mtwa mkulu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2013
- 8,586
- 11,227
KYELA.
Mwalimu wa shule ya msingi Ngeleka iliyopo Halmashauri ya Busokelo mkoani Mbeya Juma Venance Mhanga, amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela, kulipa faini ya shilingi laki tano pamoja na kuchapwa fimbo 4 baada ya kupatikana na kosa la ubakaji wa binti mwenye umri wa miaka 13.
Hukumu hiyo imetolewa na hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya Wilaya ya Kyela Paul Barnabas Mabula, baada ya kusikiliza kesi ya jinai iliyokuwa ikimhusu mwalimu huyo kudaiwa kumnajisi binti ambaye jina lake limehifadhiwa.
Baada ya kusikiliza pande zote mbili za shauri hilo, Mahakama ya wilaya ya Kyela imeeleza kujiridhisha bila kuacha shaka kwamba mshtakiwa alitenda kosa la kumbaka mtoto (13) ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi Njisi iliyopo wilayani Kyela.
Soma Pia:Mwalimu atupwa jela miaka 30 kwa kumshawishi mwanafunzi amlawiti
Akizungumza baada ya kutolewa kwa maamuzi ya Mahakama, mwendesha mashtaka wa Serikali Wakili Davice Msanga, amesema jamuhuri imeridhika na maamuzi ya mahakama na kutoa mwito kwa jamii hasa wazazi na walezi kujenga ukaribu na watoto wao ili kuwalinda dhidi ya vitendo viovu ikiwemo Ukatili wa kijinsia, ubakaji na ulawiti na kuwafanya watimize ndoto zao.
Naye Bibi wa mhanga wa tulio hilo, ameishukuru Mahakama na wadau kwa ujumla kwa madai kuwa imetenda haki kwani suala hilo lilikuwa likimletea shida.
Bibi huyo amesema amepata funzo la kuwa karibu zaidi na watoto anaowalea na kutokaribisha watu hovyohovyo ili kusaidia kuwalinda watoto.