La Liga: Hatimaye FC Barcelona yachezea kichapo, Messi hakuwepo!

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Mabingwa wa ligi kuu ya soka ya Hispania, almaarufu kama La Liga, jana wamejikuta wakipoteza mchezo wao wa kwanza kwa msimu huu baada ya kupokea kichapo cha mabao 5-4 kutoka kwa klabu ya Levante.

Pamoja na kiungo Phillip Coutinho kufunga mabao matatu, Barcelona walikubali kichapo hicho kutoka kwa Levante waliopo katikati ya msimamo wa ligi hiyo ya Hispania. Katika mchezo huo wa jana, Barcelona waliteremka dimbani bila ya Lionel Messi ambaye hakuwemo hata akiba.

Barcelona wameshaikosa nafasi ya kuweka historia ya kucheza La Liga bila kufungwa. Ingawa tayari wameshatwaa ubingwa, kuikosa rekodi hiyo ni pigo kubwa kwa Barcelona.Huo ulikuwa ni mchezo wa 37 kwa Barcelona.

Katika ligi zote, imebaki Simba SC tu isiyofungwa hadi sasa!
 
Sawa basi mwingizeni messi wenu sw. Mida hii
 
[emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji13]
 

Hapo mwishoni kabisa ulivyoquote ndiyo umenikosha kabisa mkuu
 
Acha kulinganisha Barca na vitu vya ovyo kama Mikia FC.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…