La Liga imeahirishwa moja kwa moja

hamis77

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
13,628
Reaction score
20,992
Ligi Kuu ya Spain La Liga, imehairishwa moja kwa moja msimu huu. FA ya Spain imesema haiwezi kuendelea na msimu huu wa Ligi kwa muda usiojulikana.

La Liga imechukua hatua hiyo, baada ya hapo awali kuisimamisha Ligi kwa muda wa week 2, hatua hii imekuja kutokana na hali ya Maradhi ya Covid -19, yanatokana na virusi vya Corona jinsi ilivyo nchini Hispania.

Taarifa inasema kuwa, Ligi inaweza kurudi pale tu ikiwa Serikali ya nchini Hispania itasema kuwa michezo irejee tena. Ila kwa upande wa La Liga, wameisimamisha moja kwa moja Ligi ya msimu huu.

Timu ya Arsenal wameyafuta mazowezi yao ya timu, waliyoyapanga kuyanza ndani ya Week hii, kutoka na hatarisho la Maradhi ya Covid -19. The Gunnars wamewataka wachezaji wao kuendelea kubakie Majumbani mwao.
 
Mkuu kuahirisha maana yake ni kwamba kutakuwa na marejeo, ukisema kuahirisha moja kwa moja maana yake nini? Ungetumia 'wameahirisha mpaka hapo watakapo tangaza tena'.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo kuna uwezekano ikaanza upya tena lakini si hii kuendelea?
 
Hii habari inayosema la liga imefutwa mazima kwa season hii umeitoa wapi? Mana source zote muhimu zinasema ligi imesimamishwa kwa muda usiojulikana baada ya muda ule Wa awali uliopangwa kutozaa matunda mana hali bado ni mbaya. Na wanasema wanasubiri hadi pale Serikali itaposema Michezo inaweza kuendelea. This means hali ikitengamaa hata mwezi Wa tano au Wa sita hivi ligi itaendelea mana Euro Championship imeahirishwa mwakani
 
Wahairishe na hapa bongo Tu hadi mwakani kama watavyoahirisha EPL
 
Uingereza ilishafutwa kitambo, msimu huu inahesabika hakuna bingwa inaanza upya mwakani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mnatoa wapi habari za kiswahili hizi? Kutokana na UEFA kuahirisha Euro ni wazi lengo lao ni kuzipa nafasi ligi za ndani ili zimalizike. Labda kama corona itaenda hadi mwezi Wa sita na kuendelea ndipo wataweza kufuta ligi
 
Mnatoa wapi habari za kiswahili hizi? Kutokana na UEFA kuahirisha Euro ni wazi lengo lao ni kuzipa nafasi ligi za ndani ili zimalizike. Labda kama corona itaenda hadi mwezi Wa sita na kuendelea ndipo wataweza kufuta ligi
EPL si wamesema inwezekana ikarudi April
 
Ningependa watu waamini hiki ulichokiandika maana upo sahihi ktk kuielezea habari hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…