa kambi moja mwaka 2005, lakini mwaka huu walikuwa mahasimu. Kwenye siasa kila kitu kinawezekana.
Mimi sijaongelea kutuhumiwa, nimeongelea yale yaliyotokea mbele ya macho ya Mwakalinga hapa JF. Kwa hiyo kwamba alituhumiwa na Mwakipesile na mpaka wakagombana, hilo mimi silijui. Nilichokuwa ninajadili ni yale yaliyotokea kipindi cha kuelekea 2010 hasa baada ya taarifa kuwekwa wazi kwamba Mwakalinga ana nia ya kugombea.
Tuje kwenye hoja ya kuleta mada hapa, unajua mada ikiletwa hapa na ikaanza kujadiliwa na wapambe ndipo maana na umuhimu wa mada huwa unapotea. Ukianza kujadili kitu kwa misingi ya upambe huwezi ukawa na balanced argument. Kwa hiyo dawa yake ilikuwa ni Mwakalinga kuwaomba hao wapambe wake waachane na mada hizo. Kama mtu anafuka pumba kwanini ubishane/ushindane? Itafika mahali watazamaji watashindwa kuelewa yupi mwenye akili timamu na yupi ambaye ana matatizo.
Mfano mdogo, Afande Samweli ametoa maneno mengi sana. Kama mada ya Kadi Fake na ile nyingine ya Mwakalinga kukamatwa zingekuwa bado zipo, ningekuambia kasome maandishi ya Afande Samweli na usome mabandiko ya Malafyale halafu uniambie nani alikuwa mkweli kuliko mwingine na nani alikuwa anajadili mada kiupambe na yupi alikuwa na hoja ambazo ziko balanced.
Unajua ukianza ku-dispute habari alizokuwa anatoa Malafyale na ilihali kuna ushahidi wa mambo aliyoyasema wakati wa kampeni za kura za maoni na kwenye uchaguzi wenyewe na yote yakawa yako sahihi, huwezi kunishawishi niseme kwamba habari alizotoa Malafyale huko nyuma zilikuwa ni za uongo. Kwa hiyo credibility ya Malafyale kwa sasa ni kubwa sana kwa kuwa mambo mengi aliyoyasema kwenye kura za maoni na uchaguzi yamedhihirika kuwa ni ya kweli.
Mwisho umesema kwamba Mwakalinga mwenyewe ndiyo alikuwa analeta taarifa na kukanusha za uongo, labda huko nyuma mwaka 2009, lakini siyo mwaka huu. Kwa hiyo taarifa ya kadi fake ililetwa na Mwakalinga mwenyewe? Ni Mwakalinga pia aliyekanusha kwamba hajakatwa? Ni Mwakalinga mwenyewe aliyekuwa anasema Mwakyembe amekaliwa kooni? Ni Mwakalinga mwenyewe aliyekuwa analeta propoganda za kura za maoni kwamba anaongoza? Labda kama siku hizi Mwakalinga amebadilisha jina hapa JF na inaonekana alikuwa na muda mwingi maana news zake zilikuwa zinamwagika hapa 24/7.
Ninachoweza kuomba radhi wana JF ni kukosea kutaja asilimia ambazo Dr Mwakyembe atashinda kwenye uchaguzi huo,vyanzo vyangu vya habari siku 3 kabla ya uchaguzi vilinituma nitabiri Dr Mwakyembe atashinda kwa kati ya asilimia 75 hadi 80 ya kura zote,lkn ikatokea kashinda kwa karibu ya zaidi ya asilimia 85 ya kura zote,kwa hilo naomba radhi lkn hamna lolote lingine nililokosea kuwapasha wana JF kuhusu siasa za Kyela kwenye kimbembe kile,tofauti kabisa na habari za kutunga kutoka upande ulioongozwa na Afande Samwel kwa jina jipya kama Jilala!
Keil kamaliza kila kitu na sina cha kuongeza zaidi lkn kwa mara ya mwisho nakuambia Jilala ambaye ndiye alikuwa anajiita Afande Samwel aombe radhi wana JF kwa uzushi,uongo,uzandiki,chuki na ufitina wake wa kuelezea siasa za Kyela kama anavyotaka yeye bila kusema ukweli wa mambo halisi ulivyo kwenye kampeni za kumsaka mshindi wa Ubunge kupitia CCM!
Afande Samwel Jilala kuomba radhi kwa habari zako za hovyo hovyo ulizokuwa unatuletea sio dhambi bali ni kielelezo kuwa angalau umekomaa kimaadili,kukataa kuomba radhi hata ilipodhihirika kuwa wewe ni mzushi kunazidi kuharibu image yako hapa
Afande Samwel Jilala,tuombe radhi wana JF ili urudi kundini na uache kutumia jina bandia la Jilala,kuomba radhi ndiyo ubinadamu!